LHRC yaishtaki serikali ya Tanzania ICC

Alichokifanya Mama Kijo ni hatua kubwa sana mbele,si lazima icc wachukue hatua lakini walau serikasli ijue watanzania wanajua haki zao zitapatkana wapi,lakini pia hata kama icc hawawezi kuchukua hatua walau watajua Tanzania kuna jambo baya linaendelea mwisho wa siku wakifikishwa huko vongozi wetu.
 
huyu mama is my hero, i wish Tanzania tungekuwa na watu kama yeye mia moja kwa maana wangejuwa kuwa people are watching them and stop killings.
 
Nampongeza huyu mama kwa hatua aliyochukua, sina sababu ya kumkejeli. Message yake itaamsha kitu fulani ......na hivyo jumuia ya kimataifa itajua jambo linaloendelea kwa chini chini ndani ya nchi yetu. Binafsi sipendezwi na tabia za viongozi wetu kutumia mahakama kuendesha kesi za kisanii.
Mahakama za TZ sio sehemu ambayo kuna uhakika asilimia 100 kwamba utapata haki, japo inatokea mara moja moja.
 
hata kama amekosea njia,bado sielewi hilo povu linalomtoka mleta mada linatoka wapi! Huyu mama apongezwe,halafu tuangalie wapi kakosea ndipo mjadala uanze..kulalamika tu hakukusaidii sijui mauaji yanamsaidia nin mleta mada

Mleta mada niliwahi kumuuliza huenda na yeye ni sehemu ya walalamikiwa! Hajui kabisa kuongea mbele za watu!
 
Kuna aibu kubwa kama ya rasilimali ya nchi yako kuporwa mchana kweupe? Acha aibu WAKILI JINA!
 
JAMANI, nimeshindwa kumuelewa huyu mama. anasema amepeleka malalamiko yake ICC kwa prosecutor ili prosecutor aangalie hatua stahiki anazoweza kuchukua dhidi ya tz juu ya masuala mbalimbali yanayotokea likiwepo lile la mwangosi. hivi huyu mama ana uelewa gani wa sheria za jinai za kimataifa? hivi anafikiri watachukua hatua yeyote? alienda kivipi? officially au alikutana naye wakati wa kunywa chai kwenye mgahawa? kama alienda officially kushitaki au kufungua shauri kama alivyokuwa anasema kipindi kile, ametumia procedure ya sheria ipi na nani atayazingatia anayopeleka? au wataweka kapuni? why nasema hivi?


  1. MAMA AMEENDA KUTUAIBISHA TU WATZ KULE KUONEKANA HATUJUI SHERIA. pale kwa AG kuna wanasheria waliobobea katika hili, ndio maana walishamshauri NCHIMBI aweke tume haraka na yule kijana kule iringa akamatwe afunguliwe mashitaka haraka. kufanya hivyo ni defence kubwa sana mbele ya icc na ni kuifanya icc kutokuwa na meno kwa tz katika tukio hilo. mama huyu anatakiwa aende hata course tu ya sheria za jinai ya kimataifa, kuliko kuwa mwanasiasa ambaye hajui anachokifanya.

NB: mimi si mwana ccm, wala si kiongozi yeyote yule wa polisi wala ngazi za juu. ni wakili wa kujitegemea. wala msihangaike kusema kuwa natetea ccm na uongozi wake hapa. msipoteze muda huo.


Nampongeza huyu mama kwa hatua aliyochukua, sina sababu ya kumkejeli. Message yake itaamsha kitu fulani ......na hivyo jumuia ya kimataifa itajua jambo linaloendelea kwa chini chini ndani ya nchi yetu. Binafsi sipendezwi na tabia za viongozi wetu kutumia mahakama kuendesha kesi za kisanii.
Mahakama za TZ sio sehemu ambayo kuna uhakika asilimia 100 kwamba utapata haki, japo inatokea mara moja moja.

UBUNGOUBUNGO! Kumbuka kuwa kuna msemo wa utadanganya watu wengi lakini si siku zote! Ila kwa hili ulilolileta hapa, naona umekuja kupima kiwango cha hasira walichonacho wafa na tai shingoni. Binafsi sitaki kuelewa unasali wapi, unamuunga mkono nani na unamtetea nani? Kivyako!
Kwanza tafakali hayo maneno yako niliyowekea RED halafu utwambie nini maana yake.

