Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 2,774
- 6,885
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa amesema kwa kazi kubwa ambayo Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiifanya tangu ashike hatamu ya Urais, anastahili kupewa Uprofesa.
Lela ameongea hayo mbele ya Rais Samia leo December 28,2023 wakati wa Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho ambacho Mkuu wake ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, kimemtunuku Rais Samia Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Utalii na Usimamizi wa Masoko kwa kutambua mchango wake wa kuifungua Nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii.
Lela amenukuliwa akisema “Nataka niungane na wote ambao wametoa wasifu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa anastahili kupewa tuzo na sio tu katika ngazi ya PhD lakini kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya tangu ashike hatamu anastahili Uprofesa”
“Uthubutu mkubwa ambao amekuwa akionesha katika uongozi wake, ukomavu wa kisiasa na uvumilivu wa hali ya juu ni zaidi ya PhD na niliuliza wakati linakuja wazo la kuwa anataka kupewa PhD nikauliza kwani haiwezekani kumpa Uprofesa moja kwa moja tukamaliza kazi, nikaambiwa kuna taratibu zake lakini Mheshimiwa (Rais Samia) tutazishughulikia”
“Kwa Mh. Rais Samia hii ni PhD ya tatu ametunukiwa tangu awe Rais wa Tanzania, ya kwanza alikabidhiwa UDSM na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na leo hapa anakabidhiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi lakini ya pili alikabidhiwa nchini India na alipopewa akasema anawazawadia Mabinti wa Tanzania”