SweetyCandy
JF-Expert Member
- Sep 17, 2022
- 5,221
- 9,904
Ameenda Kwao Kujifungua Namuambiaje Nimeoa Mwanamke Mwingine?
Mimi ni Kijana wa miaka 31, nimeoa, kabla ya kuoa nilikua kwenye mahusiano na Dada mmoja ambaye tulikua tunapendana sana, kila kitu tulikua tunafanya mapka kwao alishanitambulisha ingawa kwetua ilikua bado.
Mwaka jana mwishoni mimi nayeye tulikubaliana kua na mtoto kisha ndiyo tufunge ndoa ingawa tulikua bado hatujaanza kuishi pamoja, alikubali na kubeba ujauzito wangu. Sababu ya kuja kwako ni hivi, katika kipindi hiki cha miezi minne ambacho ameenda kwao kujifungua nimegundua kuwa nilifanya makosa kuzaa naye.
Sio kama nilimdanganya lakini niliona kama nimefanya makosa sikua tayari kuwa Baba. Nilijikuta napunguza mawasiliano, na kipindi hichochoicho nilijikuta naingia kwenye mahusaino na mwanamke mwingine. Ni binti ambaye nimemuona kwa muda mfupi lakini nilijikuta kuwa nampenda, kwakua nilikua nahofia asije kujua kuwa nina mtoto nilimuambia kuwa nataka kumuoa.
Alikubali, nilimtambulisha kwetu harakaharaka na kuwaambia ndugu zangu nafunga ndoa na kwakua sisi waisalamu ndoa haicheleweshwi nimefunga naye ndoa na sasa hivi tuna furaha.
Naomba unisaidie namna gani nitamuambia X wangu kuwa nimeoa, simhitaji nataka tulee mtoto tu. Lengo lilikua mimi nikienda kumchukua ndiyo nitoe Mahari na kufunga naye ndoa lakini simhitaji tena. Nina mke tayari na nampenda, siko tayari kwa mtoto kwasasa hivi, nataka kula matunda ya ndoa na wala siwezi kuoa wake wawili ingawa dini inaruhusu!.
Kila siku namzungusha X wangu kuwa nitaenda kumchukua, mtoto ana miezi mitatu sasa, anataka kurudi, kazi hana kwani baada ya ujauzito nilimuachisha kazi, tulikua na malengo mengi sana. Najua nimekosea lakini haikua mipango yangu, kila kitu kimebadilika, nisaidie hata kuongea naye ili ajisikie vizuria jue sikupanga kumuacha bali imetokea tu! Niko tayari hata kumpa mtaji aanze maisha yake na mtoto nitalea!