Kisura
JF-Expert Member
- Jun 21, 2007
- 364
- 26
Hata Hip-Hop Ilipoanza ilikutana na vikwazo vingi sana na muziki huu ulisemekena haukuwa bora lakini miaka ilivyoenda ndio mambo yakabadilika na muziki ukazidi kuboreshwa. Bongo Flava ni Muziki unaokuwa kila siku, tena kwa hivi sasa si Bongo tu bali ndio Muziki maarufu sana hata kwa nchi jirani kama Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda na hata baadhi ya sehemu za DRC Congo. Kila kitu kina mapungufu yake na hakuna ubaya kwenye kuchota utaalamu kutoka nchi nyingine.
Vijana wengi sana Tanzania wamejijenga na kujiajiri kimaisha kutokana na mafanikio ya muziki huu, nadhani kila mtu ana uhuru wa kusikiliza chochote anachopenda kama unaona Bongo Flava haikufai basi sikiliza aina nyingine ya muziki. Utakuta mtu anapiga madongo Bongo Flava lakini unakuta ndio huyo huyo anakuwa wa kwanza kusikiliza nyimbo kama Chicken Noodle Soup au Soulja Boy.
Chicken Noodle...that's funny!!!!Anyway, point taken.
Waeleze bwana. Hawajasikiliza lyrics na ngoma za vijana wa nyumbani hawa!