Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC! | Page 16 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Mar 30, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,668
  Likes Received: 23,949
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

  Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

  Sifa za Wagombea Watano watakao pitishwa na CC kuingia tano bora ya NEC ni hawa...
  1. Mgombea mmoja mwanamke
  2. Mgombea mmoja Muislamu
  3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar
  4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!
  5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

  NEC itawapigia kura, ambapo mgombea tajwa, ataongoza kwa kura nyingi atasindikizwa na mgombea mmoja mmoja Mwanamke kutoka Zanzibar na Yule Waziri Mkuu Kingio, ambapo kwenye Mkutano Mkuu, wale wagombea wasindikizaji wawili watajitoa hivyo mgombea huyo kupaswa bila kupingwa kisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu watapiga kura zuga tuu na matokeo, atakuwa amechaguliwa kwa asilimia 99%, na hiyo asilimia 1% itakayo mkataa ni kuzungia tuu kuwa CCM demokrasia!.

  Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, kwa kumchinjia rasmi baharini kwa kumpa maksi za chini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

  Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
  ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

  Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

  Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

  NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakabali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo wa uongozi, wa kulibadili taifa hili kuwa nchi ya neema, na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingi huko nyuma na ikabaki salama, hivyo kama ni kweli hiki ndicho walichopanga kukifanya this time!, hakitabaki salama!. Yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

  Paskali
   
 2. Wgr30

  Wgr30 JF-Expert Member

  #301
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 1,431
  Likes Received: 1,649
  Trophy Points: 280
  dah watu wana maneno!!
   
 3. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #302
  Nov 10, 2017
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 4,698
  Likes Received: 5,935
  Trophy Points: 280
  Ndiyo
   
 4. radika

  radika JF-Expert Member

  #303
  Nov 10, 2017
  Joined: Jul 15, 2014
  Messages: 13,176
  Likes Received: 17,634
  Trophy Points: 280
  hapa hata sijakuelewa mkuu unaweza kufafanua sijaona kosa la pascal ktk huu uzi?
   
 5. Tajirimsomi

  Tajirimsomi JF-Expert Member

  #304
  Nov 10, 2017
  Joined: Jan 12, 2017
  Messages: 4,646
  Likes Received: 4,725
  Trophy Points: 280
  Makaburi
   
 6. kipara kipya

  kipara kipya JF-Expert Member

  #305
  Nov 26, 2017
  Joined: May 2, 2016
  Messages: 4,195
  Likes Received: 3,807
  Trophy Points: 280
  kutoka maktaba ,tujikumbushe!
   
 7. ARCHBISHOP

  ARCHBISHOP JF-Expert Member

  #306
  Nov 27, 2017
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 80
  Hii comment bado ipo valid?
   
 8. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #307
  Nov 27, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,744
  Likes Received: 10,971
  Trophy Points: 280
  Of course!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...