LHRC yaishtaki serikali ya Tanzania ICC

untitled%25282%2529.jpg

untitled%25283%2529.jpg

Huu ni uthibitisho wa habari hii kwamba hatua za awali zimechukuliwa ili uchunguzi wa vyombo vya kimataifa ufanyeke kabla ya hatua stahiki kuchukuliwa kimahakama kwa wahusika na mauaji haya.

Binafsi nimefurahia jambo hili kwa vile ni mwanzo mzuri wa demokrasia kuanza kupata nafasi yake baada ya kubanwa mno na serikali yetu kwa visingizio ambavyo vinapingana na katiba ya nchi.
 
Mkuu lazima wawepo wahusika
Kenya akina UHURU KENYATA na WILIUM RUTO, Riberia CHARLES TELLOR, Ivory Coast GBAGBO nk

Sijui umegundua nin, hasa kwa jiran zetu wakenya?

Sasa kwa case hii ya kina Mwangosi, Ulimboka n.k nani atashtakiwa , Kikwete au Waziri wa mambo ya ndani au Mkuu wa majeshi ya Polisi?
 
Sasa kwa case hii ya kina Mwangosi, Ulimboka n.k nani atashtakiwa , Kikwete au Waziri wa mambo ya ndani au Mkuu wa majeshi ya Polisi?

Ulimboka ni ngumu kidogo kwa sababu ya kutokuwepo ushahidi wa wazi ingawa mazingara yanaashiria uwezekano.

Mwangosi pasi shaka viongozi wa jeshi la polisi Michael Chamuhada wanted number one.
 
wasiishie kukusudia bali washitaki natupo nyuma kwa kuwapa support za kila hali
 
Safi sana,ni lazima wote waliohusika wawajibishwe na itakuwa funzo kwa hi serikali legelege ya CCM inayotumia vitisho na risasi za polisi kuwaua watanzania waliopo kwenye nchi yao
 
Sasa kwa case hii ya kina Mwangosi, Ulimboka n.k nani atashtakiwa , Kikwete au Waziri wa mambo ya ndani au Mkuu wa majeshi ya Polisi?

1. Kwa mwangosi aliyesimamia mauwaji ni KAMUHANDA. (Kule kenya waliosimamia hasa ufadhili ni Uhuru na Ruto)

2. Kwa ulimboka mwanasheria wa serikali ashitakiwe kwa kushindwa kumfikisha Rama mahakamani si ushahidi wa

mawasiliano upo, lakini hapa Ulimboka atakuwa shahidi muhimu.

3. Morogoro kama irivyo kwa Kamuhanda, mkuu wa polisi na kule Arusha.

Serikali itawajibika kuwapeleka na kujitetea kwanini haikuwachulia hatua, hapo tena yawezekana mengine kufumka

itategemeana na wanasheria wameitengenezeje kesi.

Tuwaachie wanasheria mimi si mtaalamu wa hizi anga mkuu.
 
JAMANI, nimeshindwa kumuelewa huyu mama. anasema amepeleka malalamiko yake ICC kwa prosecutor ili prosecutor aangalie hatua stahiki anazoweza kuchukua dhidi ya tz juu ya masuala mbalimbali yanayotokea likiwepo lile la mwangosi. hivi huyu mama ana uelewa gani wa sheria za jinai za kimataifa? hivi anafikiri watachukua hatua yeyote? alienda kivipi? officially au alikutana naye wakati wa kunywa chai kwenye mgahawa? kama alienda officially kushitaki au kufungua shauri kama alivyokuwa anasema kipindi kile, ametumia procedure ya sheria ipi na nani atayazingatia anayopeleka? au wataweka kapuni? why nasema hivi?
  1. only states, security council or the prosecutor himself can initiate that, no individual person is allowed by the statute to do it.
  2. tayari serikali ya tz imeshachukua hatua stahiki ikiwamo uchunguzi pamoja na kumpeleka muuaji mahakamani kujibu shitaka, kitu kitakachowalinda viongozi wote wa tz akiwamo hata yule kamanda wa iringa, icc kama nchi imechukua hatua stahiki kama hizi haina ubavu kuingilia under article 17.
  3. kesi karibia zote ambazo zimeshatokea tz, ukiondoa ile ya zanzibar mwaka 2000, hazikolifai kwa kosa lolote lile pale icc, i mean, hakuna tukio lolote lile linaloweza kuangukia kwenye genocide, crime against humanity au war crime....hata kama crime against humanity ingekuwepo lakini tayari serikali hii imeshachukua hatua stahiki, na huwezi sema mbona wanawalinda tu, kesi bado iko mahakamani.
  4. hata mwaka mmoja haujaisha, limit ambayo imewekwa ili kuona kama nchi itachukua hatua au la. kama haijachukua hatua basi icc itaingia kuanza uchunguzi. hivyo hata kama amefanya hivyo, icc imefumbwa mdomo hawawezi kufanya chochote hapa kwa sasa.
  5. si kila mauaji au kosa icc inaweza kuingilia kati. kuna makosa mengi ambayo hayana gravity kubwa icc imeziachia nchi zishughulikie...icc inapokea tu yale makosa ambayo ni serious crimes of international concern, hayo matatu tu, na makosa haya yana element zake. hivyo hata kama angefanya nini, watu wakakamatwa hapa tz wakapelekwa kule, mawakili watakaowatetea watakuwa na kazi ndogo sana na kuwachomoa haraka....mwanzoni kabisa wakati wa pre-trial ili kujua admissibility yake pale.
  6. MAMA AMEENDA KUTUAIBISHA TU WATZ KULE KUONEKANA HATUJUI SHERIA. pale kwa AG kuna wanasheria waliobobea katika hili, ndio maana walishamshauri NCHIMBI aweke tume haraka na yule kijana kule iringa akamatwe afunguliwe mashitaka haraka. kufanya hivyo ni defence kubwa sana mbele ya icc na ni kuifanya icc kutokuwa na meno kwa tz katika tukio hilo. mama huyu anatakiwa aende hata course tu ya sheria za jinai ya kimataifa, kuliko kuwa mwanasiasa ambaye hajui anachokifanya.
NB: mimi si mwana ccm, wala si kiongozi yeyote yule wa polisi wala ngazi za juu. ni wakili wa kujitegemea. wala msihangaike kusema kuwa natetea ccm na uongozi wake hapa. msipoteze muda huo.

