Uchaguzi 2020 Lissu aifuta CCM Mtwara, Ajenda ya korosho yawa kaa la moto kwa CCM mkoani humo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,231
Hii ndio taarifa inayozunguka kwa sasa kila mahali, kwamba leo yule Rais mtarajiwa wa awamu ya 6 ambaye ameteuliwa na Mungu mwenyewe baada ya kuzuia kifo chake atakuwa Mtwara katika kinachoitwa Uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi 2020 kanda ya kusini.

Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba Shughuli nyingi za kijamii zimesimama na maduka mengi yamefungwa ili kuwezesha kila mtu kuhudhuria Mkutano huo Mkubwa kupita yote iliyowahi kufanyika Mtwara, baadhi ya Makanisa yameamua kufupisha ibada na mengine yamefuta ibada ya mchana ili kuwezesha waumini kuhudhuria tukio hilo adimu.

Kituo kinachofuata - Mtwara ( 741 X 640 ).jpg
Akiongea na wananchi wa Mtwara waliokusanyika maelfu kwa maelfu kumsikiliza, Lissu amekwenda huko na ujumbe dhidi ya unyanyasaji waliofanyiwa wananchi wa huko kwenye ishu ya gesi, korosho na Mauaji ya kutisha huko Mkuranga, Kilwa na Kibiti.

Lissu amemsiliba vilivyo Rais Magufuli kutokana na namna alivyolishughuikia siuala hilo kwa namna ambayo mkulima wa korosho alinyanyasika sana, huku kukiwa na uchukuaji wa korosho kinguvu hali iliyopelekea watu kuwa na maisha magumu ya umasikini hata kufikia hatua ya kukata tamaa kuendelea na kilimo.

Lissu amelinganisha hatua za serikali za CCM kupeleka jeshi kwa watu wa kusini kama kupelekewa vita na serikali yao wenyewe!

Pia Lissu akaelezea namna serikali ya CHADEMA itakavyokuwa tofauti kwenye kuendesha nchi, ambapo serikali yao italinda Uhuru, Haki na kuleta maendeleo.

Wakati huohuo ndugu Lissu akawaeleza wananchi wa Mtwara kuwa katika mikoa ya Kusini ya maeneo ya Mkuranga, Kilwa na Kibiti kulitokea mauaji ya kutisha, watu kupotea na wngine kuchukuliwa kutoka kwenye misikiti na kwenda kuteswa. akasema, aliyekuwa Mbunge wa Kilwa mheshimiwa Bwege alimueleza Lissu kuhusu unyama na ukatili wa kutisha waiofanyiwa watu wa maeneo hayo katika kipindi cha utawala huu wa awamu ya tano!. Lissu akasema, watu waliokotwa wamekufa katika mito na fukweni mwa bahari. Lissu akasema mambo hayo yanahitaji majibu na akasema kuwa serikali ya Chadema itatawala kwa haki

Kwa taarifa zaidi mtazame hapa Chini akiwa huko Mtwara






==

Subpost 6 - Mtwara hiyo leo ilitapika....!  KUMBUKA INAISHA LEO.  Usikose Ofa hi ( 640 X 640 ).jpg
Subpost 2 - Mtwara hiyo leo ilitapika....!  KUMBUKA INAISHA LEO.  Usikose Ofa hi ( 640 X 640 ).jpg
Subpost 3 - Mtwara hiyo leo ilitapika....!  KUMBUKA INAISHA LEO.  Usikose Ofa hi ( 640 X 640 ).jpg
Subpost 1 - Mtwara hiyo leo ilitapika....!  KUMBUKA INAISHA LEO.  Usikose Ofa hi ( 640 X 640 ).jpg
Mgombea Urais wa Chadema Mhe. @tunduantiphaslissu akizungumza na Wananchi wa Jim ( 480 X 640 ).jpg
 
Back
Top Bottom