Lebanon wameweza. Tanzania na Africa tunafeli wapi?

Lebanon wameweza. Tanzania na Africa tunafeli wapi?

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,080
Reaction score
3,771
Habarini waungwana

Okay iko hivi wiki hii story kubwa ni kuhusu kampuni ya Anghami kuweza kuingia kwenye soko la Hisa la Marekani la NASDAQ na kuwa kampuni pekee ya Lebanon kufanikisha kuingia kwenye soko la Hisa la NASDAQ

sasa basi tuangalie Anghami ni nini?

Anghami ni kampuni ambayo inatengeneza mfumo wa Ku stream miziki kama ambavyo Apple, Deezer na spotify

Anghami wao wamejikita kuweka miziki katika soko la Uarabuni kwa maana MENA Region (Middle East and North America )

Anghami ilijikita zaidi katika kuweka miziki ya wasanii wa MENA Region ambapo iliweza kuwa na watumiaji takribani 50M katika ukanda wote wa MENA sanjari na hilo iliweza kutumiwa na waarabu wengi waliopo maeneo mbalimbali Duniani

Hii ilipelekea kuwavutia wawekezaji ambapo tangu uanzishwaji wake mwaka 2012 imeweza kupata uwekezaji wa $14M ambazo ni zaidi ya Tsh 30B

Hii ilipelekea mapato ya kampuni hiyo kuongezeka kwani ilikadiriwa kuwa na watu takribani ya 5M kuweza kulipia kila mwezi

Mpaka kufikia mwaka huu mpaka kuingia kwenye soko la hisa la NASDAQ Anghami ilikuwa na thamani ya $220M sawa na zaidi ya Tsh 500B

TANZANIA NA AFRICA TUNAKWAMA WAPI?
Anghami wameweza wakitokea Lebanon sehemu ambayo imekuwa so much complecated katika uanzishwaji wa Startup, sababu Startup Ecosystem yake imekaa complecated as well

Ila wameweza kupenetrate soko

Sasa tuje hapa kwetu Tanzania na Africa kwa ujumla

Tumeshindwa nini kuanzisha kampuni ambayo itakuwa ni music streaming kwa Nyimbo za wasanii wa Africa?

Mfumo ambao utakuwa una wasanii katika nchi zote za Sub Sahara

Ambazo tuna our own kind of Genre

Tunashukuru Mungu Africa sasa hivi tunaweza ku access developer wazuri kupitia Andela ambao wanaweza tengeneza Mfumo mzuri wa kiteknolojia ambao Music streaming ikawezeshwa

Africa tuna Boomplay, Mdundo, Mkito etc lakini bado hazijaweza kukidhi mahitaji na kupenetrate soko

Tukianza na Boomplay ambao mpaka sasa hivi wameweza kupata uwekezaji mkubwa wa takribani $51M sawa na zaidi ya Tsh 100B bado sio favourite kwa Africans wengi

Ukizingatia kwamba Imeweza kuenea zaidi sababu ya kuwa pre-downloaded kwa simu za Tecno na Infinix ambazo zimeuzwa sana Africa

Lakini pia UX/UI ya Boomplay sio nzuri ukilinganisha UX/UI za Apple, Deezer na Pandora

Bado kwa Africa tuna ombwe kubwa ambayo inahitaji kuja kutengenezwa Mfumo ambao kwa namna moja au nyingine utasaidia ku penetrate soko

Ambapo Soko ni kwa Sub Saharan, ukiangalia tuna advantage kubwa sana ya kutengeneza our own version ya Apple, Deezer, Spotify na zingine

Naendelea na Reseach yangu ya kuanzisha Music Platfom for Africa Market inayoitwa DUNDA


Thread ya Dunda imeshawekwa humu na imezungumziwa

Idea ya Dunda ni Music and Podcast Streaming ambapo itabase kwa Africa Music kuweza kusikika worldwide

ADVANTAGE TULIYONAYO DUNDA

Kiteknolojia

Tayari tuna Andela ambapo Africa tunaweza access Developers wazuri wakaleta matokeo chanya kwa kutengeneza App kama za Apple, Spotify na Deezer

Content

Lakini pia tuna wasanii ambao wapo tayari kwa ajili ya kuweka miziki yao kwenye platforms mbalimbali ikiwemo ambayo itaanzishwa ya Africa


Fee

Kwa kuwa wasanii wengi wa Africa hawako kwenye Label kubwa zile major label ambazo ni Sony, Universal na Warner Brothers ambao huchaji hela nyingi kwa integration za miziki ya wasanii wao

Yaani ili kwenye platfom wako iwe na wasanii kama kina Nicky Minaj, Coldplay, Chris Brown itahitaji ulipe hela nyingi kwa Major label zinazowasimamia, na hii iliwakuta Deezer kipindi wanaanza

Ila ili katika platfom yako uwe na wasanii kama kina Dula Makabila, Joeboy, Tiwa Savage, Aka, Nuhu Msiwanda haitahitaji uweke hela nyingi kwenye fee na mambo mengine kama hayo

NIMEFANYA NINI MPAKA SASA?


1.Niko kwenye mazungumzo na Andela kwa ajili ya ku develop the platfom ili kuona what they can bring in reality based on my idea and imagination

2. Naendelea na branding idea na formation of exact color patern ya Logo, Icons etc

3. Naendelea kuifanyia utafiti soko kwa uangalifu huku nikiwa niko aware na Competition iliyopo Africa kutoka kwa Boomplay, Apple Music, Deezer, na Spotify kwa baadhi ya regions

4. Naendelea na kufanya utafiti mbalimbali kuhusu Music Streaming platforms mbalimbali na kuweza ku integrate na kutenegeza DUNDA iwe one of the kind kwa African Market



CHANGAMOTO

1. Kwakuwa tutabase kwa wasanii wa Africa tu tunategemea tutakuwa na idadi ndogo ya Miziki ukilinganisha na platforms zingine

Tunategemea kuwa na Miziki chini ya 10M kwenye platfom yetu ya DUNDA na podcast chini ya 1M

2. Tunaingia kwenye biashara na washindani ambao ni wana uwekezaji mkubwa kama vile Apple, Spotify, na apps zingine, ikumbukwe kwamba mpaka sasa DUNDA ina uwekezaji $0

3. Tunapitia changamoto ya uwekezaji kwani kabla ya kuingia kwenye biashara kupata early customer feedback ni lazima kwanza tuwe na mfumo kwa ajili ya watu kuweza kuitumia kwa wasanii na wasikilizaji

Tunahitaji Pre-Seed ya $900K ambazo hizi zitatumika katika budget ifuatayo

1.Ku outsource developers kutoka Andela ambao watatengeneza mfumo

2.Pilot itakuwa ni Tanzania ambapo wasanii wa Tanzania, Bongo Fleva, Singeli, Gospel wataweka nyimbo zao kwa ajili ya watanzania ku stream

DUNDA Main marketing Strategy itakuwa ni kupitia pages za wasanii wenyewe

How??

DUNDA itakuwa na kitengo cha graphics na artwork ambacho kila nyimbo ya msanii itakayotoka itakuwa designed na kitengo chetu cha artwork ambacho kitakuwa na uniformity reflecting our brand

So kila artwork itapostiwa na msanii kwenye page zake za social media ikiwa accompanied na link ya playstore au apple store

Eventually DUNDA kwa Tanzania Market itakuwa popular na kupanga mpango wa ku rise $5M as pre seed ili kuweza ku penetrate masoko ya

Nigeria
South Africa
Kenya
Uganda
Ghana


Ikiwemo ufunguaji wa ofisi nchi hizo

NawasilishaView attachment 1718415
images%20(1).jpg
images%20(2).jpg
 
Idea yako imesimama bro nalutakia utekelezaji mwema
Amina ila changamoto ni kubwa mno Hii idea nimekuwa nayo ni almost a Year sasa kwenye execution ndio huwa ni shida
 
Amina ila changamoto ni kubwa mno Hii idea nimekuwa nayo ni almost a Year sasa kwenye execution ndio huwa ni shida
Nakufuatilia mkuu tangu ulivyoileta hapa mara ya kwanza mwaka jana,
Changomoto za execution zinatokea upande wa investors au developers ?
 
