Leo hii ndo nimekata tamaa rasmi kuoa

Leo hii ndo nimekata tamaa rasmi kuoa

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
22,765
Reaction score
31,221
Kwanza kabisa eee Mungu nisamehe dhambi ya kumzalisha dada wa watu mwaka 2010. Pia ingawa aliolewa kwa yeye mwenyewe kukosa subira kutokana na mimi kuwa na safari ndefu ya kusoma, licha ya kumsihi sana.

Huku Cambodia nimebahatika kukutana na wa Njombe mwenzangu(Mtanzania I mean) ni wife material haswaa.

Bond ikakubali, chemistry ni ya hali ya Juu.Yani ndo aina ya mke nilikuwa namtafuta, yani pamoja na mimi kutakiwa kumpenda ila yeye pia anatakiwa awe zaidi ya mama kwani nayajua niliyopitia mie.

Masikini nimegundua ana mtoto tayari ingawa anajitahidi kuficha ili tufikie adhma yetu. Yani moyo wangu umeumia sana, ingawa nami nina mtoto.
ukweli wa Mungu nafsi yangu haipo tayari kuoa mtu aliye na mtoto tayari.

NIMEKATA TAMAA, SIELEWI NIFANYE NINI?

Na demand ya kuoa ipo sana sana kwani umri nao si rafiki.

Akili imevurugika kabisa. Ama kweli ng'ombe wa masikini hazai.
 
Kila kitu hutokea kwa sabab maalum(vingi huwa ni sabab nzur)
Huwez jua huyo mtoto wake ndo akaja kuwa msaada kwako
 
Kama umesema yuko vizuri na ni aina ya mwanamke uliekuwa unamhitaji sasa kuwa na mtoto ndo iwe shida jamani? Kama kakidhi vigezo kuwa na mtoto sio shida kabisa na single mother wengi wanajielewa! Unaweza pata huyo asiekuwa na mtoto ndo pasua kichwa sasa hapo sijui ndo maisha utayafurahia!?
 
Kinachokuzuia hasa ni nini? Mzazi mwenzake unamfahamu au rather her story ya yeye kuwa alivyo?
 
Mkuu ni kweli umri umekutupa mkono mmmmh mbona kama still una akili za kitoto.

Maana kama umri umekutupa mkono kama unavyo tupasha uwezi kataa kuoa kwa sababu tu wandani wako ana mtoto hiyo sio sababu fikirishi na yenye mantiki kwa kusema utaki mke kwa sababu ana mtoto

embu jitathimini bhana acha kuzingua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom