Kwanza kabisa eee Mungu nisamehe dhambi ya kumzalisha dada wa watu mwaka 2010. Pia ingawa aliolewa kwa yeye mwenyewe kukosa subira kutokana na mimi kuwa na safari ndefu ya kusoma, licha ya kumsihi sana.
Huku Cambodia nimebahatika kukutana na wa Njombe mwenzangu(Mtanzania I mean) ni wife material haswaa.
Bond ikakubali, chemistry ni ya hali ya Juu.Yani ndo aina ya mke nilikuwa namtafuta, yani pamoja na mimi kutakiwa kumpenda ila yeye pia anatakiwa awe zaidi ya mama kwani nayajua niliyopitia mie.
Masikini nimegundua ana mtoto tayari ingawa anajitahidi kuficha ili tufikie adhma yetu. Yani moyo wangu umeumia sana, ingawa nami nina mtoto.
ukweli wa Mungu nafsi yangu haipo tayari kuoa mtu aliye na mtoto tayari.
NIMEKATA TAMAA, SIELEWI NIFANYE NINI?
Na demand ya kuoa ipo sana sana kwani umri nao si rafiki.
Akili imevurugika kabisa. Ama kweli ng'ombe wa masikini hazai.