Leseni za Biashara kukwama kutolewa Songea, wahusika wanatengeneza mazingira gani?

D2050

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
1,902
1,067
Manispaa ya Songea inashindwa kutoa leseni za biashara kwa wakati, kumekuwa na tatizo hilo yapata mwezi sasa wafanyabiashara wanalalamikia Ofisi ya Afisa Biashara Manispaa ya Songea kushindwa kuwapa leseni za biashara zao.

Maafisa Biashara Wasaidizi wamekuwa wakiwajibu Wafanyabiashara wanaohitaji leseni hizo kuwa mtandao toka TAMISEMI unasumbua na ndio maana wao wanashindwa kutoa leseni kwa wakati.

Unajiuliza hivi Serikali kweli wapo makini katika kukusanya Mapato? Inawezekanaje kwa Dunia ya sasa mtandao unasumbua mwezi mzima? au kuna hujuma hapa au kutaka Rushwa?
 
Ina maana hao wafanyabiashara hawawezi kuomba hizo leseni mtandaoni ?
 
Huwezi kuomba leseni mtandaoni,kwasababu unatakiwa upewe namba ukalipie kwanza kisha waendelee kukuandalia leseni
Basi wangeweka namna ya kutengeneza control number mtandaoni ili watu wamalize kila kitu huko.
 
Basi wangeweka namna ya kutengeneza control number mtandaoni ili watu wamalize kila kitu hu
Wataibiwa wakiruhusu watu walio out ya mfumo kutengeneza control number,hapa kuna uzembe mkubwa sana kwenye hili jambo.
 
🤣🤣🤣🤣nilijua hii kitu mtandao unasumbua ipo Mbeya tu.

Alafu wenyewe wanatuonaga hatujui chochote kuhusu mitandao🤣😂😂😂
 
Back
Top Bottom