Serikali kufanya marekebisho Sheria ya Leseni za Biashara

SemperFI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
1,399
2,876
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, uchumi na mwenendo wa biashara, Serikali imeanza mchakato wa maboresho ya sheria ya leseni za biashara sura namba 208.

Huu ni mwaka wa 50 tangu sheria hiyo itungwe mwaka 1972, hivyo maendeleo ya sekta ya biashara yamesababisha haja ya mabadiliko yake.

Akizungumza kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo leo Septemba 14, Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andew Mkapa alisema hatua hiyo itajibu changamoto zinazojitokeza sasa.

“Kumekuwa na mabadiliko ya ulimwengu na sheria ilitungwa wakati ule kulingana na mahitaji yaliyokuwepo, lakini kwa sasa mambo yamebadilika inabidi tuwe na sheria inayoendana na sasa,” amesema.

Amesema mabadiliko hayo yametokana na pamoja na mambo mengine kuibuka kwa biashara za mtandao ambazo awali hazikuwepo hivyo sheria iliyopo haisemi chochote kuzihusu.

Amesema kwa sasa sheria hiyo inatekelezwa na BRELA na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo pia ndizo zenye mamlaka ya kutoa leseni hizo.

Kulingana na Mkapa, ukongwe wa sheria hiyo uliosababisha kuacha baadhi ya vipengele katika sekta ya biashara kwa sasa ndiyo sababu ya kubadilishwa kwake.

Amebainisha kuwa kikosi kazi kiliundwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa ajili ya kuandaa mapendekezo na sasa maoni yanakusanywa kutoka kwa wadau ili kuratibu mabadiliko hayo.

Sheria hiyo iliyorekebishwa mara 31 tangu kutungwa kwake, amesema ipo kimya kuhusu baadhi ya mambo ikiwemo wajibu wa anayepewa leseni.

“Sheria imeruhusu ukaguzi lakini haijaeleza nini kinapaswa kukaguliwa kwa hiyo kila mkaguzi akifika kwa mfanyabioashara anakagua kitu chake hii inasababisha mkanganyiko,” ameeleza.

Hata hivyo, amesema kwa sababu sheria haipaswi kuwa mgando, ndio maana mchakato wa mabadiliko yake umeanza sasa.
 
Ok9

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
4,411
3,848
Nilidhani yamesemwa yatakayobadilika ila nnachojua ni kuongeza wigo wa KODI tuu wala hakuna jingine na hii haimuumizi mfanyabiasha bali ni mlaji wa mwisho( mwananchi, mpigakura wenu)
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
13,294
10,664
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, uchumi na mwenendo wa biashara, Serikali imeanza mchakato wa maboresho ya sheria ya leseni za biashara sura namba 208.

Huu ni mwaka wa 50 tangu sheria hiyo itungwe mwaka 1972, hivyo maendeleo ya sekta ya biashara yamesababisha haja ya mabadiliko yake.

Akizungumza kuhusu mabadiliko ya sheria hiyo leo Septemba 14, Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andew Mkapa alisema hatua hiyo itajibu changamoto zinazojitokeza sasa.

“Kumekuwa na mabadiliko ya ulimwengu na sheria ilitungwa wakati ule kulingana na mahitaji yaliyokuwepo, lakini kwa sasa mambo yamebadilika inabidi tuwe na sheria inayoendana na sasa,” amesema.

Amesema mabadiliko hayo yametokana na pamoja na mambo mengine kuibuka kwa biashara za mtandao ambazo awali hazikuwepo hivyo sheria iliyopo haisemi chochote kuzihusu.

Amesema kwa sasa sheria hiyo inatekelezwa na BRELA na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo pia ndizo zenye mamlaka ya kutoa leseni hizo.

Kulingana na Mkapa, ukongwe wa sheria hiyo uliosababisha kuacha baadhi ya vipengele katika sekta ya biashara kwa sasa ndiyo sababu ya kubadilishwa kwake.

Amebainisha kuwa kikosi kazi kiliundwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa ajili ya kuandaa mapendekezo na sasa maoni yanakusanywa kutoka kwa wadau ili kuratibu mabadiliko hayo.

Sheria hiyo iliyorekebishwa mara 31 tangu kutungwa kwake, amesema ipo kimya kuhusu baadhi ya mambo ikiwemo wajibu wa anayepewa leseni.

“Sheria imeruhusu ukaguzi lakini haijaeleza nini kinapaswa kukaguliwa kwa hiyo kila mkaguzi akifika kwa mfanyabioashara anakagua kitu chake hii inasababisha mkanganyiko,” ameeleza.

Hata hivyo, amesema kwa sababu sheria haipaswi kuwa mgando, ndio maana mchakato wa mabadiliko yake umeanza sasa.
Kila wanachokuja nacho hakina baraka ya wananchi.

Mtu anaongea mabadiliko ya sheria kijumla jumla maana yake kuna kitu wamekificha ndani ya muswada ambacho ni ncha kali kwa wanaotamani kufanya ujasiriamali.

Nchi inanuka na imeoza kwa ufisadi na utendaji unaoichonganisha na wananchi wake.

Serikali inapaswa kwanza kuainisha kero wanazoziibua wananchi dhidi ya sheria na nna watakavyoziboresha ama kuzitatua kisheria. Serikali inayowaza kuvuna hafi kwa maiti ni serikali iliyofilisika kifikra na kiutendaji
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom