Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Status
Not open for further replies.
Mijadala yenye mlengo wa kidini inachosha , mbona hizo CD zinauzwa hadharani ? Pia gazeti la Tanzania Daima ni vema lifanye kazi ya ku compromise CDM na Waislamu sio kuwafanya mahasimu kama kweli lina mlengo wa kimageuzi, Habari zake nyingi zinazohusu ndugu zetu waislamu zimekuwa ni hasi , hii haitasaidia ukombozi na itafanya ngumu kwa CDM kuendesha Nchi baada ya octoba 2015.

Unamaanisha unataka liandike habari za kuwaadaa waislamu? Tukizungumzia mambo ya Imani, Mategemeo yangu ni kwamba waislamu mpaka kufikia sasa watakuwa wamekwishabaini kwamba wanasiasa wote wanaowafuata kwa sababu ya uislamu wao hata kama ni waislamu wenzao hasa waislamu wenzao ni waongo.

Na kwa sababu wanadanganywa, hoja mbadala ni kuwaeleza ukweli.

LIPUMBA HAFAI KAMA ASIVYOFAA LOWASA.
 
Huyu Lipumba kuna mtu kamtia uchizi, vitu anavyozungumza utafikiri mtoto wa darasa la pili. Yawezekana Lipumba mwenyewe ni project ya CCM kwenye mambo ya udini amabayo CCM wanajua udini unaweza kuwatoa kwenye tundu la sindano 2015.
Angelikuwa Mbowe au Slaa sasa hivi wangetakiwa kuripoti polisi.
 
Sijaona kibaya alichonukuliwa akikisema Prof Ibrahim Lipumba.
Sawa kabisa hapa Arusha Lema Aaliwaambia waumini wa kikristo wasiende kanisani siku ya Jumapili kipindi cha uchaguzi wamadiwani huo sio udini lakini Lipumba mdini :nono::nono::nono:
 
Sijaona kibaya alichonukuliwa akikisema Prof Ibrahim Lipumba.
Hakuna kibaya alichokisema, ila kitendo cha kuwaabisha waumini msikitini ili wamchague 2015 , ndio kibaya zaidi.
why Lipumba?
 
CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!

Tukumbushe, lini maaskofu walifanya hivyo? Halafu sijaelewa issue ya Mbowe kumiliki kumbi za disco, mbona Alhaji Juma Athuman Kapuya anamiliki Band, Sheikh Aden Rage naye anamiliki Radio ambayo pia hua inapiga nyimbo zinazopigwa Disco? wote hao ni viongozi na sijawahi kusikia hata siku 1 Waislam wanawalalamikia, kuna kiongozi ana historia ya kufunga familia nzima kwasababu nyumba ndogo yake ilikua ikiliwa na mtoto wa mwanamziki, sasa hvi mtu huyo ni kiongozi mkubwa, na wala hili sio siri, Waislam wanajua, wanawake wengi wa Dar wanajua, hata Masheikh pia wanajua na still ni kiongozi na msikiti hua anaenda.
 
Nimekuuliza hayo ni maneno ya Prof Lipumba? naona bado unarusha. Unanchekesha.

Hivi Lipumba ni lini alitangaza kuwa atagombea 2015?
Sasa CUF mna mgombea gani mwingine zaidi ya Lipumba?
 
Hawa Chadema wanafikiri Waislamu hawawajui wanachokifanya na huyo Padri wenu Slaa.Hao waislamu mnaoambatana nao siku wakijitambua mtaona mtakavyo kaa uchi
 
Unajifanya ushasahau waraka wa uchaguzi 2010? Hadi wakafikia kiwango cha kuanza kupingana na mafundisho yao kudai tusimwangalie mtu kwa matendo yake bali tuangalie nini anasema. Wakati kwenye biblia inapingana na hayo matendo na maneno ndio symbol of someone who is accountable and good leader. Tupisheni bwana mshasahau humu JF mlikuwa mkisema hamtakaa mumchague tena rais mwenye kuvaa kibarakashia???? Kama udini ulianzia toka zamani ndugu zetu wakristo nyie ni wadini ila mkiona mwengine anafanya kinawauma swali ni nani alianzisha? Jibu mnalo.

wakristo sio wadini wala waislam sio wadini... ndo maana wanasoma wote na wanatibiana na wanafanya biashara pamoja.... MIMI na WEWE ndo wadini... kila saa tunakaa kuchunguza viongozi wa dini flan wamefanya nini na wanamaanisha nini?
kwa hiyo basi kuanzia leo MIMI na WEWE tubadilike, tusije tukamkosoa Mungu aliyeamua kutuacha tuishi kwa pamoja kwani Yeye ni mweza wa Vyote anngetaka kututenganisha angetutenganisha ila ameacha tuishi pamoja ili Mapenzi yake yatimizwe.... Mimi nimelitambua hili na kuanzia leo naacha udini Je wewe Mwenzangu???
 