Mkuu una madini sana kila nikisoma uzi wako sitoki mtupu natamani nije kuonana na wewe siku moja Mungu akufanikishe aise.
Tuko pamoja sana .. tunajitahidi sana kuweza kuleta huu mfumo kwenye reality ila tu Bado tunapambana
 
Dunda next Godzilla

Vipi pale Silicon Dar
 
Idea yako ni safi sana mkuu. Shida wanayopata hata akina Boomplay na Mikito ni kwamba wa Africa wengi tunapenda vya bure. Hatupo radhi kulipia vitu kama mziki, hatuheshimu kazi za wasanii na hata actors.

Juzi juzi hapa mtu alileta uzi kusema kuwa Spotify wamekuja bongo na wanaplan ya hadi 6,900 lakini mtu anakwambia DJmwanga yupo siwezi lipia. Hii nadhani ni challenge kubwa sana ya hapa Africa ambayo inaua innovation nyingi sana.

Kwese iFlix nao walipata shida kwasababu hii. Unakuta umepata investors wa kuwezesha kazi yako isimame lakini hakuna profit ya maana sababu waAfrica hawapo radhi kulipia.

MuAfrica atakubali kulipia kitu kma kina trend or kinamfanya aonekana kma mtu wa western. Kma watu wanavyokubali kulipia Netflix or Apple music sababu ya status.

Nakumbuka nilisoma blog post moja inayoelezea kiundani sababu ya startups kufail in East Africa (nikipata link nitaipost hapa) na inaelezea vizuri kuhus hii issue ya wa Africa kuwa cheap.

Je wewe umejipangaje kupambana na hii issue? Maana ndio kikwazo kikubwa kuliko vyote.

Mm napenda kuona tukifika mbali kwenye mambo ya tech na kuleta changes hapa Africa.
 
Nakufuatilia mkuu tangu ulivyoileta hapa mara ya kwanza mwaka jana,
Changomoto za execution zinatokea upande wa investors au developers ?
Both kwa Investors na Developers

Tukianza na investors they dont put their money mpaka iwe kwa kitu ambacho ni ready made...

They dont invest in ideas so we need Developers kwa ajili ya ku develop the platform on otherside Developers ni ngumu kupata ambaye mtadevelop pamoja mu own the platform anahitaji umlipe


So naona ni bora nitafute hela niwalipe Andela wanitengenezee au ni assemble team tu develop
 
Usisahau GDP Per Capita ya Lebanon ni mara saba ya ile ya Tanzania. Hata US walipokuwa na GDP per capita inayofanana na yetu walikuwa wagumu sana kulipia miziki.

Disposable income ndogo sana bongo. Idadi ya walio kwenye middle class ikiendelea kuongezeka then mambo kama haya yatakaa sawa tu.

GDP PER CAPITA 2019

TANZANIA: 1,122 USD KWA MWAKA
LEBANON : 7,584 USD KWA MWAKA

Lebanon ina GDP per capita kubwa kuliko SA. Ya SA ni 6,000 USD kwa mwaka as of 2019.
 
Tuko pamoja sana .. tunajitahidi sana kuweza kuleta huu mfumo kwenye reality ila tu Bado tunapambana
Operations ndio huwa issue. Nina hakika with time unaweza tengeneza hiyo platform though sina hakika na option ya kutumia Andela kama itakuwa effective kuliko ya kutafuta competent developers mwenyewe.

But kaza kwenye operations research. Costs za kuleta wateja vs costs za retention vs customer lifetime value.

Idea wengi tu wanayo ila execution ndio hapo kunatofautisha kati ya failure na success. Pia sio vizuri kujilinganisha na hawa wenzetu ambao ukifuatilia kuna watu wame inject fedha zao nyingi sana na wametumia influence yao kufika walipo.

Ni good inspiration but bad comparator
 
UX/UI ya Boomplay haiko poa?
Probably wewe sio mtumiaji wa Boomplay.
IMG_0584.jpg
 
Naogopa kusema sana, lakini mkuu unapoteza tu muda..

Waafrica bado tuko Ulimwengu wa nyuma sana kwa hayo unayoyawaza, hata Elon na ideas zake angesema aanze kuziimplement huku Africa angefeli mapema mno..

Kuna jamaa amekushauri hapo, hao Boomsplay na sijui Muziki wanakofeli sio content ila sokoni ndio kuna changamoto. Hata FB, Twitter na mitandao mingine ya kijamii haikuwa kama ilivyo sasa miaka mitano tu nyuma. Innovations zinafanyika kama biashara inaingiza faida, sasa hizi zetu sijui Muziki tangia zianzishwe ziko hivohivo sababu hakuna kinachoingia cha maana kuweza kuupgrade contents na huduma zao..

