Leaving on a Jet Plane by John Denver: Hakika Hustle Life is a lonely life!

thatHUMBLEguy

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
223
522
So kiss me and smile for me
Tell me that you'll wait for me
Hold me like you'll never let me go
'Cause I'm leavin' on a jet plane
Don't know when I'll be back again
Oh babe, I hate to go

Nimeusikia wimbo huu wa John Denver uliotoka miaka ya 1960/70—sikua nimezaliwa— maneno yake yakanigusa na kunipa kumbukumbu za mwanamke. Jesca. Mwanamke niliyempenda sana, lakini tulidumu kwa muda usiozidi siku 60 katika mapenzi, kwa makosa ambayo hayakuwa yangu wala yake. Bali uhalisia wa Maisha.

Katika harakati za utafutaji, Mwaka 2014 nilipata deal la ushiriki kampeni za uchaguzi wa serikali za Mitaa katika Wilaya ya Kwimba kama Msafirishaji kwenye Chama kimoja. Gari ilikuwa inatumiwa na Mkubwa mmoja wa Chama Mkoa na timu yake. Kwa kweli kazi ile ilikuwa ni ya kijeshi haswa, STANDBY AND READY TO GO. Kipindi naanza hii kazi nilikuwa nina siku kadhaa nimeanza mahusiano na Mwanamke mmoja anaitwa Jesca. Jesca alikuwa ni mwanamke mweupe, urefu takribani futi 5.5 na umbile lililopangilika vyema. Jesca alikuwa mwanamke mpole sana na mvumilivu na muelewa sana. Mpole. Kwa anayewajua wanawake wa kisukuma waliokulia kwenye ukatoliki, nadhani atanielewa. Jesca nilikuwa nampenda sana, mbaya zaidi, chumbani ndipo alipokuwa akinimaliza. She really got me!

Mambo yote yalikuwa yakienda sawa tatizo likawa moja tu, muda wa kuwa pamoja. Sasa nilipoanza kazi, base yetu ilikuwa ni Ngudu, kuna lodge inaitwa Safari pale ndio yalikuwa makao. Tunazunguka vijijini, halafu tunarudi pale kulala. Mara kwa mara alikuwa akinitaka weekend aje, then jumapili arudi kazini. Wasiwasi wangu ilikuwa kukosa utulivu wa kuwa naye. Basi, nyakati fulani akaja. Kafika mida ya jioni mimi sikuwepo, niko vijijini, sababu logistics zote zilikuwa sawa hakupata shida. Nimefika saa 7 usiku tukalala. Saa 11 safari zikaanza. Nilikata siku mbili tunalala vijijini. Malalamiko yakaanza. Siku ya tatu, nikarudi mida ya saa 10 jioni. Nilioga, baada ya kuwa kula, tukaanza kustarehesha miili. Kuna mambo yanaweza watokea watu, wakagombana lakini wakashindwa elezea wa nje chanzo cha ugomvi wao. Nikiwa katikati, simu yangu ikaita. Huwa naiweka pembeni ya mto na tulikuwa 'Missionary.' Nikaichungulia, 'Boss'.

Niliipokea, Loudspeaker, bila hata salamu, 'Dakika 5, nitakuwa nje, uwe tayari, tunatakiwa twende Mwanza, kuna dharura'.

Nilishuka, bafuni kwa haraka, na kuwahi kwenye gari. Kwa kweli niliumia mno, sio sababu yangu bali sababu ya Jesca. Masaa mawili baada ya kufika Mwanza, ndipo nikapata wasaa wa kuongea naye na kumplease. Kesho yake, nikiwa njiani nikamwambia ninarudi na tutakuwa wote hatuna ratiba yoyote ya kikazi.

Nikiwa nimefika, niko chumbani, navua nguo nioge, mlango ukagongwa, kwenda kumsikiliza anaye gonga, ni Boss:

'Umeshakula?'
'Bado?'
'Sasa nimepigiwa simu, kuna ugeni unakuja Malya, tunapaswa sasa hivi tuondoke, tutakula tukifika, niko kwenye gari ninakusibiri
'😇

Sikua na namna. Nilimuaga Jesca. Nikachukua Backpack na kutoka. Nilikaa Malya siku tatu. Jesca, alichoka akaondoka. Hata mvumilivu, ana ukomo wake. Usiku nilipokea ujumbe wake kuniambia kuwa ni bora tuachane mapema, kama maisha yangu ndio hayo, hatoweza. Miezi kadhaa baadae, aliolewa na Mwalimu mmoja pale Shinyanga.

Nilionana naye Mwaka juzi, Dar, ndiko anakoishi sasa, ni heshima tu, lakini nilitamani sana, kuomba 'kukumbushia'. Aliniambia:
'Kipindi hicho nilikuwa na Mwanume wangu wa muda mrefu, lakini sikua na plan naye ndefu sababu sikua namuelewa, nilipokupata wewe nikaamini muda wa kumuacha umefika. Ila wewe ndio ulikuwa hueleweki kabisa, bora yeye, ndio maana nikaamua kuoelewa naye'. 😁

Maisha ya utafutaji, yamejaa upweke sana!

View: https://youtu.be/bRe648clNjg?si=49Y3wEnoi5lmi8-t
 
So kiss me and smile for me
Tell me that you'll wait for me
Hold me like you'll never let me go
'Cause I'm leavin' on a jet plane
Don't know when I'll be back again
Oh babe, I hate to go

View attachment 2884027

Daaah nimeguswa pia Mkuu, story inarelate na uhalisia wa wengi si wewe tu. Pole
 
Back
Top Bottom