LINI JK ATATEUA WAKUU wa WILAYA?

LATTICE BOND

JF-Expert Member
May 30, 2011
219
48
Kikatiba Ukomo wa wakuu wa mikoa na wilaya ni miaka mitano. Baada ya hapo uteuzi unatakiwa kufanyika tena. Mpaka sasa miaka miwili imepita Rais hajateua wakuu wa wilaya. Tatizo nini?
Hapo si kuvunja Katiba ya nchi?
 
watu aliwaahidi wengi mpaka hajui ampe nani amwache nani? kingine ukata
 
Ndo mwisho wao,
Taratibu post hizo zitajiuta kwa mbinu kama hiyo atumiayo sasa!
 
Hapo matotos yanajiandaa kuchukua nyadhifa, ila huwa naangalia kuwa kunaweza kuwa na utendaji bora mutu kama Fatuma Kimario
 
Hata hivyo hawana kazi, hasa hasa ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima. Toka niwafahamu hawa watu sijaona kazi ya maana wanayofanya kwa ajili ya wananchi, labda kuisaidia CCM basi. Na kama ndiyo kazi yao basi walipwe na chama na siyo serikali kama ilivyo sasa.
 
Akiwateuna atawalipa hela gani za uhamisho au kuripoti vituo vipya? Zilizopo sasa ivi ni za uchaguzi tuuu.
 
Afadhali hata asiwachague katika hii miaka mitatu iliyosalia. So far nchi inakwenda bila kuwa na wakuu hao wa wilaya.
 
Vipi mkuu umechoka kusubiri ahadi isiyotimilika nini!! Subiri tu atateua hivi karibu na nadhani hajakusahau.

Hata bila kuwa na wakuu wa wilaya mbona poa tu mambo yanakwenda, tuna ma DED, MED, na Ma RAC.
 
Kati ya nafasi ambazo katiba mpya inatakiwa kuziondoa ni UKUU WA WILAYA kwan hawana kazi yoyote zaidi ya kugombana na Wakurugenzi wa Wilaya ambao ndio watendaji na watekelezaji wa shughuli zote za serikal..
 
Ah...Kama ni ukata katika serikali,na tukae tu bila ma DC.. Labda ndiyo itasaidia kuchagua vipaumbele...

Au anangoja kikao cha CCM,cha baadaye mwaka huu,watakaokuwa kwenye mkondo wake,awatambue na wasio upande wake awajue,kisha nafasi za maDC aje kuwapa majeruhi wake katika mkutano huo..
 
Hawahitajiki tena, DAS yupo kama afisa tawala, DED yupo kama mtendaji wa wilaya pamoja na wakuu wa idara zote elimu, afya kilimo nk, wakuu wa mikoa wanatosha sana, hii ni mizigo ambayo serikali inaitua taratibu. Viongozi wamekuwa wengi sana na serikali inaelemewa na mzigo wa kuwahudumia. Hawa waliopo wanamalizia halafu watastaafu soon, huu ni mzigo sana
 
Kikatiba Ukomo wa wakuu wa mikoa na wilaya ni miaka mitano. Baada ya hapo uteuzi unatakiwa kufanyika tena. Mpaka sasa miaka miwili imepita Rais hajateua wakuu wa wilaya. Tatizo nini?
Hapo si kuvunja Katiba ya nchi?

Hatuwahitaji mkuu,hawana faida yoyote,bora asiwateue kabisa
 
then tunaposubiri katiba mpya ma-DED wakaimu ukuu wa wilaya ili kupunguza gharama za uendeshaji!!! jamani mnaonaje?
 
Back
Top Bottom