Makonda ambananisha meneja TANROADS Geita: Ahoji ni lini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Kakoro (km 60) utasainiwa ili ujenzi kuanza

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amembananisha Meneja wa TANROADS Geita kukihakikishia Chama Cha Mapinduzi kuwa ni lini barabara ya Kahama - Kakoro yenye urefu wa Kilomita 60 itajengwa kwa kiwango cha lami.

Mwenezi Makonda ambananisha Meneja huyo mara baada ya kutoridhishwa na majibu yake na kumtaka kuwasiliana na Viongozi wenzie kisha kutoa majibu papo hapo kwa Wananchi wa Geita ili kujua lini wataondokana na hadha hiyo.

" Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amerahisisha mifumo ya Mawasiliano hivyo wasiliana na Viongozi wenzio mjue ni lini na uje kutoa jibu ili Wananchi hawa wajue na sio kuwadanganya " Alisema Mwenezi Makonda.

Mara baada ya kufanya Mawasilano, hatimaye Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa alipiga simu na kukihakikishia Chama Cha Mapinduzi kuwa hadi kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu hatua za manunuzi zitakuwa zimekamilika na mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu Mkandarasi (CCIC) ataianza kazi rasmi ya ujenzi wa barabara hiyo.

Mwenezi Makonda amewataka Wananchi kuwa wavumilivu na kusubiria kuona utekelezaji wa ahadi hiyo iliyotolewa huku akiahidi kuweka msukumo mkubwa kufanikisha utekelezaji huo kwa haraka.

Ameyasema hayo leo tarehe 11 Novemba, 2023 wakati alipozungumza na Wananchi wa Wilaya ya Geita akiwa ziarani kikazi katika Mkoa wa Geita

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendaNaMama

WhatsApp Image 2023-11-11 at 18.50.37 (1).jpeg


PIA, SOMA:

Kauli na matamko mengine ya Makonda
 
Back
Top Bottom