TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Kwa nini Mkuranga. sasa hivi kila tukio la mauaji Mkuranga. kuna nini huko. Tutashindwa hata kutembelea site zetu huko ukanda wa baharini, Mkuranga
 
HUU MWENDO SIYO.
::mwinyi
::mkapa
::kikwete
::wazee wa chama.
::NINI HIKI?
.
IMG-20190730-WA0102.jpeg
 
Kiwango cha uhakika wa kuishi nchini Tanzania kwa sasa ni kidogo sana.
Vyombo vya ulinzi na usalama ndio vya kuogopwa .
 
pole mno kwa wafiwa,BUT mtu ameripotiwa kupotea na jeshi la polisi linawajibu wanandugu wasubiri kwanza 72hrs ndio msako uanze,tukiambiwa tunaishi in a pithole country tunalalamika mno,common police mtu akipotea msako unaanza straight sio kusubiri,huyu atakuwa ni another Akwilina,tutamsahau punde ,maana sisi ni mahodari wa kulalama mitandaoni.
Angekuwa kapoteza police mwenzao msako ingeanza pale pale. Hata sijui utaratibu wa saa 72 umeanzishwa na nani. Hii inatutia shaka sana kuhusu utendaji wa jeshi letu la polisi.
 
yani anatumia US kama kigezo, hatari sana..
Kwa Marekani mtuhumiwa wa hayo mauwaji anayodai yanafanyika sio serikali. Ni mauwaji yanayotekelezwa na magenge ya uhalifu au watu waliochanganyikiwa na kutumia silaha vibaya

Zaidi ya yote matukio hayo yanachunguzwa kwa haraka na weledi na uma unaona wazi kua yanachunguzwa na wanakua na imani na vyombo vya uchungizi kwasababu havina hila

Jambo moja alilodanganya mchana kweupe ni kuhusu takwimu ya idadi ya watu aliyodai wanauwawa huko Marekani kwa kila dakika ipitayo! Watu hamsini kwa dakika!!!

Nadhani ni kosa la kimaadili kujenga hoja ya uhalalisha kuuwawa na kutekwa watu Tanzania kwavile tu na Marekani nako eti ni mambo ya kawaida!
 
Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopord Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.

Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.

Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.

Taarifa zaidi zinakuja
======

Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.

Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.

“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.

Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli.

Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.

Sasa hii hali inatisha. Itafikia mahali mtu yeyote atakaye kusimamisha mahali popote na kutaka kukuhoji upambane naye. Kwa sasa haijulikani ni wahalifu na wasio wahalifu.
Wanaoiongoza nchi na waliopewa dhamana ya kulinda watu kwa muda mrefu sasa wameshindwa kutolea maelezo yanayotokea kuhusu utekaji, hii imewafanya watu wahamini kuwa waliopewa hiyo dhamana ndiyo wanaofanyahayo.


Yawezekana huyu alikataa kufanya madudu fulani kazini kwake uli pesa chafu zipatikane, wakaamua kumwaondoa kupoteza ushahidi ili pesa zakampeni 2020 zipatikane
 
*MKURUGENZI Msaidizi wa miradi katika wizara ya fedha na mipango, Mhandisi Leopold Lwajabe (56), ameripotiwa kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.*

Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kigogo huyo mwandamizi katika wizara ya fedha, mwili wake umekutwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
“Niko hapa hospitali ya Mkuranga mkoani Pwani. Nimeona mwili wa ndugu yangu Leopald Kweyamba Lwajebe, ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti,” ameeleza Mugisha Bagoka Brassio, ndugu wa Mhandisi Lwajabe.
Anasema, “tumeambia na viongozi wa hospitali hii, kwamba mwili wa ndugu yetu uliletwa hapa hospitali na askari poli. Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kunyongwa shingo yake kwa kutumia kamba.”
Kwa mujibu wa Brassio, polisi wamemueleza kuwa mwili wa kaka yake huyo waliukuta kwenye kichaka ukiwa unaning’inia, huku shingo ikiwa imefungwa kamba.
Mhandishi Lwajabe alitoweka ofisini kwake, Alhamisi ya tarehe 25 Julai mwaka huu, baada ya kuwaaga wafanyakazi wenzake, kwamba anatakiwa kuripoti kituo cha Polisi cha Mburahati, kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
MwanaHALISI ONLINE halijaweza kufahamu, Mhandisi Lwajabe alikuwa anakabiliwa na tuhuma gani.
Mhandisi Lwajabe, kwa muda mrefu amekuwa mfanyakazi katika wizara ya fedha na mipango, akisimamia Idara ya fedha za Nje, kitengo cha mfuko wa maendeleo wa umoja wa Ulaya (EU).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mugisha Bagoka Brassio, ni kwamba kaka yake huyo alianza kupata misukosuko siku 10 zilizopita, baada ya kuhojiwa na polisi kwa masuala ambayo hakuyataja.
Anasema, “Jumanne ya tarehe 16 Julai 2019, majira ya saa tatu asubuhi, Mhandisi Lwajabe aliaga ofisini kwake, kwamba anakwenda kuonana na mtu aliyempigia simu. Hakurejea tena ofisini kwake.”
Anasema, kwa sababu ndugu yao hakurejea nyumbani, familia iliamua kutoa taarifa kesho yake, tarehe 17 Julai 2019 katika Kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dar es Salaam na walifanikiwa kufungua jarada la uchunguzi lenye Na. CD/RB/4122/2019.
Mwanandugu huyo anasema, jeshi la polisi liliwambia kuwa watulie na Polisi watafanya jitihada za kumtafuta na ikiwa hajarejea nyumbani baada ya saa 72, warudi tena kuripoti kituoni hapo.
Badala yake, Brassio anasema, “siku iliyofuata, watu wasiojulikana walimrudisha Lwajabe kwa gari na kumshusha nyumbani kwake, alfajiri ya Ijumaa, tarehe 18 Julai 2019.”
Taarifa zinasema, Mhandisi Lwajabe alinukuliwa akiwambia wanafamilia yake – kabla ya kufikwa na mauti – kwamba ameelekezwa na watu waliokuwa naye kuripoti kwenye kituo cha Polisi cha Mburahati kwa mahojiano zaidi.
“Tumefanya jitihada mbalimbali kumtafuta mpendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi Kituo cha Kati (Central Police Station), lakini hakuna tulichoambulia,” ameeleza Brassio.
Mhandisi Lwajabe anaingia katika orodha ya watu wanaodaiwa kutekwa na baadaye kupotezwa nchini na wanaoitwa na serikali, “watu wasiojulikana.”
Mhandisi Leopold Kweyamba Lwajabe, amezaliwa katika kijiji cha Ihembe, kata ya Ihembe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera. Ameacha mke na mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la Doreen Leopald Lwajabe.
 
Hembi tujiongeze kidogo.
Huyu kiongozi mkubwa namna hii ameona kuwa kuna tatizo kwa kuwa katika mikono ya Serikali lakini katika hali hii hakuna ndugu au rafiki au mfanyakazi mwenzake ambaye alikuwa anamsindikiza?
Hapa kuna jambo kubwa la binafsi ambalo hata marehemu hakutaka mtu yeyote ajue na aliamini kuwa litakwisha salama kwa maslahi yake binafsi na hasa ajira yake.
 
Awamu hii kama una mishe zako zinazokuingizia kipato ni vyema ukatulia, Mambo ya kujiingiza katika siasa mwisho wake ndio kama huu...

Kama huwezi kuisifia ni vyema ukaacha kujihusisha na siasa...

Apumzike kwa amani.
Alikuwa mwanasiasa huyu marehemu?
 
Back
Top Bottom