Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,985
Nilitokea mitaa ya Tazara na shida ilikua nifike Sokoni Buguruni ili kununua mazagazaga ya nyumbani, kwasababu ya foleni nikaamua kupiga teke tu.
Nilipofika pale kwa wauza mbao nikaamua kula 'chocho' upande wa kulia ili nitokee Sokoni.
Kiukweli nimejikuta nipo Malapa tena ni baada ya kuhangaika sana kuitafuta barabara ya Uhuru ili nisome ramani upya. Ilifikia wakati nikataka kuchukua pikpiki but nikasita maana pengine nipo sokoni tayari but ni kutafuta tu kaupenyo. Kwenye picha nimeweka mitaa ambayo nimeisaganya leo kwa masaa mawili!