Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!
Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?
Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??
Kwa nini tunazaa watoto?
Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??
Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???
Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?
Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??
NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?
Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!
Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?
JeTunaishi ili tufe???
Nini maana ya maisha???
View attachment 1575137
Mkuu Yoga
Umeuliza maswali muhimu mno na aina hii ya maswali haulizi mtu ila mwenye kutafakari.
Ukiupitia uzi mzima kuanzia mwanzo mpaka ulipo sasa Wakuu wamejitahidi kuchangia kila mmoja kwa anavyoona , nami naomba nichangie kwa uchache
Na Swali lako hili hakuna AKILI YA MTU , SAYANSI, inaweza kukupa jibu litakaweza kukukinahisha.
Sehemu pakee inaweza kukupa jawabu sahihi ni kurudi katika VITABU VYA DINI( religious scriptures) . Huko huenda ukakinahi
Mimi nitaleta kulingana na Imani yangu na Kama kuna wenzetu wanaweza kutuletea kutokana na imani zao tena kwa ushahidi basi nao wafanye ili tuone kama walau tutaweza kukidhi haja ya muulizaji.
Katika uislam imejibiwa hivi:-
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ﴿٥٦﴾
Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. Qur'an [51:56]
Anatujulisha MUUMBA kwamba Ametuumba Sisi kwa hikmah nayo ni kumpwekesha (oneness) katika ‘ibaada wala hakutuumba kwa kuwa Ana haja nasisi kwani yeye ni Mkwasi Asiyehitaji kitu kama Anavyosema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ﴿١٥﴾
Enyi watu! Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote. Qur'an [35:15]
Akathibitisha hayo MUUMBA Anapoendelea kusema baada ya Aayah iliyotangulia ya Sura ya 51
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ﴿٥٧﴾
Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe.Qur'an [51:57]
Akatujulisha kwamba Hahitaji lolote kutoka kwa waja Wake, bali waja ndio wanaomhitaji MUUMBA (Mwenye nguvu na utukufu) kwani Yeye Ndiye Anayewaruzuku na Anawaendeshea maisha yao na Ndiye Anayewapangia na kuwatengeneza mambo yao. Yeye ni Allaah, Anayestahiki kuabudiwa kwa haki Naye Ndiye Muumba wa kila kitu:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾
Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote. Qur'an[6: 102]
Na Anasema pia:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾
Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa ( mnadanganyika)? Qur'an [40: 62]
Viumbe hao, wanajumuika Malaika, majini na wana Aadam. Wote hao wanastahiki kumwambudu kwa kuwa ni haki ya MUUMBA (kuabudiwa) kutoka kwao na lau kama watamshirikisha, basi Atawaadhibu hata ikiwa Malaika watamshirikisha, kama Anavyosema:
وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾
Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: “Mimi ni mwabudiwa badala Yake,” basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu. Qur'an [21: 29]
Na atakayemshirikisha MUUMBA hatoweza kufidia kuepukana na adhabu ya Allaah (Mwenye nguvu na utukufu ) hata akiwa na dhahabu inayojaa ardhini! Anasema Allaah
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾
Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru. Qur'an[3:91]
Kwahiyo ukitizama reference zote zinaelezea lengo Mama la uumbwaji ni KUMUABUDU MOLA MLEZI. Na si kingine
Na ukajaribu kutafakari ni kuwa hapa Duniani ni kama tupo katika chumba cha mtihani humu humu kuna watakaofeli na watakaofaulu
Omba usiwe katika kundi la waliofeli.