Waterlemon
Senior Member
- Sep 2, 2016
- 137
- 178
Hili tukio lilitokea kipindi cha nyuma... nimeona nilieke hapa jukwaani myaone wenyewe wana JM.
Tulikuwa tupo ndani ya basi kwenye mizunguko ya kawaida... kila mtu na shughuli zake na mawazo yake kichwani. Mara tukaskia mzozo kwa sauti za juu na za jazba.
Lijimama la kinaijeria ambalo lilikuwa limwili limemjaa haswa alikuwa akumtuhumu abiria wa pembeni yake ambae alikuwa kijana mdogo tu kwa kufoka kama kamchomolea pochi yake ya pesa kutoka kwenye mkoba wake.... kijana wa pembeni alionyesha kupinga hiyo tuhuma... lakini lawama ziliendelea kumwelemea na kipigo kuanza kumuangukia. Mwanzo kuanzia kutoka lijimama la kinaijeria kwa vibao na makofi, na abiria wengine wakaanza kumsaidia...
Kijana akakung'utwa vya kutosha.... kuanzia ndani ya basi ambali lilikuwa limejaa ... mpaka basi likasimama na kipigo kuendelea nje.
Katika pirika pirika za kuendelea kumpiga kijana wa watu... lijimama la kinaijeria katika kuruka ruka kusambaza kipigo, kati kati ya matiti pochi lake likachomoka na kuanguka hadharani... watu wote wanashuhudia ...
"Ooooh, kumbe pochi yangu ilikuwa hapa?" ... akaiokota na huyooo taratiiiibu, akaanza kuondoka.
Wapigaji waliokuwa wakisaidia wote macho yamewatoka wakimwangalia kijana aliepigwa wasijue la kufanya.
Je muungwana... anapopigwa mwizi . Ni sahihi kuingilia kutoa adhabu?