Rushwa na dhulma: Ukaguzi wa leseni za biashara Tegeta

LIVELIFE

New Member
Jan 31, 2022
2
0
Naeleza niliyoyashuhudia,

Nilipokea simu toka kwa Binti wa dukani kwangu, kwamba amekamatwa na anapelekwa Manispaa kwa kufanya biashara bila leseni. (Binti wa dukani alikuwa mgeni na Leseni ililipiwa,leseni inatolewa ndani ya siku tatu za kazi baada ya kulipiwa.

Zoezi la ukaguzi wa leseni lilianzia Madale mpaka Tegeta wazo hill (Urefu wa Kilometa 6 hivi) hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wasio na lesesi (labda ndio sababu ya kukodisha Coaster)-Picha Namba 1. Binti alikamatwa na kuwekwa kwenye hiyo Coaster safari ya kuelekea ofisi ya manispaa, Tegata Kibo Complex ilianza, gari ilijaa wafanyabiashara wengi (ishara ya wengi hawana leseni za biashara).

Nililazimika kuanza kulifuata hilo gari, Mile chache kabla ya kufika huko ofisini wafanyabishara makundi makundi walianza kushuka na mpaka kufika ofisi zao ni wafanyabishara watano tu waliofikishwa hapo.Kumbe wale Wengine walilazimika kutoa pesa Tshs 20,000 mpaka Tshs 30,000 kila mmoja na kuachiwa huru. Picha namba 2 na 3 Mfanyabiashara akiachiwa huru baada ya “kuongea vizuri na hawa wazalendo” hivyo hakupakiza kwenye gari.

Kulikuwana Askari mmoja, na wafanyakazi wanne-Picha Namba 4, wawili wanaume wawili wanawake. Wanaume wanakusanya pesa toka kwa waliokamatwa na kupakizwa kwenye gari.Wanawake wanakusanya pesa toka kwa wafanyabiashara waliofunga biashara zao.Ikumbukwe, kwenye kamata kamata kuna wafanyabiashara wanawahi kufunga maduka yao. Sasa Hawa wanawake ujificha ukifungua duka/biashara wanajitokeza na wanakusanya pesa pia.Ukikataa Polisi na wafanyakazi wengine wanaitwa kuja kukubeba. Hiki kikosi ni kibaya Zaidi.

Matokeo yake :
  • Wanaoshindwa kutoa rushwa, ndio wanao kwenda kupigwa fine ofisini kwao,
  • Mwenye biashara zenye mitaji mikubwa hawana leseni wenye mitaji midogo wana leseni, kwani hawa ndio upigwa fine.Hawana pesa za kutoa kila wakaguzi wakipita
  • Kuna matapeli, wanatumia mwanya huu huu kuchukua bidhaa, rushwa na kuwalazimisha watu kufunga biashara zao. Matapeli wanajifanya watu wa manispaa,
  • Matendo haya yanakatisha tamaa ya watu kufanyabiashara.
  • Manispaa inakosa mapato stahiki.
Kwenu Manispaa;

Hakuna namna ya kuhakiki leseni za kila Mfanyabiashara Kidijitali? au kwa nini serikali za mitaa zisihusike kwenye ukaguzi kwenye maeneo yao?

je wafanya biashara wote walioko Madale, Mivumoni, Salasala, Mbweni,Boko, Bunju Msigani, Kunduchi n.k wana leseni za bishara?.

Petro, huwa mnakusanya kiasi gani cha pesa toka kwa wafanyabishara maeneo haya, ni za kwenu tu au na walio juu yenu?.Bila shaka hii ni bishara yenye faida kubwa kwenu.

Asante jamiiforum, sikuwa na sehemu ya kuyasemea haya!

Hakika zama zimebadirika,
RIP JPM Mwana wa Africa
Jamani tuombeane uhai, kila mtu anapenda kuishi.

page.jpg
 
Back
Top Bottom