Kukatwa kwa Lowassa, ni mwisho wa ile safari, au ni mwanzo wa Safari Halisi ya Matumaini?

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
25,773
Likes
24,367
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
25,773 24,367 280
Wanabodi,

CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.

Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, aliwahi kusema, upinzani wa kweli, utatoka CCM. Jee hiki ndio kipindi cha upinzani huu?

Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?

Jee Lowassa tuliombatiza jina la mwamba, ataliishi hilo jina la mwamba kwa kuonyesha umwamba wake kwa kutokubali kuchinjwa na kufanywa mbuzi wa shughuli, au lile jina la mwamba, tulimpachika tuu, ila in reality kumbe sii mwamba lolote wala chochote, bali ni kichuguu tuu?.

Mimi bado ni muumini wa andiko hili lisemalo "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!", jee Watanzania tuendelee kuwatumainia hawa waashi wa CCM kuamua hatma yetu na taifa letu, au tumchukue mtu wetu na kusindikiza ikulu nje ya CCM?

Nauliza tena, jee huu ndio mwisho wa safari, au mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini kwanza kwa kuingoa CCM na kuikomboa Tanzania?!.

Japo CCM ni chama kikubwa, kikongwe, na chenye nguvu, mbele ya Lowassa CCM ni chepesi kama unyoya, akipuliza tuu kinapeperuka, na hizo nguvu CCM inazojivunia, mbele ya Lowassa ni kama uzi wa utando wa buibui, ukigusa tuu umekatika!.

Wapenzi, wafuasi, na mashabiki wa Lowassa, wanachosubiri sasa ni aseme neno moja tuu na roho zao zitapoa!, akiamua kukubali matokeo kuwa kukatwa kwake ndio mwisho wa safari, na akubali na aseme wazi, "Eloi Eloi, Yemekwisha!", na kama hajakubali, atamke wazi kuianza ile safari ya ukombozi wa pili wa Mtanzania, dhidi ya mkoloni mchwa CCM, aliyelitafuna taifa letu kwa miaka 50, na akitamka tuu!, "CCM Basi!", huo ndio utakuwa mwisho wa hili zimwi linaloitwa CCM!, CCM itakuwa ni bye bye jumla, kaburini forever!, kwa sababu kazi kubwa ya kwanza ya serikali mpya, itakuwa ni kuzitaifisha mali zote za umma CCM iliyozipora na kuzipata kwa njia dhalimu kwa kuzipora toka kwa Watanzania katika kipindi cha utawala wake, na kujimilikisha kujifanya ni mali zake, yakiwemo majengo yake yote!. CCM ikiishakuwa haina kitu, hiyo sio CCM tena bali itageuka CCM mfu na tutaizika rasmi kaburini!.

Lowassa sema....
Sema usiogope sema!.

Linasubiriwa Neno tuu!.

Pasco!

 

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,851
Likes
22,940
Points
280

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,851 22,940 280
Pasco ungepumzika for now
sioni kama una make sense anymore
kila ulichotuambia huko nyuma kimeenda the opposite
labda sasa ungenyamaza kwanza.......ni kama vile nyinyi wapambe wa mgombea
mna kiu na urais kuliko mgombea mwenyewe
 
Last edited by a moderator:

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
2,794
Likes
18
Points
135
Age
48

Gor

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
2,794 18 135
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....

Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.
 

Deo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Messages
1,213
Likes
116
Points
160

Deo

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2008
1,213 116 160
Pole sana
Edo hajakatwa ni kwamba jina lake halijapelekwa kwenye kamati kama alivyoeleze Nchimbi
Japo sikupenda na nilihisi kuwa Edo asingepita lakini njia hii imeniumiza kwa vile kwa viwango hata ya ibilisi ni mbinu chafu sana.
Itoshe kusema hiyo ndio mbinu yenyewe ya sisiem mafisadi na hasa wenye iq ndongo kwa vile hawaba mbinu zaidi
paskali subiri uchaguzi na utangazaji wa raisi chini ya jk. itakuwa kiama
 

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
6,570
Likes
4,761
Points
280

Hute

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
6,570 4,761 280
lowasa akienda ukawa anashinda urais, achague vyama vile ambavyo havina hata shilingi mia mfukoni au vile vinavyotaka kufa, achukue fomu, anashinda uchaguzi bila shida. ila awe makini ahofie usalama wake kwa sasa kwasababu ni kitu kigumu sana kupigana na system hasa katika wakati kama huu ambao wamemwonyesha wazi kuwa wanapambana naye.
 

Ozzie

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Messages
3,235
Likes
46
Points
145

Ozzie

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2007
3,235 46 145
Kwa Katiba ya sasa 1977:

itakuwa sawa na mamba Nje ya maji... Ajaribu aone.
Kaka wengi hawajashitukia hilo. Lowassa asithubutu kujifanya atagombea chama kingine, maana hatopitishwa na tume zinazohusika. Labda akitaka kujitoa ufahamu ni kuhamishia majeshi yake UKAWA kama mwezeshaji tu. japo ambalo silioni kama lawezekana. Na asithubutu kwenda ACT, maana huko chama kichanga, wengi walimpenda akiwa ndani ya CCM. Pesa si kila kitu.
 

Mjasiria Akili

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Messages
826
Likes
191
Points
60

Mjasiria Akili

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2012
826 191 60
lowasa akienda ukawa anashinda urais, achague vyama vile ambavyo havina hata shilingi mia mfukoni au vile vinavyotaka kufa, achukue fomu, anashinda uchaguzi bila shida. ila awe makini ahofie usalama wake kwa sasa kwasababu ni kitu kigumu sana kupigana na system hasa katika wakati kama huu ambao wamemwonyesha wazi kuwa wanapambana naye.
Umeona ukawa ndio wa kukaribisha wezi? Labda aende kile chama cha zambarau au chama kingine nje ya ukawa
 

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
880
Likes
24
Points
35
Age
34

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
880 24 35
Wamejipanga kushinikiza jina la Lowasa kurudishwa ndani ya NEC . Ikishindikana kutumia mkutano mkuu kukataa maamuzi yote ya vikao vya awali yani Kamati ya maadiki CC na NEC
.
inadaiwa Kwa Mujibu wa Katiba ya CCM, Toleo la Mwaka 2012 Ibara ya (105), Inazungumzia Kazi za Mkutano Mkuu. Ibara Ndogo ya (03), ya Ibara ya (105), ya Katiba ya CCM toleo la Mwaka 2012 inaipa Mkutano Mkuu mamlaka ya Kuthibitisha, Kubadili, kukataa, au kuvunja uamuzi wowote uliotolewa na kikao chochote cha chini yake au na yeyote wa CCM.
Mkutano Mkuu ndio Ngazi ya Juu na ya Mwisho ya Kimaamuzi ndani ya CCM kwa mujibu wa Ibara ya (104), Ibara Ndogo ya (2), ya Katiba ya CCM.
habari kutoka moja ya mjumbe Dodoma ila siwezi sibitisha
 

Mr. Django

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Messages
1,358
Likes
1,328
Points
280

Mr. Django

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2014
1,358 1,328 280
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....

Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.
Wapinzani ntawadharau na pasina shaka hata watanzania wengi watawadharau kama wakimpokea Lowassa!

Wameimba nchi nzima kwa miaka chungu nzima kwamba EL ni fisadi eti leo wampokee na kumpa nafasi ya juu kabisa ya kugombea urais!!!
 

Forum statistics

Threads 1,189,307
Members 450,597
Posts 27,631,832