Elections 2015 Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Wacha urongo Kaka, Lowassa ni kipenzi cha mafisadi, si cha watu. Jiwe walilolikataa waashi? Lowassa? Don't let me puke! Jiwe la msingi halitumii mabilioni kutaka litumiwe. Kwa miaka mitatu minne iliyopita, Watanzania tumekuwa na jinamizi la mafisadi kununua Ikulu. Mungu anatupenda, kapishia mbali.una mtu wake kakamatwa na bulungutu pale St Gasper, hukumwona? Kipenzi cha watu hanunui uongozi kutumia Wahindi. William Marconi.
 
The Boss umemaliza kilakitu. Pasco, with all due respect, uchambuzi wako juu ya matukio muhimu ya kisiasa nchini hivi karibuni umekuwa kama utabiri wa hayati Shehe Yahya. Ulisema Zitto angeibuka mshindi katika kesi yake dhidi ya Chadema na kupinga kwake kufukuzwa na chama chake lakini bado Zitto alishindwa kesi na alifukuzwa na Chadema. Ulisema CCM hawana ubavu wa kumkata Lowassa. Wamemkata kiulaini sana tu. Na sidhani kama ana nguvu ya kufanya chochote dhidi ya CCM. Watu tuna kumbukumbu ndogo sana. Historia inaonyesha mifumo mibovu ya uongozi Tanzania ni mifumo ambayo haiwezi kung'olewa na mtu mmoja mmoja kwa style ya Zitto na Lowassa. Strong teams, kama wanavyojaribu kufanya UKAWA sasahivi ndo strategy inayoweza kusaidia kubomoa mifumo dhalimu Tz. Siyo individuals. Tanzania siyo kama Rwanda au Burundi huko ambako mtu mmoja anaweza kusumbua jamii karne hadi karne. Shetani wetu ni wa tofauti sana.
 
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....

Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.

Ni upuzi kudhani kuwa UKAWA Watamchukua Lowassa! Aende kwenye chama chake ACT ZZK anamsubiri ili utabiri wake wa wabunge 40 kuhamia ACT utimie. Amchukue Hamadi na Shibuda pia Leticia Nyerere na Mzee wa Sumbawanga Arfi pamoja na hao wabunge wa Lowassa.
 
Wakati mwingine ni bora kukaa kimya..Lowassa alikuwa chaguo la wachumia tumbo, watumwa wa mali walopanda mbegu za magugu katika shamba la ngano na kuishi kwa matumaini - HOPE ya kwamba ONE day YES mbegu hizo zitaota baina yake na Ngano bila kugunduliwa. Wakasahau ya kwamba magugu kusubiriwa kwanza yakaota pamoja na ngano, kwa sababu huwezi ng'oa miche ya magugu pekee unaweza kung'oa hata miche ya ngano safi. Hivyo husubiria yakaota kisha kupaririwa na kuchomwa moto, watu wakavuna ngano safi na kuiweka Ghalani..

Katika mambo yote alowahi kufanya JK atakumbukwa zaidi kwa hili, na Heko CC ya CCM kwa kufanya maamuzi sahihi. Kusema kweli sitojali tena nani baina yao atakuwa rais wa JMT maadam sio Lowassa..

Vipi mkuu Akiingia ACT ya "kipenzi chako" Zitto utamsapport?
 
Vipi mkuu Akiingia ACT ya "kipenzi chako" Zitto utamsapport?
Nai akiingia ACT! Lowassa? huyu mwizi hawezi kujiunga ACT kwa sababu hana sifa za uongozi, pengine UKAWA maana ndio mtu pekee anayeweza kuwashinda CCM kwa sababu ya watumwa wengi wa akioli wapo huko. UKAWA wanachotaka ni kugawana kwa hiyo hii ime fit vizuri kwao. Lowassa alipendwa na UKAWA wote na muda wote dhidi ya JK..
 
Kumbuka Zitto alisha mkaribisha, alisema Lowassa anakaribishwa iwapo akitangaza madeni na mali zake.
 
Kumbuka Zitto alisha mkaribisha, alisema Lowassa anakaribishwa iwapo akitangaza madeni na mali zake.
Mkuu Lowassa toka mwaka 2005 alijulikana na kutishia kuhamia CDM huu ni muendelezo tu. Kwa nini UKAWA hawakutangaza mgombea wao hadi CCM watangaze kwanza walikuwa wanasubiri nini? Anyway Lowassa akikaribishwa ACT naachana na siasa za Bongo napaka kila kona..
 
Wanabodi, CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

Lowassa sema....
Sema usiogope sema!.

Linasubiriwa Neno tuu!.

Pasco!