INVESTA, MAMA KIJO+ na wadau wote mliochangia>SALUTE. Muacheni huyu pumba kwani naye ni walewale wanaosema kuwa wana interijensia ya kuona mipango ya matukio ya uharifu kote duniani halafu kesho wanauawa wao, sijui camera zao zinakuwa zimezimwa?
Kama unatoka kwa AG au unajitegemea ipo siku ukweli utaonekana. Pole na msiba.
 
Iam not sure kama wana weza kutusaidia kwa hili suala. Sina imani na utendaji wa hii mahakama ICC lazima tujue ni mambo mangapi watatua na mangapi wameshindwa kutatua. Hapa tupambane wenyewe kwanjia yoyote then tukishindwa tufikie hapo.Mimi siamini kama nikweli tumeshindwa kuidhibiti serikali ambayo tume iweka sisi wenyewe Kwenda huko ni dalili yakushindwa na kama ICC itashindikana tufanye nini sisi waTANZANIA hapo tukubaliane kujitoa muhanga kupigania haki kwa kuingia barabarani mpaka kieleweke. Huu ni mtizamo wangu.
 
Awamu ya kwanza ya ukoloni ilikwishapita na kuzikwa. Ikaja awamu ya pili ambapo nchi huru zilikiona cha moto kwa kupunduliwa mfululizo kutumia vibaraka wanajeshi wengi wakiwa hawana elimu kama wakina idd amini, bokasa, na wengine. Tanzania ilipona kwa sababu mwalimu alijiwahi na kuanzisha usalama wa taifa ambao ni jabari linalowanyima usingizi vikaragosi wanaotaka kututia kwenye machafuko ilimradi watimize malengo ya uchu wao. Awamu ya tatu ya ukoloni ilikuwa ni kuwaandaa mafashisti kama savimbi naafonso dhlakama kuendesha vita za wenyewe kwa wenyewe nayo ikakoma bila mafanikio. Serikali huru za mozambique na angola kwa kusaidiwa na wakina baba wa taifa hayati mwalimu nyerere iliweza kuwasambaratisha. Awamu mpya inakuja na visingizio vya demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Hii ilifanikiwa nchi za misri na libya, lakini ivi sasa wanajuta na wanakula dhambi zao za kujkomba kwa wazungu. Icc ni kati ya taasisi zinazotumuka kuhalalisha huo udhalimu wa kuzivuruga nchi za afrika. Ndo maana hata huyu eleni kisima hawezi kuipeleka marekani au uingereza huko. Sasa hii kali kuuwawa kwa mwangosi huyu mama kisima anataka kuipeleka tanzania icc. Je atafaidika na nini?? Anatumwa au anatumiwa na nani?? Akishafungua kesi tutaanika mpango mzima kwenye hii jf watanzania waamke usingizini wajue wanaishi na watu wa namna gani na wanataka kutupeleka wapi.
 
Mama Helen Kisima anatafuta nini ICC ni kitu gani akikueleweka mpaka akaipakazie nchi kwenye mataifa ya nje??. Hii ni hatari kwa rekodi ya nchi na kama unadhani hawa pua ndefu wanaitakia mema Afrika endelea kupeleka hizo kesi kuna siku utaelewa kuwa hawakutakii mema
 
Safi sana mama kijo keep it up. Tanzania inahitaji watu wa dizaini hii kufanya mabadiliko ya kweli
Katika hali inayoleta matumaini kituo cha haki na sheria kimeishaki serikali katika mahakama ya icc.

Akizungumzia hatua hiyo bibi helen kijo,alisema hatua hiyo ni ya mwanzo na hawatarudi nyuma hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono.

Bibi kijo amesema kuwa wameiomba mahakama hiyo kufanya uchunguzi wa mauwaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi na kusema wamefungua pia shauri kama hilo katika mahakama ya africa.

Amesema kitendo cha serikali kuwahamisha watendaji wanaofanya mauwaji hayo na kuwapeleka sehemu nyingine bila kuwawajibisha hakivumiliki na kuwa hawata kaakinya mpaka watendaji hao watakapo wajibishwa na sheria kufata mkondo wake.

