Lema: "Serikali inaonewa"

Lema: "Serikali inaonewa"

It's ver true, serikali iliyoshindwa hata kununua vidonge vya panadol kwa baadhi ya zahanati zake vijijini, leo hii unaipachika jukumu zito la kununua madege ya Boeing 767, ni serikali ya aina hiyo ya ubabaishaji itaweweseka tu!!

Ni jambo ambalo ni next to impossible, kuona nchi kubwa kama TZ, iliyosheheni utajiri wa kila aina wa rasilimali tulizojaaliwa na Mungu, kama vile madini ya uranium, dhahabu, tanzanite, almasi na madini mengine mengi yenye thsmani, na pamoja nchi yetu kujaaliwa kuwa na gesi nyingi sana pamoja na mafuta, lakini ni jambo linaloshangaza kupita kiasi kuona nchi yetu shirika letu la Taifa la ndege la ATCL likiwa halina hata ndege hata moja, nchi jirani kama Rwanda, ambbako ni kanchi kadogo sana kenye eneo dogo sana linalofanana na mkoa wetu mmoja tu wa Singida, na kanchi ambacho hakina rasilimali zozote kilichojaaliwa na Mungu, kanchi hako kanatushinda kwa kwa kuwa na ndege zaidi ya nne wakati sisi tuna ndege ZERO!!!!

mkuu Rwandaair walikuwa na ndege 12 mwaka 2012 sijui kwa sasa hivi. shida yetu ni uongozi mbovu tuu.
 
Lema ni Jembe presida wa Arusha, mtabakia hayohayo ndio maana hamuwezi kuona mmekimbilia kuweka Meya wakichina R Chuga
 
Kawapiga vijembe kuwa serikali ineshindwa kazi hata dawati imeshindwa watoto wenu wanakaa chini. Je ndege itaweza au kwa kuwa ni ulaji. Hongera Lema fasihi uliisoma na kufaulu.
 
Huyu Mtu sijui ana akili ya wapi! Kama alijua kuwa Shule hazina madawati, Hospitali hazina vitanda etc Mbona anapokea Posho ambazo angeweza kuamrisha zielekezwe kwenye shuguli nyingine za maendeleo? Mbona alipokea Milioni tisini ya shangingi? etc Godbless J Lema , na wabunge walalamikaji aina yake ni wanafiki na wanapoteza sifa za kuongoza wananchi kila uchao.

Kauli ya Lema inahitaji kutafsiriwa kwa umakini sio juu juu tu, kwa kifupi ina maana kuwa kama wewe ni Baba wa familia, kwa sababu ya kutosimia vizuri mapato na matumizi ya familia, umeshindwa kusomesha mtoto katika shule ya awali, utaweza kumsomesha Chuo Kikuu ? Posho ya Lema na hao wabunge wengine hata wakizitoa kwa muda wa miaka 1000 hazitaweza kitu, inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwenu nyie Chama tawala kutoa miongozo inayotekelezeka na kuisimamia kwa vitendo.
 
Kwahiyo na LEMA ni mmoja wa wasomi nchi hii?
Tatizo wewe huwa unachangia bila kuwa na hoja. Kama ulimsikiliza Lema alisema Mh Raus anateua watu kwa kuangalia vyeti badala ya yfanusu na uwajibikaji. Hiyo ya usomi ni mawazo yaki. Avatar ---- inaonyesha upeo wako wa mawazo.
 
Lema anaweza kuwa na kauli nyingi alizotoa lakini hili la Kuonewa kwa Serikali inayoshindwa kununua madawati ila inapanga mipango ya kununua ndege inahitaji tafakari ya kutosha.

Achana na ushabiki, achana na chama...........Lema kuna vitu vya msingi anataka Serikali ione na kutafakari..

1. Mambo ya muhimu na lazima kwanza vs mambo ya kujionyesha kuwa mmeendelea.

Hivi ni kweli tunahitaji kutumia pesa nyingi kununua ndege badala ya kuwekeza kwenye mambo ya lazima na muhimi katika ustawi wa jamii ya Watanzania.

Nimetembea baadhi ya maeneo ya vijijini nilipokuwa ninafanya tafiti mbalimbali za maendeleo. Baadhi ya maeneo maisha bado yapo duni mno, hakuna maji safi, hakuna huduma ya afya watu wanaishi tu katika hali mbaya kabisa.

