Leo najihisi "guilty" sana moyoni

Latifaa

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
501
257
Yaani mapenzi sijui ni nini hata. Nimekuwa na mpenzi wangu kwa muda tunapendana na tuna mipango mingi. Nimeridhika naye sana sijawahi kuwaza kuwa ipo siku nitamsaliti.

Kuna kaka tunafahamiana muda kama miaka minne hivi kwenye mambo ya kazi na huwa tunaheshimiana sana. Kuna kazi fulani nilikuwa namsaidia mara kwa mara kishikaji tuu, cha kunishangaza huyu kaka kaanza kunitokea.

Nilimkatalia katakata nilijitahidi kumuonyesha sitamkubalia hata kwa dawa kwa jinsi nilivyokuwa namchukulia kama ndugu kabisa. Kweli nimeamini hakuna urafiki wa hivihivi kati ya mwanaume na mwanamke. Huyu kaka aliendelea kunisumbua bila kukata tamaa hatimae niliingia line.

Kwakweli hata kule kumgomea ilikuwa ni roho ngumu tuu maana ni mkaka mwenye sifa zote za mwaunaume. Wacha mahusiano yetu yaanze mambo yakawa moto nikajikuta nimefall in love hatari sio kwa kunicare kule. Sio mtonyo sio malavidavi nilipagawa naye kwakweli na ametokea kunipenda mno jamani nami namkubali mno amenichanganya sana.

Kinachoniuma nimeanza kufeel vibaya kwamba namsaliti mpenzi wangu japo bado nampenda huyu kijana sana tena sana.

Nawaza nimuache au nijikaushe tuu niwe nao wote?
 
Huyu kaka kila nikitaka kumuhakikishia nina mtu wangu hataki hata kunielewa tunaheshimiana nasipendi watu wanatuzunguka wajue maana naona kama hawataamini ila wanaume sio watu jamani sikutegemea kabisa mimk
 
Kwakua hakunaga moyo mmoja unaopenda watu wawili ,na ili ww ndo usichakazwe zaidi .....3 sentences

Achana na wakwanza

Endelea na wapili

Kwasababu hukumpenda wa kwanza .


UPDATES

nmepitia nyuzi za mtoa mada ,nmegundua mambo makubwa matatu.

mwanaume mwenye ID yakike...Au
ni mtunzi wa stori...... Au
ni Sukubasi (In Mshana JR's Uzi waleo)


ACHEN KUJIPINDA KUANDIKA MAANDIKO MAREFU YENYE KUTUKANA,KUSHAURI WALA NN..MNAPOTEZA MUDA WENU !!

uzi mwema !!
 
Huyu kaka kila nikitaka kumuhakikishia nina mtu wangu hataki hata kunielewa tunaheshimiana nasipendi watu wanatuzunguka wajue maana naona kama hawataamini ila wanaume sio watu jamani sikutegemea kabisa mimk
mkuu sasa sio watu kivipi? alikushikia bunduki kumkubali?
 
wakwa
Kwakua hakunaga moyo mmoja unaopenda watu wawili ,na ili ww ndo usichakazwe zaidi .....3 sentence

Achana na wakwanza

Endelea na wapili

Kwasababu hukumpenda wa kwanza .
wakwanza tuna fiucha huyu wapili sina fiucha nae hata kidogo nijifurahisha tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom