Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC! | Page 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Mar 30, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

  Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

  Sifa za Wagombea Watano watakao pitishwa na CC kuingia tano bora ya NEC ni hawa...
  1. Mgombea mmoja mwanamke
  2. Mgombea mmoja Muislamu
  3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar
  4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!
  5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

  NEC itawapigia kura, ambapo mgombea tajwa, ataongoza kwa kura nyingi atasindikizwa na mgombea mmoja mmoja Mwanamke kutoka Zanzibar na Yule Waziri Mkuu Kingio, ambapo kwenye Mkutano Mkuu, wale wagombea wasindikizaji wawili watajitoa hivyo mgombea huyo kupaswa bila kupingwa kisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu watapiga kura zuga tuu na matokeo, atakuwa amechaguliwa kwa asilimia 99%, na hiyo asilimia 1% itakayo mkataa ni kuzungia tuu kuwa CCM demokrasia!.

  Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, kwa kumchinjia rasmi baharini kwa kumpa maksi za chini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

  Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
  ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

  Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

  Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

  NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakabali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo wa uongozi, wa kulibadili taifa hili kuwa nchi ya neema, na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingi huko nyuma na ikabaki salama, hivyo kama ni kweli hiki ndicho walichopanga kukifanya this time!, hakitabaki salama!. Yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

  Paskali
   
 2. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #281
  Jun 20, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,934
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mbona mrema alikatwa, na hakununua watu na bado nchi ilibaki salama; sio lazma uwe rais TZ
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #282
  Jun 20, 2015
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,493
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  kumbe jibu unalo
  Lowassa akiachiwa tu na CCM basi UKAWA watachukua Urais

  ili kuondoa Makundi kashfa na Ufisadi ni kulikata tu jina lake
  (waturudishie tu Chama Chetu CCM si chama cha mafisadi, watu waliingia wakiwa maskini leo wanataka kukiendesha km chao - By Makongoro JK)
   
 4. BABU KIDUDE

  BABU KIDUDE JF-Expert Member

  #283
  Jun 20, 2015
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,439
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Hata CCM Leo wanamwita LOWASA fisadi duh kweli ujafa ujaumbika
   
 5. Zatara

  Zatara JF-Expert Member

  #284
  Jun 20, 2015
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 558
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Naheshimu mawazo yako SHEMGUNGA, Ila napata shida kuelewa unaposimamia mtu baada ya mfumo.

  Huyu bwana anaweza kukatwa na maisha yataendelea. Unawajua wa Tanzania ndugu!!!! Sekunde kumi (10 Sec) wameshasahau kila kitu, wanaangalia maslahi ya muda mfupi kwa mwengine.

  Halafu huyu jamaa, watangazo ya biashara ndio yanambeba kuliko history ya utendaji wake. Lakini nafikiri mwaka huu "atayetoa noti za bandia atapewa tu cheni ya bandia". Ningefurahi iwapo zingekuwa zinajengwa hoja kwanini yeye, kuliko lazima awe yeye (Ni mtazamo wangu tu).
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. g

  ganda JF-Expert Member

  #285
  Jun 20, 2015
  Joined: Nov 10, 2014
  Messages: 468
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uchaguzi wa mwaka huu, fisadi kuingia ikulu itakuwa ni sawasawa na ngamia kuingia kwenye tundu la sindano. Na ni kheri wale wote waliohusishwa na ufisadi wa aina yeyote ile, wangeendelea kula hela zao waachane na kimeo ccm
   
 7. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #286
  Jun 20, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,468
  Likes Received: 1,315
  Trophy Points: 280

  CCM wangekuwa wajanja wangepiga sana pesa.
  Watoe tenda ya kuchezesha Kamari ya nani atakuwa Mgombea ya CCM 2015 Uraisi. Maana hii idadi inaruhusu kabisa na ukiangalia karibia zaidi ya Waombaji 15 uwezo uko sawa.

  Kama kweli watafanikiwa kumchinjia baharini Lowassa mchezo unaweza kuwa kama hapa chini.
  Ebu twende taratibu wagombea mpaka sasa 35.  1.Mgombea mmoja mwanamke-Dr A. Migiro
  2. Mgombea mmoja Muislamu-Balozi Amina Salumu Ali.
  3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar-Dr. Bilal
  4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!-Mhe.Pinda
  5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.?????????????

  1.Prof Mark Mwandosya 2.Charles Makongoro Nyerere 3. Judge Augustine Ramadhani.

   
 8. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #287
  Jun 20, 2015
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,493
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
 9. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #288
  Jun 21, 2015
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,816
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  ????????
   
 10. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #289
  Jun 21, 2015
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,578
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  Nakuhakikishia wakikata jina lake hakutakuwa na chochote kitu wanamuogopa bila sababu kwanza hatawafanya kitu kwa sababu stress na stroke atakayopata kwa kukatwa jina vitamuweka busy sana.
   
 11. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #290
  Jun 22, 2015
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 692
  Trophy Points: 280

  • Pasco vipi mkuu................? Nakushangaa...............!!   
 12. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #291
  Jun 22, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,703
  Likes Received: 5,587
  Trophy Points: 280
  Chaguo la Mungu hakuna anaye weza kupinga...!!!
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #292
  Jul 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280
  soma hii thread nilisema nini na kimetokea nini!
   
 14. loykeys

  loykeys JF-Expert Member

  #293
  Jul 11, 2015
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 1,157
  Likes Received: 747
  Trophy Points: 280
  chaguo la Mungu yupi labda embu tufafanulie?
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #294
  Jul 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280
  ........................................................
   
 16. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #295
  Jul 14, 2015
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,769
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  At last!!
   
 17. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #296
  Jul 14, 2015
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,067
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Thamani yako imeporomoka kama ya Lowassa. Ndo tatizo la kuwa bendera kufuata upepo. Vijana mnaoonekana kuwa na uelewa mkubwa mnajidhalilisha kwa kutumika kama toilet paper. Sasa mnavuna mlichopanda...
   
 18. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #297
  Jul 14, 2015
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,612
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  mkuu angalia uzi ni wa tarehe ngapi. Pasco umewashinda gwajima na tb joshua
   
 19. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #298
  Jul 14, 2015
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,612
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  heshima sana pasco kwa uzi huu una asilimia 70 za utabiri ni correct. Umewashnda ccm kwa hilo but what is your plan b?.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #299
  Jul 14, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280
  Baada tuu ya jina la Lowassa kukatwa kwenye 5 bora, nilipandisha uzi huu, Kukatwa Kwa Lowassa, Jee Ndio Mwisho wa Ile Safari, Au..., nikishauri ahame CCM safari iendelee, huku nikitaraji atakayepita ni Membe!.

  Lakini baada ya kupitishwa Magufuli, nilifanya about turn na kumshauri sasa atulie tuu, kwa sababu Magufuli ni jembe zaidi ya Lowassa!. Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali yaishe, vunja kambi na kujisalimisha!.

  Pasco
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #300
  Jul 27, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280

  ..............................................
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...