Kushiriki katika ukombozi kwa njia hiyo ni jambo ambalo anaweza kulifanya ili aweze kujitendea haki baada ya udhalilishaji mkubwa aliofanyiwa na wanamtandao na hasa Rafiki yake. "Hatuja kutana barabarani"

Hana cha kupoteza zaidi nikujijengea nafasi mpya mbele ya Safari kwani UKAWA watakuwa magogoni na kama ujuavyo Siasa ni Sanaa kwa hiyo kuwapo yeye kwenye vita ya Ukombozi lazima kuna zawadi /malipo anayostahili baada ya kazi kukamilika maana Majimbo kadhaa yaliyo ngome kuu za CCM watachukua yeye na Chama chake kipya.

Mfano kwa Membe,Samwel Sita,Makinda yako mengi na hili liutaleta uwiano wa yeye na Chama chake kuwa na Sauti na kwa vile watakuwa wapinzani lazima UKAWA itawapa fadhila-huu ni muda kwa UKAWA kuwa na MOUDs na chama atakacho hamiana si kwa minajili ya kuungana bali kwa mikakati ya Ushindi dhidi ya goli la Mkono.
 
Wanabodi,

Wapenzi, wafuasi, na mashabiki wa Lowassa, wanachosubiri sasa ni aseme neno moja tuu na roho zao zitapoa!, akiamua kukubali matokeo kuwa kukatwa kwake ndio mwisho wa safari, na akubali na aseme wazi, "Eloi Eloi, Yemekwisha!", na kama hajakubali, atamke wazi kuianza ile safari ya ukombozi wa pili wa Mtanzania, dhidi ya mkoloni mchwa CCM, aliyelitafuna taifa letu kwa miaka 50, na akitamka tuu!, "CCM Basi!", huo ndio utakuwa mwisho wa hili zimwi linaloitwa CCM!, CCM itakuwa ni bye bye jumla, kaburini forever!,

Lowassa sema....
Sema usiogope sema!.

Linasubiriwa Neno tuu!.

Pasco!

Nimepewa tip, neno litapatikana ndani ya saa 72 kutokea sasa!.

Pasco
 
Kushiriki katika ukombozi kwa njia hiyo ni jambo ambalo anaweza kulifanya ili aweze kujitendea haki baada ya udhalilishaji mkubwa aliofanyiwa na wanamtandao na hasa Rafiki yake. "Hatuja kutana barabarani"

Hana cha kupoteza zaidi nikujijengea nafasi mpya mbele ya Safari kwani UKAWA watakuwa magogoni na kama ujuavyo Siasa ni Sanaa kwa hiyo kuwapo yeye kwenye vita ya Ukombozi lazima kuna zawadi /malipo anayostahili baada ya kazi kukamilika maana Majimbo kadhaa yaliyo ngome kuu za CCM watachukua yeye na Chama chake kipya.

huu ni muda kwa UKAWA kuwa na MOUDs na chama atakacho hamiana si kwa minajili ya kuungana bali kwa mikakati ya Ushindi dhidi ya goli la Mkono.
Mkuu Mp Kalix2, nayatafakari maneno haya kwa kina!.
Pasco
 
Mkuu Lowassa toka mwaka 2005 alijulikana na kutishia kuhamia CDM huu ni muendelezo tu. Kwa nini UKAWA hawakutangaza mgombea wao hadi CCM watangaze kwanza walikuwa wanasubiri nini? Anyway Lowassa akikaribishwa ACT naachana na siasa za Bongo napaka kila kona..
Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.

Pasco
 
Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.

Pasco
Kifupi, Lowassa ni mtu mwenye KASHFA nzito nzito za uongozi ambazo anatakiwa kusimamishwa na hata kushtakiwa. Mbali na hilo ni mtu anayetaka uongozi by any means necessary! Kiongozi huchaguliwa na watu sio haki ya mtu. Hatakiwi mtu wa aina hii kupewa uongozi atakuwa na kisasi, ni wa kuogopwa kama Ukoma!..Mimi nilikuwa mwanachama wa CCM toka mwaka 1973, ni watu kama yeye waloniondoa imani na chama hicho...
 
Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.

Pasco

Ktk vitu ambavyo CCM watajuta ni mchezo walioufanya Dodoma!!

Sisi wakristo tunayaamini sana mafundisho ya Suleiman pale aliposema 'KURA' huamua mashindano.... huwanyamazisha hata wakuu...

Najiuliza hiyo system imekosa akili ya kutengeneza mazingira ambayo ingeonekana Lowassa ameshindwa kwa njia ya kura??

Kinyongo kitaimaliza CCM.... kinyongo ndio kimefanya Magufuli ashindwe ku make headlines mbele ya Lowassa!!!

Hata kama Magufuli atashinda itamgharimu muda mrefu sana kufanya reset ndani ya mioyo na masikio ya watu.....

Sanduku la kura pekee lingenyamazisha watu ila kwa uzandiki ule ngoja tusubiri....
 
Aliiba mini? Mbona hajapelekwa mahakamani? Alijihudhuru kwa hasira turn! maana hata kamati iliyoundwa na spika Sitta haikumhoji, Lowasa alilalamikia hilo mlemle bungeni.
 
Back
Top Bottom