Hivi ni nani atakayetusifia na kutuona tumeendelea kwa kuwa tu tuna shirika la ndege kubwa.

Watanzania tuhjifunze kuwa na vipaumbele vitakavyotukomboa na sio kushabikia sifa zisizo na maana.

Ni shirika hili hili liloingizia Serikali hasara halafu leo watu na akili zao hawaoni kwamba huku ni kukosa mipango na hadithi zile zile za kunufaisha wachache.

Kwa hili nakuunga mkono Lema.
 
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema Jana aliitetea Serikali ya ccm kuwa siyo sahihi kuitaka inunue ndege mpya.

Alisema Serikali ambayo watoto wa shule wanakaa chini mpaka sasa miaka hamsini baada ya uhuru itawezeje kufufua kampuni ya Ndege?

Akaendelea, serikali ambayo mpaka leo miaka 50 baada ya uhuru haijaweza kununua vitanda vya wagonjwa na mpaka sasa wamama wanajifungulia sakafuni itawezaje kufufua kampuni ya ndege?

Kwa maoni yake, kudai kampuni ya ndege ya Tanzania pamoja na kuwa ni muhimu na ni heshimu kubwa sana kuwa na kampuni ya ndege ya nchi, lakini jambo kubwa kama hilo kuidai itekelezwe na serikali ya ccm kwa sasa ni kuionea serikali tu.

Akamalizia, wanaotaka Kampuni ya ndege wafanye sala, maombi na dua ili serikali hiyo iondoke madarakani na ije serikali itakayofanya mambo makubwa kama hayo.

Ni hayo tu kwa asubuhi ya leo, na siyo maoni yangu, bali maoni ya Mheshimiwa Godbless J Lema, Mbunge wa Arusha mjini.

Nawasilisha.
 
Lema hana uwezo wa kujenga hoja ikajengeka, labda vioja: Kumbuka hivi majuzi, Kenya Airways, imenunua Ndege mbili aina ya B777-300ER zenye uwezo wa kubeba abiria 400 kila moja. Lema anataka kusema nchi jirani ya kenya hakuna changamoto za HOSPITALI wala ELIMU? Je Kenya hakuna changamoto zozote za Kimaisha? Ifike mahali LEMA ache ujinga, wakati anaongea bungeni awaze kabla, asije akadhani kuongea bungeni ni kama anaongea na wahuni wenzie.

Hata kama zipo ni kwa kiasi gani ukiringanisha na nchi yetu?
 
LEMA amekuwa ni mmoja wa wabunge vikwazo katika kampeni ya "SAY NO TO POSHO".
Mara kadhaa tumeshasoma comments za LEMA hapa jamvini alivyokuwa akimshambulia mbunge mwenzie ambaye amekataa kuchukua posho.
Huyo Mbunge mwingine aliyekataa posho - posho zake zimeshanunua madawati? mshauri arudishe zile USD250000 kila mwezi alizokuwa akitumiwa Germany.
 
Kwahiyo na LEMA ni mmoja wa wasomi nchi hii?

Hapana mkuu, nakubaliana na wewe kabisa kuwa Lema si msomi ila ni inteligent. Nchi hii ingekuwa na watu inteligent kama Mh LEMA watoto wetu wasingekosa madawati, wake zetu wasingezalia chini kwa uhaba wa vitanda. Kwa maana kama usomi wenyewe ndo huu wa akina Muhongo, unaotutaka tufikiri kuuza juice tu, huoni kuwaambia wanunue ndege ni kuwaonea. utauza juice lita ngapi ili upate ndege? Dawa ni kuwaondoa wasomi wetu wanaowaza uwekezaji wa Juice na tuwaweke watu inteligent kama Mh LEMA watusaidie.
 
yaani nimfume akimshika mai-dia wangu namna hii - aisee tunatoana utumbo na chama baasi!!

attachment.php
 
kila siku nasemaga lema ni jembe na hoja zake ni nzito sana kwa watu wenye busara kama sisi kina gogo la shamba lema hapo ameonyesha ni jinsi gani serikali hii ya ccm isivyowajali wananchi wao.nakupongeza sana lema kwa kuwa mkweli na mtu asieyekuwa woga kusema ukweli
 
Lema ni binadamu kama wengine, ila ni extra ordinary katika kuthubutu!
 
Back
Top Bottom