Hao masingle mama mnao wakataa wanashida gani?
Ina maana hao watoto wamekuwa laana kiasi hicho?
Ina maana mtoto ni kikwazo kwako kuoa?
Na upande wa pili wadada wengine wanakataa watoto wenye watoto lakin kwa wadada ni wachache sana wanao kataa.
Nashindwa elezea nisemeje hapa kwa ufupi Mungu haangalii hao watoto kama wengine wanavyo angalia
Hao watoto waliachwa kwa mama zao, ni watoto ambao Mungu anawasikia kuliko kawaida, dhambi ya mama mtu isikufanye ukamuacha mtoto ukaona labda ukipata asiye na mtoto mtakuwa vzr.
Hao watoto wanaletaga baraka mno ndani ya familia kama ukijua kumtunza vizuri bila manyanyaso, Mungu atakufungulia mlango kupitia huyo mtoto kuliko hata watoto wako binafsi wakati mwingine.
Nimeona watoto wa aina hiyo mama zao wanapo olewa na baba akampenda mtoto, au baba anapo oa na mama wa kambo akampenda mtoto, kuna baraka kama huamini tafuta family inayo tenga watoto wa kambo huwa hawabaki salama.
Mnapo weka akilini mimi sioi mtu mwenye mtoto au siolewi na mwanaume mwenye watoto, huwez jua baraka zako zipo wapi kila mtu.ana mlango wa kumtoa afike katk mahal ambapo Mungu alipo muandalia, inakuwaje kama ni huyo single mama kupitia mtoto.wake ndipo baraka zako zilipo
Msipende kujifungia ndani ya box. Mungu hana ubaguzi mnao ufanya baadhi ya watu.
All single mama na single dad. Mungu awape nguvu ya kulea watoto wenu na Mungu awape watu sahihi.ambao sio wabaguzi