Lets talk science kwa leo: Kwanini mpaka leo hakuna chanjo ya mafua?

Lets talk science kwa leo: Kwanini mpaka leo hakuna chanjo ya mafua?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,267
Reaction score
102,461
Nadhani mafua( common colds) yamekuwepo tangu kuwepo kwa binadamu.
Pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, bado mpaka leo hakuna chanjo ya mafua.

Tatizo ni nini?

Tuchepuke kidogo siasa tupeane elimu juu ya mafua.
 
Hahahaaaa!!!

Chanjo ipo, tena inakuwa updated kila mwaka kwasababu virusi vya mafua vinabadilika (evolve) haraka.

Hapa kwetu haifiki kwa watu wote kwakuwa sisi ni masikini mno. Lakini wenyenazo wanaipata baadhi ya hospitali Dar na labda Arusha.

Google "flu shot".
 
Mimi nadhani umechanganya "common cold" na "influenza" au "flu".
Ni kweli zipo chanjo za influenza kama ulivyosema, lakini mwenye swali alitaka kujua chanjo ya common cold.
 
Mimi nadhani umechanganya "common cold" na "influenza" au "flu".
Ni kweli zipo chanjo za influenza kama ulivyosema, lakini mwenye swali alitaka kujua chanjo ya common cold.
Nimekupata. Unfortunately common cold ni mwavuli tu unatumiwa kuelezea ugonjwa wa mfumo wa hewa wa juu. Kuna zaidi ya virusi 160 vinavyosababisha common cold. Nadhani kupata chanjo hapo ni changamoto. Lakini pia common cold ni ugonjwa nafuu (watu hawaumwi sana wakipata) ukilinganisha na flu.
 
Nadhani mafua( common colds) yamekuwepo tangu kuwepo kwa binadamu.
Pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, bado mpaka leo hakuna chanjo ya mafua.

Tatizo ni nini?

Tuchepuke kidogo siasa tupeane elimu juu ya mafua.
Swali zuri, lakini lilitakiwa kuwa "Kwa nini hakuna chanjo ya virusi viavyosababisha mafua ya common cold".

Msingi wa rekebisho, ni kutokana na uwepo wa aina nyingine za mafua ambayo:
1: Hayahitaji chanjo(mzio).
2: Yenye chanjo kama infuenza nk.

Na kwa mkutadha huo, ujumbe nama 3 unahusika.

1: Ni kwa kiasi gani ugonjwa ni mhimu/madhara yake kwa binadamu na uchumi. Hapo ndo utaona mafua yanayoletwa na influenza kupata chanjo.

2: Gharama za chanjo zitaepusha hasara ya ugonjwa wa moja kwa moja kwa viumbe kwa kiasi gani?

3: Aina ya virusi vinavyosababisha common cold kuwa ni vingi/zaidi ya aina 200 na vyenye uwezo wa kujibadilisha kwa kasi kubwa.
 
Virusi vinavyo sababisha mafua ni vingi sana na huwa vinabadiika haraka sana kulingana na mazingira, ukitengeneza chanjo ya aina moja, lazima kitokee kingine kipya, ni mwendo wa non stop mutation tu.
 
Ngoja walokole na vijana wa TEC watoke kuabudu na kusifu, watasema Israel anazo zote sema bei yake sisi wamatumbi hatuiwezi wanauza ulaya, USA na china uko wanawategemea wao
 
Nasikia wazungu mafua huwa yanawaua! Au ni stori za mtaani tuu! 😊
Ni kweli ingawa msingi wake ni aina gani ya chanzo:
1: Mzio au allergy haina matokeo ya vifo
2: Virusi: hutegemea aina ya kirusi na ukali wake mfano: Infuenza au Covid(hii imeleta shida hata kwetu, ingawa kwa kiwango tofauti pia).

NB: Cha kuzingatia ni kuwa bado kuna mamilioni ya virusi huko misituni. Kadri tunavyoendelea kujichanganya bila tahadhari na wanyama wa msituni tutaendelea kuja navyo kwenye jamii.
 
mafua ni viral infection inayo sababishwa na wadudu tofauti tofauti na wanao badilika ndo maana utakuta mtu anamafua ya kubana, kesho ya kutiririka, kesho kutwa ya kupiga chafya ko inakua ngumu kutengeneza chanjo ya moja kwa moja na ndo maana hata dawa nyingi huwa zinatibu zile signs and symptoms
 
Back
Top Bottom