Leo nimemuota Magufuli Amekufa, usiku wa kuamkia leo, Nikafadhaika sana. Hii maana yake nini?

Kuota mtu aliyekwisha kufa akafa tena kunaweza kuwa na implication mbaya kwa mhusika, maana imeandikwa siku ya mwisho wafu watafufuliwa. Wale waliotenda mema wataingia kwenye uzima wa milele, waliotenda maovu wataenda jehanamu au kuzimu na hii ndo mauti ya pili, tujitahidi sana kuishi kwa kumtumainia Mungu Mwenyezi ili mauti ya pili isije kutupata...


Mkuu hiyo ndio Tafsiri yenyewe au?
 
Mkuu, siyo wote tuna vipawa tofauti. Mwingine anaota ndoto, mwingine anaona maono, mwingine anatabiri, mwingine miujiza, mwingine anafundisha, mwingine uponyaji, mwingine tafsiri za ndoto.

Wewe umeota ndoto kama wafalme na watu wengi kwenye Biblia waliota ndoto lakini hawakujua maana zake. Ilibidi watu wengine maalumu, (si kila mtu) watafstiri ndoto zile. kuna ndoto zilizotimia na kufanya madhara, kuna zingine zilikuwa zitimie lakini kwa kutumia vipawa mbalimbali vya watu wengine, waliojitambua, walichukua hatua na kubatilisha utimilifu wa ndoto na hivyo hazikutimia. Unaweza kuota ndoto yenye taswira nzuri lakini mchawi akijua, anaharibu utimilifu wa ndoto yako.
Kutokana na hizo kanuni batilishi, binadamu wasio na uelewa husema, zilikkuwa ndoto tu, hazikutimia n.k.

Ndoto isipotimia kuna maana nyingi na siyo lazima kwamba eti ilikuwa fake. Kuna viapwa vinaweza kubatilisha utimilifu wa ndoto.

Nimesoma ndoto yako, nimeelewa na nilichokifanya ndicho nilichotakiwa kukifanya katika hili..

Tusubiri nini? Kwamba mzee mgl afe naye ndipo tuanza kufanya nini? Kushangaa? kulaumiana? Kufanya nini?
Maombi haya nilyoyafanya yamebatilisha vitu vingi sana kwenye hiyo ndoto. Hutaona ikitimia kama ulivyoota. Ila ukitaka kujua kwamba ninachosema ni kweli, anza kufuatilia, utimilifu wa maombi nilyoomba na mikondo tuliyoelekezea uharibifu. Utawakumbusha wasomaji tena muda si mrefu.


Sawa Mkuu
 
Ndoto sio za kuamini sana,japo kuwa zingine huwa za kweli..kuna nyakati huwa naota ndoto za ukweli.
 
ni ndoto nzuri sana mkuu.ukibahatika kukutana na kiongozi wa nchi kwenye ndoto basi tegemea mambo yako yalifungwa yatafunguka utapanda cheo kama ulikuwa na kazi.au jambo lako lililokuwa linakutatiza litatimia.sebule kuwa na vitu manaake mafanikio kadri ulivyokuwa unaona vitu vingi sebuleni ndivyo mafanikio au jambo lako litavyokuwa.
 
ni ndoto nzuri sana mkuu.ukibahatika kukutana na kiongozi wa nchi kwenye ndoto basi tegemea mambo yako yalifungwa yatafunguka utapanda cheo kama ulikuwa na kazi.au jambo lako lililokuwa linakutatiza litatimia.sebule kuwa na vitu manaake mafanikio kadri ulivyokuwa unaona vitu vingi sebuleni ndivyo mafanikio au jambo lako litavyokuwa.


Nashukuru Sana Mfalme Njozi
 
Wakuu Kwema!

Usiku wa leo nimefadhaika Sana, nimesononeshwa mno, nimepatwa na uchungu usioelezeka mpaka usingizi ukakata nikaamka yapata saa saba na dakika ishirini na mbili Kwa saa ya ukutani.

Mwaka Jana niliota ndoto ya namna hii hii lakini nikashindwa kuipandisha hapa kutokana na sababu kadha wa kadha, nilimuona Mzee Magufuli amefariki, kisha nikamuota na Mzee mwingine wa CCM naye kafariki Ila huyo Mzee mpaka sasa hivi ninapoongea yupo hai na hi mzima ea Afya. Sitamtaja, Ila ni mstaafu wa CCM katika nafasi ya Ukaribu taifa bara.

Nikirejea kwenye ndoto ya Leo inayonifanya niandike hapa;
Iweje niote mtu aliyekufa kafa tena?

Ndoto inaanzia tukiwa ofisini mahali, nikiwa na watu kadhaa waserikali. Ofisi ilikuwa kubwa yakutosha yenye meza za kisasa, ukutani ikiwepo picha ya Magufuli, pembeni kabisa kwenye dirisha likiwepo Sofa moja la watu Kama watano hivi lenye rangi ya ugoro la ngozi kwenye pembe lilikuwepo Ua sijajua ni ua bandia au ua kabisa.

Waserikali walikuwa watatu Mimi nikiwa wanne. Wawili walikuwa wamesimama, Mimi na mwingine tukiwa tumekaa kwenye viti(sio sofa)
Tukiwa tunapiga soga, punde bila kutarajia mlango wa Ile ofisi ulifunguliwa, akaingia mtu mmoja wa usalama akifuatwa na watu wa nne kisha Magufuli akafuatia. Mioyo yetu wote ikalipuka Sisi tuliokutwa mule ndani.

Mshtuko wetu ulisababishwa na kumuona mtu ambaye tunajua ameshakufa.
Tukiwa wote tumesimama Kama ishara ya heshima na adabu Kwa Rais, bado tukishangaa Magufuli WA kwenye ndoto akatusalimia Kwa matani Kama ilivyo desturi yake.

Kisha baadaye akasema hajafa, kama mtu anayejibu maswali yaliyomo mioyoni mwetu yaliyochorwa katika Sura zetu zenye wasiwasi..

Wakati akiwa anaongea, mlango wa pili unaoingia ndani kabisa kwenye ofisi zile, ukafunguka na akatokea mtu mmoja aliyevalia suti nadhifu akiwa kaongozana na mtu mwingine mwenye mwili wa kawaida Kama wangu. Walipotokea watu hao, nikashangaa kumuona Magufuli akishika katikati ya Kufua, akilalama kichomi, akilalama hivyo Kwa muda.
Mpaka machozi yakawa yanamtoka.

Wale watu aliokuja nao wakawa wanamshika ili kumpa msaada ili wambebe wamtoe pale wampeleke Hospitalini. Lakini akakataa, mwishowe akaanguka chini lakin kabla hajaanguka kabisa wakamdaka.

Alikufa.

Basi moyo wangu ukafadhaika Sana mpaka nikashtuka usingizini, bado nikiwa nimefadhaika.

Iweje niote mtu aliyekufa kafa tena?
Hii imekaaje kitaalamu.

Na Kwa nini moyo wangu ulifadhaika mno kiasi kile?
Wakati mwaka Jana, nilivyomuota Amekufa sikuwa na wasiwasi na hofu kama hivi leo?

Wataalamu wa tafsiri mje

Ndimi;
Taikon
Ukiacha bangi utafika mbali dogo
 
Nilichojifunza hapa umetuambia namna JPM alivyokufa kumbe alilalamika kifua kinauma mpaka machozi yakawa yanamtoka then akadondoka wakamdaka ikawa ndio ntolee
.
Wewe ndio umejua mtoa mada kamaanisha nini. Katumia fasihi nzito mnoo kwa mtu wa kawaida kufahamu.
 
Back
Top Bottom