Yote kwa yote kila la kheri, Idea nzuri, ila upokewaji mtaani utakuwa sifuri ukizingatia tu startup unayoitaka ni zaidi ya billion na nusu tayari
 
You are very right sir.. na hii ni changamoto kubwa

Nilifanya reseach ndogo kuona kwanini watu wengi hawawezi kulipia online, ambapo factors ziko nyingi ila moja wapo ni kutokuwa na elimu ya online subscription

Watu bado wana hofu ya nanma ambavyo wanaweza integrate kadi zao za benki na online platforms

Lakini pia wanahisi hela zao zitachukuliwa kwenye account

Ukiona watu wanalipia Netflix au Apple ni wanaamini kuwa these companies hawawezi waibia kuliko Mr Ojo from Nigeria aanzishe startup yake then aseme kuwa ana charge per subscription ni ngumu sana kutusua unless afanye B2B model of business

Sasa basi kwa sisi DUNDA kwanza tutakuwa tuna kazi ya moja ya ku integrate nyimbo nyingi kwenye platform yetu lakini pia itakuwa ni ruksa kuwa na account ya bure


Sasa hapa ndipo the tricky part kwamba tukiwa na watu let's say 10M+ kwenye platfom yetu tayari ni utajiri

Tutakachokifanya ni tutakaribisha makampuni katika nchi mbalimbali ku place matangazo

Hapa tutaajiri wataalamu wa B2B business development kwa ajili ya ku snatch ad deals na makampuni mbalimbali ambapo hii inaweza wakera baadhi ya users so ili kusiwe na matangazo he or she has to pay

Lakini pia Kuna Diaspora wengi maeneo mbalimbali duniani ambao tayari wana western mindset ambao kwa namna moja au nyingine ni rahisi kwa wao kulipia ili asikilize nyimbo za wizkid kuliko Mwanakhamis aliyepo Mbagala charambe alipie kwa ajili ya kumsikiliza Dulla makabila obviously huyu atakuwa kwenye free plan

Premium plan itakuwa na features ambazo free plan haina ambazo ni kama

1. Create a playlist
2. Skip a song
3. Offline play etc
 
Usisahau GDP Per Capita ya Lebanon ni mara saba ya ile ya Tanzania. Hata US walipokuwa na GDP per capita inayofanana na yetu walikuwa wagumu sana kulipia miziki.

Disposable income ndogo sana bongo. Idadi ya walio kwenye middle class ikiendelea kuongezeka then mambo kama haya yatakaa sawa tu.

GDP PER CAPITA 2019

TANZANIA: 1,122 USD KWA MWAKA
LEBANON : 7,584 USD KWA MWAKA

Lebanon ina GDP per capita kubwa kuliko SA. Ya SA ni 6,000 US kwa mwaka as of 2019.
Jamaa anafanya mchezo sana, mbongo alipie kununua mziki?? Hell no, hiyo Netflix yenyewe unakuta analipia mmoja then wanashare watu kama kumi hiyo account tena hapo ni mwezi mzima.

Ndio mtu alipie mziki mmoja sijui wa Zuchu!!
 
Usisahau GDP Per Capita ya Lebanon ni mara saba ya ile ya Tanzania. Hata US walipokuwa na GDP per capita inayofanana na yetu walikuwa wagumu sana kulipia miziki.

Disposable income ndogo sana bongo. Idadi ya walio kwenye middle class ikiendelea kuongezeka then mambo kama haya yatakaa sawa tu.

GDP PER CAPITA 2019

TANZANIA: 1,122 USD KWA MWAKA
LEBANON : 7,584 USD KWA MWAKA

Lebanon ina GDP per capita kubwa kuliko SA. Ya SA ni 6,000 US kwa mwaka as of 2019.
Uko sahihi lakini mkuu DUNDA haiwalengi watanzania pekee

DUNDA inawalenga Mtu yeyote aliyepo Duniani anayeitwa Muafrica

DUNDA inamlenga mtu yeyote aliyepo Duniani anayependa African Music
 
Back
Top Bottom