Baada ya ujio wa Tundu Lissu, CHADEMA yatangaza kuvurumisha Mikutano ya hadhara Kanda ya Kusini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,733
218,320
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuanza ziara kabambe ya Kikazi kwenye Kanda ya Kusini.

Katibu wa Kanda hiyo Governor Kaduma amewaambia waandishi wa habari Mjini Masasi kwamba kwenye Mikutano hiyo ya hadhara , Kikosi kazi cha Chadema kitaongozwa na yule yule Mwamba wa siasa za Tanzania Freeman Mbowe.

Pamoja na kufanya mikutano ya hadhara Chama hicho kitakagua uhai wa chama , kufungua matawi mapya na kupokea Wanachama wapya.

Kivutio kikubwa kwenye mikutano hiyo ni Uwepo wa Tundu Lissu , ambaye atapewa nafasi ya kusalimia Wananchi (Subirini Spana za CAG).

Ratiba Kamili ya Mikutano hiyo ambayo ni Nonstop hii hapa.

12/4 Kilwa kaskazini na Kilwa kusini
13/4 Mchinga na Lindi Mjini
14/4 Mtama na Nachingwea
15/4 Liwale
16/4 Mtwara vijijini na Mtwara mjini
17/4 Newala Vijijini na Newala Mjini
18/4 Masasi
19/4 Tunduru kusini na Tunduru Kaskazini
20/4 Namtumbo na Songea Mjini

Mungu Ibariki Chadema

FB_IMG_1672921103951.jpg


UPDATES
========
View attachment 2585930
 
(Subirini spana za CAG)

Mambo yale yale

Serekali ile ile

Watu wale wale

Huwa nakuheshimu

Lakini
 
Kwa hivi sasa ukiwa ni Mpumbavu na Mwendawazimu ndiyo utapoteza muda wako kujihusisha na Siasa na Kuviamini vinavyojiita Vyama vya Upinzani nchini vilivyojaa Unafiki mtupu huku vyote vikiwa vimeshawekwa Mfukoni mwa CCM na Serikali yake.
Achana na Chadema wewe endelea na ccm yako ili uteuliwe kama wachumia tumbo wenzako
 
Kwa hivi sasa ukiwa ni Mpumbavu na Mwendawazimu ndiyo utapoteza muda wako kujihusisha na Siasa na Kuviamini vinavyojiita Vyama vya Upinzani nchini vilivyojaa Unafiki mtupu huku vyote vikiwa vimeshawekwa Mfukoni mwa CCM na Serikali yake.
Wasira amesema CCM ndo kiwanda cha unafiki duniani, unamwamini au unampuuza?
 
Lema kaishia wapi hivi? Au Geodarvie ameshamshusha kwenye ulimwengu wa siasa.?

Ogopa sana kupambana na mtu asiyekujibu kwa sauti ya kibinadamu.
 
Back
Top Bottom