Kuvaa sare za chama haimaanishi wewe ni mzalendo kwa nchi wala chama

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
253
629
Wakuu ni kwamba kila chama kina sare zake na zimekuwa zikivaliwa sana na makada. CHADEMA na magwanda yao huku CCM wakipendeza kwenye kijani na njano. Ni jambo jema kwa sababu sare zinapunguza sana matabaka kwenye mikusanyiko, mikutano na vikao. Kinachoniudhi ni tabia ya makada wengi wa vyama kudhani kwamba wanapovaa sare za chama ndo wazalendo kwa vyama na nchi.

Sitaiongelea sana CHADEMA kwa sababu ni chama kilicho kwenye mwisho wa uhai wake. Kuongelea chama kinachopigania uhai wake ni dhambi. Tuongelee makada wa CCM.

Kiukweli maigizo ni mengi sana na show off kwamba wao ni wazalendo huku nyuma ya pazia makada kibao wakiwa na tuhuma kibao. HAMKUMBUKI AHADI ZA MWANACCM? Zile sare zimekuwa kama kinga za kuficha maivu ya baadhi ya makada.

Hii tabia ya kudhani mzalendo kisa umevaa sare za CCM ife mara moja. Matendo yako ndo yanatakiwa yakutambulishe kuwa wewe ni mzalendo na sio mavazi.
 
Back
Top Bottom