Kanisa likipanga mipango wanokabidhiwa kuitekeleza ni CHADEMA mfano mzuri ni yale maazimio ya kurasini yaliyofanywa na viongozi 117.waliopewa wayapeleke Bungeni ni wabunge wachadema mfano baada ya kanisa kutoa tamko lenye maagizo lukuki kwa serkali wabunge waliopewa ni Joseph Selasini aelezee kwa nini VC wa udom nimwislaam,Lema aeleze udini wa kikwete ,Msigwa na Lissu
lkn mbele ya macho ya watu wa yessu hao si wadini bali ni mashujaa wa dini yao sasa mbona Tanzania daima washupalie Lipumba alieamua kusema kweli na kushindwa kuwasema wabunge wa chadema kupeleka usini bungeni?
 
ngoma anayocheza ni ileile inayochezwa na chadema kila siku. sema kiwanja kinachochezewa ngoma ndio kimebadilika.
hawa wooote kama walivyo chadema, hawana JEMA
 
Msimamo wa Tanzania Daima dhidi ya Waislam unajulikana sana hata kwa Muislam Muasi ndio maana haukuweka kambi pale Sumbawanga kanisa lilipotangaza kuwatenga Wakristo wote walompa Kura Mh.kessy, Rev Mtikila alipotengeneza na kusambaza Waraka wa kuwataka Wakristo wote wasimpe kura Jakaya 2010, halikupiga kambi kuripoti Mgombea aliekusanya Viongoz wa Dini Singida ili waingie kwenye Kampeni, siku nyingine likapige kambi makanisani lije litoe Habari kuwa wakristo kupitia Jukwaa lao walitangaza kuinyima Serikal ya Jakaya Ushirikiano na ifikapo tarehe 1july,2013 wakristo wote wawe wamejitoa CCM. Tangu mmeanza Vita zenu dhidi ya Uislam na Waislam kama kuna kitu kimepatikana basi ni kuwatia Ujasiri Waislam, Jifunzen kuendesha Siasa zenu bila ya kukabiliana na Uislam, maana hii dini mmeikuta na mtaiacha
Bora ukose mali kuliko kukosa akili. Like Songoro like Sylvester Mabumba.
 
Sijaona kibaya alichonukuliwa akikisema Prof Ibrahim Lipumba.
hivi kuhimiza haya nayo ni udini

“Kwahiyo, huu ni wakati wa kuwa macho kwamba tupo njiapanda. Hii neema, utajiri unaogunduliwa ikiwa hatutajipanga vizuri, neema hii itabadilika kuwa balaa, neema hii badala ya kumsaidia kila Mtanzania aweze kuneemeka na neema hii, itageuka kuwa balaa dhidi yetu,” alibainisha Profesa Lipumba.

Aliwaeleza waumini hao kuwa kwa sasa Waislamu wanapaswa kushiriki kikamilifu katika harakati za siasa za nchi kama walivyoshiriki wazee wao wakati wa kudai uhuru.

“Kwamba kila mwananchi, kila Mtanzania awe raia wa daraja la kwanza. Apate fursa ya uhuru wa dini yake, apate fursa ya kuelimishwa kwa kadiri ya uwezo ambao Mwenyezi Mungu amempa bila kubaguliwa, apate fursa ya kupata huduma bora za afya, apate fursa ya kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa serikali, apate fursa ya uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu.

“Kazi ipo kwetu, na ndugu zangu sisi tunapozungumza hapa tumejitoa mhanga. Kwamba hii ni nchi yetu sote, tunamuogopa Mwenyezi Mungu Tunamuogopa Mwenyezi Mungu na huu mwezi wa Ramadhan,” aliweka mkazo Profesa Lipumba
 
Huyu Lipumba kuna mtu kamtia uchizi, vitu anavyozungumza utafikiri mtoto wa darasa la pili. Yawezekana Lipumba mwenyewe ni project ya CCM kwenye mambo ya udini amabayo CCM wanajua udini unaweza kuwatoa kwenye tundu la sindano 2015.
Hata slaa ni project ya CCM pia, we unadhani ni kwanini ataki kurudisha kadi yao?
 
hii sasa imekuwa too much tukiendelea kuwaendekeza hawa watatula sana hasa nchi yetu iliyobakia ni kuomba kwa sana Mungu awatokee kwani serikali imeshindwa kufanya kitu inawabeba sana hawa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom