Uchaguzi 2020 Leo ni mwezi mmoja kamili toka kampeni zianze, CCM tu ndio inanadi Sera na Chama wengine wanajinadi wao binafsi kuwa nichague mimi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,906
51,924
Kampeni ni kunadi Sera na chama ili chama kishike dola.

Leo ni mwezi mmoja kamili toka kampeni zianze CCM tu ndio inanadi sera na chama wengine wanajinadi wao binafsi kuwa nichague mimi.

Kampeni kwao zimejikita zaidi kwenye u imimi sio chama ndio maana tunaona hata vyama vingine kama Chadema vikisema Zanzibar mchagueni Maalim Self hawasemi ichagueni ACT wazalendo na pia tumeona Act wazalendo ikisema Mchagueni Lisu haisemi ichagueni Chadema ishike dola nk.

Kawasikilize na mashabiki wa upinzani wengi wamelishwa u mimi kiasi kuwa hata hawajui kuna wagombea wengine wa ubunge na udiwani .Wengine hata hawawajui wanawajua Lipumba,Maalim.Self na Lissu tu.

CCM so far imekinadi chama na Sera vizuri. Sera ya mfano ya maendeleo ya vitu kama barabara miradi ya maji hospital nk ambayo wananchi wenyewe waliiomba kwa hiari yao maeneo husika inapokelewa vizuri. Tuendelee kushikilia hapo hapo na kuendelea kukinadi chama chetu na Sera zetu ili October 28 tupate kura zote za raisi wabunge na madiwani wa CCM kwa mpigo.

Jambo lingine ni kuwa kumekuwa na mwamko kichama kwa upande wa vyama wa wanachama kuhamasika kichama na kuonyesha wazi mhamasiko mkubwa wazi ni vyama vitatu tu vimeweza kwa wanachama wake kila ukitembea kuwaona wakiwa katika sare za vyama vyao kwa wingi mikutanoni kuonyesha kuwa kuna uhai wa chama kwenye mikutano inapogayika.

Chama cha CCM kinaongoza kwa uhai wa chama kwenye maeneo yote kampeni zimepita watu wamejitokeza kwa wingi na sare za CCM kwa Maelfu chama cha pili ni ACT-Wazalendo maeneo yao wanayopita mikutano yao wengi wanatoka na sare za chama chao unaona kuwa hapa pana uhai wa Chama.

Chama cha Tatu ni CUF hawa nao uhai wa chama unaonekana wazi maeneo wanayopita wanachama wenye sare waliohamasika ni wengi kwenye maeneo ya kampeni.

Chama ambacho kiko wazi kuonyesha uhai wa chama maeneo mengi haupo au umekufa kabisa ni Chadema. Ukifuatilia mapokezi kitu pekee ambacho Chadema inajitutumua kuonyesha kuwa uhai wa chama upo ni kuwagawia bodaboda wanazokodi bendera za Chadema wazifunge kwenye pikipiki wanaposindikiza msafara wa mgombea ambazo wakishamfikisha mkutanoni huzitoa na kurudi kuendelea na biashara zao. Lakini ukiangalia mkutano mzima unaona uhai wa chama hapo mkutano unafayika haupo ni watu tu wamekuja kusikiliza na kuondoka zao.

Sare za chama utaziona tu jukwaa kuu Lakini huhitaji kuwa mtaalamu wa political science kujua kuwa eneo hili mkutano wa unapofanyika uhai wa Chadema haupo.Chadema wanajivunia watu wasiwajua kujaa mkutanoni wanasahau kuangalia uhai wa chama hapo upo? Uhai wa chama ni muhimu eneo LA kampeni sababu umati wao ndio utaenda kunadi Sera za chama mtaani na kwao kwenye matawi yao kwa wale ambao hawakuja mkutanoni hivyo kuleta multiplier effect kubwa ya kupata wapiga kura wengi zaidi kuliko waliohudhuria mkutanoni.

Uhai mkubwa wa chama kwenye eneo ndio determinant factor kubwa ya ushindi
 
Wewe umeshindwa kumsaidia Mwenyekiti wako kujibu hoja umekuja na hoja nyepesi namna hii. Hoja zote za Chato, Mayanga na nk zote hizi hujasziskia? Pia wewe kwa ufahamu wako kuvaa sare za vyama ndy kukubalika? Sare zenu si mnagawaga bure?sasa ulitegemea mtu uliemtengenezea umaskini na ujinga kwa mda mrefu ukimdanganya kwa tishet na kofia atakataa? Leta hoja fikirishi katika nyakati hizi ili tujue mstakabar wa Taifa letu. Na sio tantalila hizi!
 
Sare zenu si mnagawaga bure?
2015 tuliona mwamko mkubwa wa kuvaa sare za Chadema uchaguzi mkuu watu walivaa nguo ,kofia hadi heleni ,raba,shanga za shingoni na viunoni akina mama zenye rangi ya bendera ya Chadema mlikuwa mkiwagawia bure?

CUF wanavaa sare na ACT wazalendo wanavaa sare wanagawiwa bure?
Chadema wanachama wamekibwaga kwa wingi .Tukutane October 28
 
kwenye mdahalo na Rais wa Ghana hilo jiwe lenu litakuwepo au atawakilishwa na Rasi simba?
n
Kwa hiyo Lisu anatafuta wapiga kura Ghana ha ha ha!! Kuna kitu kinaitwa concetrate on what matters most at a particular time.SAA hii kampeni za uchaguzi Tanzania Huyo raisi wa Ghana ni mpiga kura wake? Mwenzie kakulia Ikulu baba yake alishakuwa raisi Ghana yeye Lisu wa ikungi singida ndio anaona deal kuongea na raisi wa Ghana anaona kama kipofu kaona mwezi!!!
 
n
Kwa hiyo Lisu anatafuta wapiga kura Ghana ha ha ha!! Kuna kitu kinaitwa concetrate on what matters most at a particular time.SAA hii kampeni za uchaguzi Tanzania Huyo raisi wa Ghana ni mpiga kura wake? Mwenzie kakulia Ikulu baba yake alishakuwa raisi Ghana yeye wa ikungi singida na ndio anaona deal kuongea na raisi wa Ghana anaona kama kipofu kaona mwezi!!!
Hebu tuambie kada👷
Meko leo siku ya 4 hajafanya kampeni vipi kulikoni
 
2015 tuliona mwamko mkubwa wa kuvaa sare za Chadema uchaguzi mkuu watu walivaa nguo ,kofia hadi heleni ,raba,shanga za shingoni na viunoni akina mama zenye rangi ya bendera ya Chadema mlikuwa mkiwagawia bure?

CUF wanavaa sare na ACT wazalendo wanavaa sare wanagawiwa bure?
Chadema wanachama wamekibwaga kwa wingi .Tukutane October 28
Ulichoandika hapa "umemsaidia mgombea wako kujibu hoja kule jukwaani?"hivi huoni mda unaenda Kasi sana "mwokoeni mkubwa wenu hoja nzito kila siku znaongezeka na hazjibiwi!! Munalipwa bure kabisaa!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
This time around nchi ya ahadi tunaingia maana pharaoh wa kijani kashatepeta
 
Back
Top Bottom