LHRC yaishtaki serikali ya Tanzania ICC

Nasubiria stesheni mbalimbali ze TV zitakavyowasilisha hilo jambo. Sitegemei mengi toka TBC.
 
After investigation the report will tall who is liable in that crime and the Prosecustion side shall prepare the "charge" agaist them and they will issue the sommuns to appear before the court of Law in order to answer the case against them. And the court will tell prosecution side to bring the witness and failure to that the court may acquit but if they will gate new avidence the case will start again.
 
Ni habari njema ila mama helen awe mwangalifu acjepelekwa mabwepande
 
Kumbe Tanzania yrtu hii nayo kuna vichua jamani; that is the way to go - mauaji ya raia sasa basi!!!!!!!!
 
nammis Luis Moreno Ocampo sijui huyu mama kama ataweza kuja wachukua kina Mwema, Nchimbi et al. then akawachuje Hague
 
Katika hali inayoleta matumaini kituo cha haki na sheria kimeishaki serikali katika mahakama ya icc.

Akizungumzia hatua hiyo bibi helen kijo,alisema hatua hiyo ni ya mwanzo na hawatarudi nyuma hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono.

Bibi kijo amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kufanya uchunguzi wa mauwaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi na kusema wamefungua pia shauri kama hilo katika mahakama ya africa.

Amesema kitendo cha serikali kuwahamisha watendaji wanaofanya mauwaji hayo na kuwapeleka sehemu nyingine bila kuwawajibisha hakivumiliki na kuwa hawata kaakinya mpaka watendaji hao watakapo wajibishwa na sheria kufata mkondo wake.

Huku akitolea mfano wa kamanda wa mkoa wa iringa aliye hamishiwa iringa kwa kosa la mauwaji
na kurudia kitendo kilekile cha kuwauwa raia wasio na hatia na mpaka sasa hajachukuliwa hatua yoyote,huku serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani kwa kitumia kodi za walalahoi wakijaribu kuficha ushahidi.

Bibi kijo amesema ni lazima serikali iwawajibishe wote waliohusika na mauwaji ya watanzania na kusema si iringa pekee,ni pamoja na mikoa yote ambayo mauwaji kama hayo yalipotokea.


Mama unatumika vibaya , wanakutumia kisha watakuacha wakiisha timiza matakwa yao, CDM mpooooooo? naona mmeamua kutoka kivingine safari hii
 
Huyu mama ninamashaka nae, Baada ya kusikia kwenye majarida na vyombo vya habari vya kimataifa juu ya kuletwa kwa wachunguzi TZ, naona akapata sehemu ya kudandia hapohapo (ili ionekane taasisi yake inafanya kazi), ila nimeshangaa mauaji yote hayo ya watu zaidi ya 35 tangu utawala wa kikwete ukamate dola, kumekuwepo pia na unyanyasaji wa raia na ukiukwaji wa haki za binadamu wa hali ya ya juu Tz.Ila muda wote huo alikuwa anapiga tuu kelele tuu (kuwaridhisha wafadhili wa taasisi yake kuendelea kunyonya dolla tu) na hakuna action yoyote.Ngoja tuone!!
 
Asante sana mama Helen Bisimba. Usiogope, sema hata wakikuua but umeacha legacy mama si kama hawa madhaifu na wauaji wakifa tutawakumbuka kwa wizi na mauaji yao. Go mama Go!!
 
Tangu sasa katuhesabu sisi vijana kuwaungeni mkono katika kila hatua ya harakati hizi za kutafutia haki marehemu wetu na watoto yatima walioachwa nyuma kujiandaa kushika kibakuli kuwa omba omba mi-barabarani.
 

Mama unatumika vibaya , wanakutumia kisha watakuacha wakiisha timiza matakwa yao, CDM mpooooooo? naona mmeamua kutoka kivingine safari hii

Pole sana kila mtu anauona uovu wa SSM, hata mtoto mdogo. Nimepigiwa simu na ndugu yangu sasa hivi kuwa mtoto wake mdogo wa miaka 6 anasoma academy moja mbagala wakati wanarudi vurugu mtindo mmoja na mabomu mtoto amefika nyumbani hana amani anasema presha inapanda hadi ameingia chooni kujisaidia kwa ghafla na anamwita dada aangalie kama kweli tumboni hazitoki risasi anavyofikiri yeye. Sasa nchi kama hii ambayo inapoteza ile amani na usalama wa watanzania unataka ipongezwe? Use your common sense. Achana na ushabiki wa chama hauna lolote. Chadema is for the people na wale ambao ni for the people kama huyu mama ni lazima akemee. Da kweli akili nyingine kazi.
 
Serikali haishitakiwi ICC! Hii ni mahakama ya makosa ya jinai ya kimataifa, inahukumu watu tu, haina jurisdiction juu ya States... Sema wame-apply for investigation, and that's upon the Prosecutor to accept or decline entering into oinvestigation.

No the prosecutor has no jurisdiction to commence investigation or deny the investigaation.. the only body under the ICC which even the prosecutor is subject too is the so called pre-trial chamber hiyo ndio inampa go ahead mwendesha mashitaka kuanza uchunguzi wakiona inafaa...hivyo kusea jurisdiction ni ya prosecutor sio sahihi kwa sababu hiyo chamber inaweza kutaka yeye achunguze hata kama yeye hajasema. Nakubaliana na wewe kwamba only individual are subject to ICC but viongozi wanashitakika take reference to ocampo 4 wa kenya.
 
No the prosecutor has no jurisdiction to commence investigation or deny the investigaation.. the only body under the ICC which even the prosecutor is subject too is the so called pre-trial chamber hiyo ndio inampa go ahead mwendesha mashitaka kuanza uchunguzi wakiona inafaa...hivyo kusea jurisdiction ni ya prosecutor sio sahihi kwa sababu hiyo chamber inaweza kutaka yeye achunguze hata kama yeye hajasema. Nakubaliana na wewe kwamba only individual are subject to ICC but viongozi wanashitakika take reference to ocampo 4 wa kenya.
 
untitled.jpg
Na: Rodrick Maro
Ndugu zangu;

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinasikitishwa sana na mauaji yanayoendelea kufanywa na vyombo vya dola hususan vyombo vya ulinzi na usalama bila hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watuhumiwa wa ukiukwaji huo wa haki ya kuishi.

Tangu mwaka 2001 hadi sasa, LHRC tumekuwa tukifuatilia matukio mbalimbali ya kuuawa kwa raia yanayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama. Hivi karibuni, mnamo tarehe 2 Septemba, 2012 tulishuhudia mauaji ya kinyama kule Iringa yaliyofanywa na polisi kwa kutumia kile tunachosadiki kuwa ni ‘bomu la machozi' kwa kumuua mwandishi wa habari ndugu Daudi Mwangosi.

Leo hii, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimetoa taarifa baada ya uchunguzi na kufuatilia mwenendo wa matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu, hususan ukiukwaji wa haki ya kuishi (waathirika wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola).

Taarifa rasmi imeambatanishwa. Kwa mfano kwa mwaka huu tu hadi mwishoni mwa mwezi wa tisa takwimu za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu zinaonyesha kuwa tayari watu 24 walikwisha uawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama. Baadhi ya sababu ni kushindwa kuhimili siasa za vyama vingi na ukosekanaji wa uvumilivu wa kisiasa.

Pia, kushindwa kuwa na mipango shirikishi ya kiusalama katika maeneo ya uwekezaji hususan kwenye migodi na kwenye hifadhi za taifa. Baada ya kutafakari na kuangalia uwajibikaji wa viongozi wa nchi hii, Kituo kimechukua hatua zifuatazo, baina ya nyingine: ·

Kupeleka malalamiko kwa Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola (UN-Special Rapporteur on etra-judicial killings). Kumtaka mjumbe huyu kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki kwa serikali ya Tanzania. Taarifa ilipelekwa tarehe 28 Septemba 2012. Na tayari ameshaanza kupitia malalamiko ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu; ·

Kupeleka malalamiko kwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa (ICC Prosecutor) na kumtaka kufanya uchunguzi na kuona hatua anazoweza kuchukua, Tarehe 28 September 2012; · Kupeleka suala hili kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za Watu katika kikao chake cha mwezi wa Oktoba 2012, kule Ivory Coast na kuitaka Tume kuchunguza na kuchukua hatua ikiwemo kulipeleka suala hili Mahakama ya Afrika; ·

Taarifa hii pia imepelekwa kwa wadau wengine mbalimbali wa haki za binadamu kama Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) na Ofisi za umoja wa mataifa Tanzania kwa hatua mbalimbali.

Nchi hii inaheshimu utawala wa sheria na katiba. Katika haki zilizoainishwa kwenye katiba ibara ya 18 ni haki ya kutoa maoni na uhuru wa mtu kushirikiana na wengine ibara ya 20. Matumizi ya mikutano ya hadhara na maandamano yenye kufuata taratibu za kisheria ni njia mojawapo ya demokrasia.

Hivyo ipo haja kwa serikali kutoa taarifa na habari kwa umma kuhusu juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuwalinda wao na mali zao, kuwaletea maendeleo na kupunguza ugumu wa maisha.


Attention:
Mikael P Aweda, KASPERSKY ANT- CCM mleta mada tunatanguliza shukrani kama habari hii hapa utaiweka ukurasa wa mbele ili kuleta uzito wa ujumbe huu. Tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom