Leo hii ndo nimekata tamaa rasmi kuoa

Leo hii ndo nimekata tamaa rasmi kuoa

Kwanza kabisa eee Mungu nisamehe dhambi ya kumzalisha dada wa watu mwaka 2010.
Pia ingawa aliolewa Kwa yeye mwenyewe kukosa subira kutokana na mie kuwa na safari ndefu ya kusoma,licha ya kumsihi sn.

Huku Cambodia nimebahatika kukutana na wa Njombe mwenzangu(Mtanzania I mean) ni wife material haswaa.
Bond ikakubali,chemistry ni ya hali ya Juu.Yani ndo aina ya mke nilikuwa namtafuta,yani pamoja na mie kutakiwa kumpenda ila yeye pia anatakiwa awe zaidi ya mama kwani nayajua niliyopitia mie.

Masikini nimegundua ana mtoto tayari ingawa anajitahidi kuficha ili tufikie adhma yetu.Yani moyo wangu umeumia sn, ingawa nami nina mtoto.
Ukweli wa Mungu nafsi yng haipo tayari kuoa mtu aliye na mtoto tayari.

NIMEKATA TAMAA,SIELEWI NIFANYE NINI?
Na demand ya kuoa ipo sana sana kwani umri nao si rafiki.

Akili imevurugika kabisa.Ama kweli ng'ombe wa masikini hazai.
Wee wa ajabu mno. Kamwene!.
 
Sina nia mbaya na dada zangu hawa Mkuu na wala sijawakashfu hapana.

Ni nafsi tu vile inavyonituma.

Nawaheshimu sana.

Ila ktk hili moyo umevunjika vunjika kabisa.
Bora huyo umemkuta na mtoto kuliko kuliko kuoa binti ukijua hana mtoto Kumbe Alisha toa mimba sita. Ushauli wangu mwanamke mwenyewe mtoto kama sifa zingine Zote amado oa tu mkuu mtoto siyo sababu ya msingi kumuacha Mke kwanza ukimkuta na mtoto Ndiyo unakuwa na huakika kizazi anacho
 
Kwanza kabisa eee Mungu nisamehe dhambi ya kumzalisha dada wa watu mwaka 2010.
Pia ingawa aliolewa Kwa yeye mwenyewe kukosa subira kutokana na mie kuwa na safari ndefu ya kusoma,licha ya kumsihi sn.

Huku Cambodia nimebahatika kukutana na wa Njombe mwenzangu(Mtanzania I mean) ni wife material haswaa.
Bond ikakubali,chemistry ni ya hali ya Juu.Yani ndo aina ya mke nilikuwa namtafuta,yani pamoja na mie kutakiwa kumpenda ila yeye pia anatakiwa awe zaidi ya mama kwani nayajua niliyopitia mie.

Masikini nimegundua ana mtoto tayari ingawa anajitahidi kuficha ili tufikie adhma yetu.Yani moyo wangu umeumia sn, ingawa nami nina mtoto.
Ukweli wa Mungu nafsi yng haipo tayari kuoa mtu aliye na mtoto tayari.

NIMEKATA TAMAA,SIELEWI NIFANYE NINI?
Na demand ya kuoa ipo sana sana kwani umri nao si rafiki.

Akili imevurugika kabisa.Ama kweli ng'ombe wa masikini hazai.
Sasa wewe hutaki kuoa mwenye mtoto wakati huo ww unamtoto!
 
Ulitaka mrembo kama huyo unayekiri kuwa ni waifu matirio awe amekaa mwenyewe kwenye vichaka kama karunguyeye (kidungumalia)?

Kama kweli ni mzuri ulipaswa kujimilikisha kisheria.
 
Yaan Wewe unataka ambaye hajazaa huku Wewe ukiea used

Ebooo!! Shenzi type
 
Mkuu pengne hata wewe hujui au utakataa ila ukikaa ukitafakali tena hasa ukizingatia nawe una mtoto km yeye belive me chanzo kikubwa cha hilo ni ubinafsi.
 
Nyie ndio waharibufu ambao mwisho wa siku huishia kuharibiwa. Usitusahau mrejesho wa ndoa yako na binti kigoli.
 
Na wewe si ulimzalisha mtu akaolewa????

Tatizo nini sasa.???
 
DEVINE... wengu hawapendi complications zinazoletwa na aina hii ya uhusiano. Kama baba wa mtoto yuko hai bond yao haiwezi kuvunjika kamwe. Mama kwa namna moja au nyingine lazima amshirikishe baba kwenye malezi ya mtoto.
Inategemea makubaliano yenu, na kwanini isivunjike? Inavunjika vizuri tu, ukiplay part yako vizuri huyo mtu baki atabak baba wa mtoto lakin ndoa yako hawezi ingilia,

Humu kuna wengine wanasuport kwa kusimuliwa tu, maisha hayaendi kwa group, maisha yanaenda binafsi, kama ndoa isivyo ya group ni ya mmoja mmoja hivyo hivyo usifikirie kwakuwa fulan kapata hivi na mimi nitapata hivi hapana.

Lazima useme hapa haipo hiyo bond, kama huyo mtu alitaka kumuoa huyo dada angeoa mbona kamuacha, shida inakuja wakaka wakizalisha wakiona huyo mdada anaolewa huwa wanaumia walitegemea mdada abaki hivyo hivyo mnaanza kuleta vurugu ktk ndoa ya mdada hata kama mwanzo ulikuwa hujali mtoto utajifanya kujali mtoto,
Na kama ukimtunza huyo mtoto kama wako unafikiri mawasiliano ya nn yatakuwepo hapo, sababu kila kitu mtoto anapata hapo kwako.

Cha muhimu makubaliano kabla hujaingia katika hiyo ndoa.
Na mtoto muone ni baraka kwako
 
KUNA WANAWAKE NI WAJINGAAAA!
YANI MI NIWE NA MTOTO,NA WEWE UNA MTOTO HALAFU NIFICHE KUWA SINA MTOTO!
chaaaaaaaaaaaaa!?
hata usingekuwa nae,kitu cha kwanza nitakwambia kwenye introduction yetu siku tunaanza story ni
..........naitwa flora,nina mtoto wa kiume/kike ana miaka 5 ,nina umri wa miaka 30,ninauza mashuka na sidiria ,ninapenda kucheza mziki na kupika chapatti.''
mengine yaendelee baada ya hapo!
na utamsikia mwanangu katika ratiba zangu!
utamsikia mwanangu katika excuse zangu
utamsikia mwanangu katika furaha zangu!
THTS MY LIFE,UKITAKA KARIBU HUWEZI KATAFUTE MABIKIRA WA PLACENTA BABA!
langu used liwache!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom