Napoteza matumaini ninaposikia watu kama Lema wakisema mshahara wa $ 4000 ni mdogo.Matumaini yangu mimi nimekuwa nayaweka kwa CHADEMA kuwa ndiyo wenye lengo la kuikomboa nchi hii kutoka kwenye lindi la umaskini. Kwa bahati mbaya maneno kama hayo nimewahi kuyasikia yakisemwa na Tundu Lissu pia. Swali langu ni kwa nini basi alitaka kufanya kazi ya ubunge huku akijua kuwa mshahara wake ni kidogo. Swali lingine ni udogo huo wa mshahara ni kwa standard gani? Analinganisha na mshahara wa akina nani hapa Tz. Madaktari wanapata kiasi gani. Walimu je wanapata kiasi gani? Asije akataka kulipwa kama mbunge wa Canada huko aliko. Napata wasiwasi kuwa Lema anachogombea sasa si ukombozi wa watz bali wa tumbo lake. Kinachomsukuma sasa ni wivu dhidi ya walio madarakani.Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini bwana Godbless Lema, katika Mazungumzo huko space twitter alisikika akikwambia Kitila Mkumbo kwamba mshahara wa mbunge ni Mdogo mno yaani ni 4000$ Kwa Mwezi hivyo aache Ubunge amfundishe cryptocurrency apate zaidi ya hiyo maana anazidiwa na vijana wanaoifanya.
Kumbe LEMA anasema mshahara wa mbunge Mdogo ama uongezwe
Britanicca