Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
26,660
Likes
27,483
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
26,660 27,483 280
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

Sifa za Wagombea Watano watakao pitishwa na CC kuingia tano bora ya NEC ni hawa...
1. Mgombea mmoja mwanamke
2. Mgombea mmoja Muislamu
3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar
4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!
5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

NEC itawapigia kura, ambapo mgombea tajwa, ataongoza kwa kura nyingi atasindikizwa na mgombea mmoja mmoja Mwanamke kutoka Zanzibar na Yule Waziri Mkuu Kingio, ambapo kwenye Mkutano Mkuu, wale wagombea wasindikizaji wawili watajitoa hivyo mgombea huyo kupaswa bila kupingwa kisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu watapiga kura zuga tuu na matokeo, atakuwa amechaguliwa kwa asilimia 99%, na hiyo asilimia 1% itakayo mkataa ni kuzungia tuu kuwa CCM demokrasia!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, kwa kumchinjia rasmi baharini kwa kumpa maksi za chini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakabali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo wa uongozi, wa kulibadili taifa hili kuwa nchi ya neema, na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingi huko nyuma na ikabaki salama, hivyo kama ni kweli hiki ndicho walichopanga kukifanya this time!, hakitabaki salama!. Yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Paskali
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,805
Likes
9,880
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,805 9,880 280
Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza
 
Eistein

Eistein

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Messages
1,107
Likes
8
Points
135
Age
34
Eistein

Eistein

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2011
1,107 8 135
Kwa kuwa umejitetea hii ni info tu, no maswali basi ngoja nikuache tu.... But lowasa hawezi kuwa rais wa nchi hii.. Liko wazi, kuleni tu pesa zake... Naamini duniani kote watz tunaongoza kwa kuwa na kumbukumbu za muda mfupi sana. Njaa mbaya sana.
 
Freeland

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
14,459
Likes
6,754
Points
280
Freeland

Freeland

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
14,459 6,754 280
Hhahaahahhah...Huyu ndiye Pasco bana.....Thanks JF Thanks Maxence Melo watu kama hawa tungesoma wapi vijimambo vyao hivi
 
Last edited by a moderator:
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified User
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,143
Likes
12,659
Points
280
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified User
Joined Dec 27, 2012
8,143 12,659 280
Hivi kaka Pasco unaamini hadi leo kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania? Kwa lipi hasa? Mtakuwa na madodoki na magunzi mangapi kumsafisha? Kuongozwa naye ni pigo kwa nchi na vita dhidi ya ufisadi
 
Last edited by a moderator:
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2009
Messages
4,373
Likes
136
Points
160
Nyunyu

Nyunyu

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2009
4,373 136 160
Hivi kaka Pasco unaamini hadi leo kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania? Kwa lipi hasa? Mtakuwa na madodoki na magunzi mangapi kumsafisha? Kuongozwa naye ni pigo kwa nchi na vita dhidi ya ufisadi
Mkuu ndo maana mwekundu kasema kwanza atueleze ya Richmond ilikuwa ya nani?
 
Last edited by a moderator:
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
6,340
Likes
10,372
Points
280
G Sam

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
6,340 10,372 280
Ngoja nikuhakikishie bwana Pasco, Nape Nnauye kwa mdomo wake alinitamkia kuwa "Endapo Lowassa atajitokeza kugombea, basi jina lake litakatwa katika hatua za mwanzo kabisa"

Ni ndoto za mchana kwa Lowassa kupitishwa na chama chake eti awanie urais! Ni ndoto za mchana!
 
Last edited by a moderator:
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
30,366
Likes
57,961
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
30,366 57,961 280
Hii thread naona kama vile imelenga kujihami zaidi kuliko kutoa taarifa!

Hata hivyo,binafsi niliwahi kupost uzi hapa mwaka jana nikionya kuwa Lowassa hawezi pitishwa kwani hakubaliki na safu ya juu niliyoitaata "top layer ya viongozi wa CCM" na nikasema kabisa hii issue inaweza kukisambaratisha kama sio kukigawa chama hiki.

Hivyo, mimi sishangai na mpaka leo bado naamini jina la Lowassa halitapita na hicho ndio kitakachokuja kutokea.

Time will tell
 
A

AIR MISSILE 2015

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
500
Likes
0
Points
33
Age
36
A

AIR MISSILE 2015

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
500 0 33
Pasco naye kaweka mtego Jf!!!! Hongera sana, ila ukweli ndio huo, wewe endelea kula pesa zake lakini mtu wako HAWEZI KUWA RAIS WA TANZANIA!! Ilo sahau.
 
Simba Mangu

Simba Mangu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
351
Likes
17
Points
35
Simba Mangu

Simba Mangu

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2010
351 17 35
Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza
MWEKUNDU wewe ni kiziwi? si alisha mwambia mwenyekiti nini hujui? au wewe sio mtu mzima?Mtu mzima ukiambiwa sio lazima ujibu unaweza guna au kukohoa ina maana ndiyo.Natumaini umepata jibu,kama sivyo uliza wajumbe wa kamati kuu ya chama chako/au nje nkapa
 
K

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Messages
1,595
Likes
747
Points
280
K

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2015
1,595 747 280
Lowassa ni mwizi hafai kuwa kiongozi. Lowassa ni fisadi hafai kuwa kiongozi, huko kupendwa na wengi siyo bali ananunua kupedwa
Heshima mbele mkuu.Lowasa ni kweli kabisa anapendwa na wengi lakini kwa mimi mwaka huu sijaona mgombea mahususi toka vyama vyote.Lakini kuna baadhi ya masuali huwa najiuliza,Ni mgombea gani ndani ya CCM hana kashfa ya ufisadi?.Je baada ya EL kuenguliwa kutokana na ufisadi hatujaona tena au kuthibitisha ufisadi mwingine baada ya yake?.Je kama viongozi wote ni wachafu ndani ya ccm itabidi wawapitishe kuangalia nani mchapakazi zaidi ingawa ana makandokando?.Je ccm itakapo acha kumpitisha kuwania uraisi ana ujasili wa kuhama chama?.Na nini kitakachotekea ndani ya ukawa baada ya EL kuacha kupitishwa ndani ya CCM?.Na je hatuoni kwamba baadhi ya wagombea wa UKAWA kila mtu atahisi kuishinda ccm imeyobaki dhaifu baada ya EL kuondoka?.Je hao mashekhe na Maaskofu wanao mpigania EL kuwa raisi wanahitaji nini kutoka kwake?.Mimi nafikili ccm wawe makini sana na uamuzi wowote ule watakao fanya.Na pia Ukawa wawe makini sana kama EL akihama chama mana kila mgombea wa ukawa anaweza hisi anazo nguvu za kuishinda ccm dhaifu baada ya EL kuondoka na kundi kubwa na hivyo ikawa ni mwazo wa UKAWA kusambaratika.
 

Forum statistics

Threads 1,213,835
Members 462,336
Posts 28,491,948