Leo nimemuota Magufuli Amekufa, usiku wa kuamkia leo, Nikafadhaika sana. Hii maana yake nini?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,886
Wakuu Kwema!

Usiku wa leo nimefadhaika Sana, nimesononeshwa mno, nimepatwa na uchungu usioelezeka mpaka usingizi ukakata nikaamka yapata saa saba na dakika ishirini na mbili Kwa saa ya ukutani.

Mwaka Jana niliota ndoto ya namna hii hii lakini nikashindwa kuipandisha hapa kutokana na sababu kadha wa kadha, nilimuona Mzee Magufuli amefariki, kisha nikamuota na Mzee mwingine wa CCM naye kafariki Ila huyo Mzee mpaka sasa hivi ninapoongea yupo hai na hi mzima ea Afya. Sitamtaja, Ila ni mstaafu wa CCM katika nafasi ya Ukaribu taifa bara.

Nikirejea kwenye ndoto ya Leo inayonifanya niandike hapa;
Iweje niote mtu aliyekufa kafa tena?

Ndoto inaanzia tukiwa ofisini mahali, nikiwa na watu kadhaa waserikali. Ofisi ilikuwa kubwa yakutosha yenye meza za kisasa, ukutani ikiwepo picha ya Magufuli, pembeni kabisa kwenye dirisha likiwepo Sofa moja la watu Kama watano hivi lenye rangi ya ugoro la ngozi kwenye pembe lilikuwepo Ua sijajua ni ua bandia au ua kabisa.

Waserikali walikuwa watatu Mimi nikiwa wanne. Wawili walikuwa wamesimama, Mimi na mwingine tukiwa tumekaa kwenye viti(sio sofa)
Tukiwa tunapiga soga, punde bila kutarajia mlango wa Ile ofisi ulifunguliwa, akaingia mtu mmoja wa usalama akifuatwa na watu wa nne kisha Magufuli akafuatia. Mioyo yetu wote ikalipuka Sisi tuliokutwa mule ndani.

Mshtuko wetu ulisababishwa na kumuona mtu ambaye tunajua ameshakufa.
Tukiwa wote tumesimama Kama ishara ya heshima na adabu Kwa Rais, bado tukishangaa Magufuli WA kwenye ndoto akatusalimia Kwa matani Kama ilivyo desturi yake.

Kisha baadaye akasema hajafa, kama mtu anayejibu maswali yaliyomo mioyoni mwetu yaliyochorwa katika Sura zetu zenye wasiwasi..

Wakati akiwa anaongea, mlango wa pili unaoingia ndani kabisa kwenye ofisi zile, ukafunguka na akatokea mtu mmoja aliyevalia suti nadhifu akiwa kaongozana na mtu mwingine mwenye mwili wa kawaida Kama wangu. Walipotokea watu hao, nikashangaa kumuona Magufuli akishika katikati ya Kufua, akilalama kichomi, akilalama hivyo Kwa muda.
Mpaka machozi yakawa yanamtoka.

Wale watu aliokuja nao wakawa wanamshika ili kumpa msaada ili wambebe wamtoe pale wampeleke Hospitalini. Lakini akakataa, mwishowe akaanguka chini lakin kabla hajaanguka kabisa wakamdaka.

Alikufa.

Basi moyo wangu ukafadhaika Sana mpaka nikashtuka usingizini, bado nikiwa nimefadhaika.

Iweje niote mtu aliyekufa kafa tena?
Hii imekaaje kitaalamu.

Na Kwa nini moyo wangu ulifadhaika mno kiasi kile?
Wakati mwaka Jana, nilivyomuota Amekufa sikuwa na wasiwasi na hofu kama hivi leo?

Wataalamu wa tafsiri mje

Ndimi;
Taikon
 
Bas ndo amefanikiwa kufa kweli,maana ulimwenguni hapa kuna kunyakuliwa na mwanadamu na kunyakuliwa na Mungu,huenda alikowekwa huko kula pumba nako kakata moto

Mkuu najiuliza, Kwa nini nimefadhaika mno, unajua nikipata uchungu mno, mpaka naamka kitandani bado moyo wangu ulijazwa na mfadhaiko usioelezeka.
 
Jana nilipata ndoto Moja ya ajabu sana,

Nilikua kwenye boti moja ikatokea kwenye Boti hiyo alikuwepo Rais wa sasa ila alipokaa alizongwa na watu wengi sana na walinzi wake walikua wanajitahidi mno kuwaondosha wasimsonge ,

Katika jitihada hizo ikatokea boti kuyumba na kutaka kuzama lakini ikasimama ghafla na baada ya muda watu wakaanza kushuka lakini wengine hawakufanikiwa kwani mlango wa boti ulijifunga.
 
Mkuu Mimi majuzi niliota ndoto inayoshabihana na yako kidogo !niliota Magufuli yupo sehemu flan ya ovyo Sana amewekwa huku akiwa mgonjwa, akiwa anasikitika Sana, sehemu kwa kweli ilikua nyuma ya mbavu za mbwa kukiwa na sofa moja chakavu na kimeza.
Ikaja gari ya wagonjwa ikimchukua akiwa katika hali dhaifu Sana.
 
Back
Top Bottom