TensorFlow
JF-Expert Member
- Feb 11, 2020
- 812
- 969
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke haijaweza kutoa leseni za biashara kwa watu waliolipia tayari tangu wiki iliyopita. Binafsi ninasubiria leseni, hivi karibuni baada ya kufuatilia sana mara ya mwisho nilijibiwa hivi "wewe elewa kuwa huwezi kupata leseni kwa sababu vitabu hakuna na vinasubiriwa kutoka mkoani." Kimsingi nilikumbana na mlolongo wa majibu kama ifuatavyo tangu wiki iliyopita:
1. Anayetoa leseni ametoka.
2. Kuna shida ya mtandao kulipia.
3. Hakuna vitabu vya leseni.
Niliwauliza tatizo liko kwa nani ? Wakanijibu wewe elewa tu kuwa hakuna vitabu.
Wanachukulia issue kirahisi wakati wafanyabiashara wanalipia sehemu za biashara, hasa biashara mpya, na kuingia gharama zingine na kupata hasara kila siku bila kufanya biashara.
Raisi aliongea jana na kuhimiza kuwa vijana watafute ukwasi kwa kufanya biashara. Kuwa serikali haitoi ajira bali inatengeneza mazingira ya kujiajiri. Nilimwelewa sana.
Lakini Kuna mambo kama haya yanawaletea hasara na kuwarudisha nyuma vijana na watu wengine.
Rai: wahusika wafuatilie na kutatua hizi changamoto.