Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Mbwana Makata
Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imeipa Namungo FC pointi 3 na mabao matatu na kusema kuwa imejiridhisha Mbeya Kwanza waligomea mchezo huo licha ya taratibu kuwa sawa dakika ya 23 ikiwa ni dakika saba kabla ya kutimu nusu saa.
Aidha, Kocha wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma na mchezaji wa timu hiyo, Jamali Mtegeta wamefungiwa michezo mitatu na faini ya Tsh 500,000 kila mmoja kwa kosa la kushambuliana kwa mateke wakati wa mechi ya timu yao dhidi ya Biashara United, Mei 5, 2022.