pekee alichofanya ambacho naweza kumsifu ni kwamba, kwa kufanya hivyo anakuwa kama amewapiga mkwara viongozi wetu, amewaweka aware ili wajue kuwa wakifanya hivyo wanaweza kufikishwa the hague siku moja. ila kwamba kwa yaliyotokea hadi sasaivi yata effect yeyote mbele ya icc, mama hapo amepotea na anatuaibisha watz kuonekana hatujui sheria za kimataifa.
 
Kwa maoni yangu wewe ndio unatuangusha watanzania kwa kuamini kuwa hatua inazo chukua serikali ya tanzania ni zenye nia ya kweli kutaka kuwawajibisha wabakaji wa DEMOKRASIA.Alichofanya huyu mama kinamkumbusha mwendesha mashtaka wa ICC kuanza kitupia macho serikali ya tanzania kwani amepata mahali kwa kuanzia. kimsingi siyo lazima yatokee mauaji ya halaiki ndio ICC waingilie.WEWE UMETUAIBISHA WATU WOTE TUNAO JUA KUSOMA NA KUANDIKA KWA KUANDIKA MAMBO MENGI YENYE DHAMIRA YA KUITETEA SERIKALI DHAIFU YA CCM.Haya ni mapambano,silaha yeyote inayo weza kusaidia kumshinda adui itumike tu,
 
angalia kwenye red alafu ujitathimini mwenyewe kama unakijua ulichoandika. umepotoka aisee, si kila kosa icc inaingilia kati, na wewe utakuwa shahidi wa wengi katika hili, utaona kama icc itachukua hatua yeyote, amini usiamini, nothing is going to happen, the only thing ambacho amekifanya huyu mama ni kuiweka aware selikali ili ijue kuwa kuna siku wanaweza kujikuta wamefikishwa kule hivyo wawe makini na operation zao..lakini si kwamba kwa haya ambayo yameshatokea kuna lolote litafanywa na icc. you very wrong aisee.

unasema sio lazima yatokee mauaji ya halaiki (ukimaanisha crimes against humanity), ni kweli, mengine ni mauaji ya kivita na mengine ni mauaji ya kimbari. ni hayo matatu tu. sasa niambie kwa makosa hayo matatu ambayo icc inashughulikia (kimbari, ya kivita na halaiki), lipi kati ya hilo linaweza kuinasa tz kama unazijua element za makosa hayo? hapo huna jibu kwasababu unapoongea haujui nini maana na ingredient gani zinaunda kosa moja baada ya lingine kisheria, hapa hatuendi kwa siasa, tunaenda kwa sheria na vigezo vyake aisee...fafanue nini unaelewa na makosa hayo na kama icc ikija tz tutashitakiwa na makosa gani...nakupa iyo kazi uifanye.
 
Huyu mama ni mpuuzi matatizo ya Watanzania tunayamaliza wenyewe anajitafutia umaarufu wa kipumbavu.Damn
 
Mkuu naona umekuja kivingine tena kwa Issue hii hii... Mwanzoni uliapa abadani asilani kuwa hawezi kwenda,Ukataka uelezwe nyia atakazopita;Tukakushtukia tukakuacha bila majibu. Sasa ameenda,Bado unauliza maswali yale yale kwa njia nyingine.
Binafsi sijui ni nini kinachokufanya ulalamike sana juu ya hii issue. Labda nikueleze jambo dogo sana la kukusaidia; UKISHINDWA KUFANYA JAMBO KWA AJILI YA NCHI YAKO,AKIFANYA MWENZAKO ULICHOSHINDWA KUFANYA KWANZA UNAPASWA UMPONGEZE NA SI KUMTUSI NA KUMKEJELI.
 
hata kama amekosea njia,bado sielewi hilo povu linalomtoka mleta mada linatoka wapi! Huyu mama apongezwe,halafu tuangalie wapi kakosea ndipo mjadala uanze..kulalamika tu hakukusaidii sijui mauaji yanamsaidia nin mleta mada
 
Back
Top Bottom