Huku akitolea mfano wa kamanda wa mkoa wa iringa aliye hamishiwa iringa kwa kosa la mauwaji
na kurudia kitendo kilekile cha kuwauwa raia wasio na hatia na mpaka sasa hajachukuliwa hatua yoyote,huku serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani kwa kitumia kodi za walalahoi wakijaribu kuficha ushahidi.

Bibi kijo amesema ni lazima serikali iwawajibishe wote waliohusika na mauwaji ya watanzania na kusema si iringa pekee,ni pamoja na mikoa yote ambayo mauwaji kama hayo yalipotokea.
 
Kwa viwango vya mauaji kwa RAIA kiholela hapa nchini katika mikono ya dola na bila kuchukuliwa hatua zozote za maana, Tanzania hatuko salama kama tulivyozoea huko nyuma.
 
Kuna watu humu walinitolea uvivu kwamba hii kitu haiwezekani, yako wapi sasa. Afadhali watu LHRC wamefanya kweli. Ni kutwanga kote kote, mtwango wa mwisho ni 2015
 
[h=2]
icca_logo.gif
[/h]








Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimba, akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamko lao kwa mauaji ya mwandishi wa Chanel Ten, Daud Mwangosi.


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewasilisha malalamiko kwa mjumbe Maalum wa Umoja wa Kimataifa kwa ajili ya mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo –Bisimba, alisema kuna matukio mbalimbali yamefanywa na dola na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa na serikali.

Alisema wamemtaka mjumbe huyo kufanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya serikali ya Tanzania.

Pia alisema wamewasilisha malalamiko hayo kwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ya Makosa ya Jinai (ICC), kumuomba afanye uchunguzi na kuona hatua anazoweza kuchukua dhidi ya serikali.

Alisema mauaji kwa raia yanayofanywa na vyombo vya dola yanazidi kuongezeka na kuhatarisha usalama wa wananchi.

Alisema wamewasilisha matukio mbalimbali ambayo yamefanyawa na vyombo vya dola katika mamlaka hizo ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwemo tukio la kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten, Daudi Mwangosi.

Pia alisema suala hilo wamelipeleka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na haki za watu katika kikao chake cha Oktoba mwaka huu huko Ivory Coast na kuitaka ichunguze na kuchukua hatua ikiwemo kulipeleka suala hili katika mahakama ya Afrika.

Bisimba alisema taarifa hiyo wameiwasilisha kwa wadau mbalimbali wa haki za binadamu ikiwemo Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) na ofisi za Umoja wa Mataifa.

Alisema kufuatia tukio la kuuawa Mwangosi, hakuna hatua za kuridhisha zilizochukuliwa licha ya kutolewa kwa ripoti tatu zilizofanya na timu maalum ya uchunguzi.

Timu hizo ni zile za Baraza la Habari Tanzania (MCT), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Emanuel Nchimbi.

Alisema kituo chake kinasikitishwa na ripoti iliyotolewa na kamati ya Nchimbi ambayo imeweka wazi mapungufu mengi ya serikali kwenye mauaji yanayofanywa dhidi ya raia.

Hata hivyo, alisema serikali haijajenga mfumo wa kujichunguza na kujiwajibisha yenyewe na kwamba katika tukio hilo, imeonyesha haikuwa na nia ya dhati kuchunguza mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi.

Alisema wanachokitaka nikuona uwajibikaji wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola waliohusika ikiwemo kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa mahakamani kwa wale wote waliohusika katika mauaji mbalimbali yaliyotokea.








CHANZO: NIPASHE
 
LHRC tusaidieni watanzania tunaopenda kutumia sheria kusuruhisha migogoro yetu kwa amani. Hatutaki kufikia 'liwalo na liwe ' ambalo serikali imeshatamgaza na ku-implement. Hakika kama sheria isipochukua mkondo wake liwalo litakuwa. Haiwezekani serikali kuua watu inaopaswa kuwalinda then wanakuja na taarifa zs uongo. mkuu wa nchi yuko kimya hata kukemea mauaji hayo hataki.

Mauaji ya mtu mmoja pasipo hatia ni mengi mno. Tusisubili mass killings ndo tuitafute ICC.
 
Back
Top Bottom