Niliyoyaona baada ya kuweka wazi khali yangu ya maambukizi ya UKIMWI

Witch hunter

JF-Expert Member
Nov 21, 2018
1,917
5,014
Kwanza, nyuzi kama hizi ni muhimu sana katika jamii ili kuelimisha na kukumbushana juu ya hali halisi za Maisha, UKIMWI UPO NA UNAUA. Huu ni ukweli ambao kila mtu anapaswa kuujua ya kwamba, UKIMWI USIPOKUUA WEWE, HAKIKA UTAUA NDOTO ZAKO, ndoto za wanao, ndoto za Wazazi wako na taifa kwa ujumla. Mi ni muhanga wa hili na nalijua vyema…. Mtu yeyote aliyesoma ule uzima atakuwa ameyaona haya au Zaidi ya haya

Takribani kila mchangiaji anamfahamu mtu mmoja au Zaidi aliyeaga dunia kwa gonjwa la UKIMWI.

Takribani kila mchangiaji anamfahamu mgonjwa mmoja au zaidi wa UKIMWI aliyeko hai katika familia ukoo au mtaani kwake.

Licha ya kujua hatari ya gojwa hili badoo watu wengi hawachukui hatua stahiki za kujikinga

Watu wengi pia huishi na ugonwa huu bila kujua (PIMA, TAMBUA AFYA YAKO, TIMIZA NDOTO ZAKO)

Wanawake wengi wamemuachia mwanaume ndiye aamue kama atatumia CONDOM au laa. Hii ni hatari sana akina dada badilikeni.

Hali ya unyanyapaa bado ni kubwa sana kwa wenye maambukizi, binafsi nimeishuhudia sana mtaani na hata mtandaoni, kwa ndugu, rafiki na jamii kwa ujumla. (sometimes huwa natamani kungekuwa na Kijiji kwa ajili ya waathirika wa UKIMWI tu, huenda tungeweza kufanya kazi zetu kwa uhuru Zaidi)

Wagonjwa wengi hawako tiyari kuweka wazi khali zao za maambukizi, kwa sababu zao mbalimali, huenda ni kwa kuhofia unyanyapaa au kutengwa na ndugu na marafiki.

Wagonjwa wengi wa UKIMWI huwa na kisasi mioyoni mwao, wakitaka kulipiza kwa kumuambukiza kila mtu watakaye jamiiana nae, kwa gharama yoyote ile. (si unaninyanyapaa acha nikukomeshe / mi mwenyewe nilipewa acha nikupe na wewe) mgonjwa wa ukimwi ukiiondoa hii utaishi maisha safi sanaaaa japo pia huchangiwa na kunyanyapaliwa ila tunapaswa kulishinda hili.

Kuna watu wachache sana wana vipimo vya HIV majumbani mwao na huwapima wenzi wao kabla ya kujamiiana nao. Hii ni hatari sana maana mteja (muathirika) akitumia ARV vizuri kuna uwezekano wa kipimo kile kushinwa kuonesha ukweli juu ya hali yake ya maambukizi, hivyo ni rahisi sana kukuambukiza pamoja na vipimo vyako vingi.

Bado kuna upotoshwaji mkubwa juu ya ugonjwa wa UKIMWI, mfano:- maombi yanaweza tibu UKIMWI (SI KWELI), mgonjwa wa UKIMWI anaweza asitumie ARV na bado Akaishi vyema (SI KWELI), UKIMWI hauambukizwi bali ni uchafu ulioko mwilini (SI KWELI na ni hatari sana kwani ukiamini hivo utaambukizwa asubuhi na mapemaaa)

Pamoja na kuwa na vyombo vya habari ni vingi lakini ukweli ni kwamba elimu juu ya ugonjwa huu bado ni ndogo sana. Elimu sahihi juu ya VVU na UKIMWI inapatikana ZAHANATI au KITUO CHA AFYA, tembelea sehemu hizi kuondoa wasiwasi wako na kupata majibu sahihi kwa maswali yako. Pia wape elimu wanao, na ndugu zako, sikuhizi mtoto ni mdogo lakini tiyari ashajaribu kujamiiana. TUWE MAKINI NA WANETU.​

KWA PAMOJA TUIJENGE KESHO MPYA, ISIYOKUWA NA VVU WALA UKIMWI

AKHASANTENI.
 
Kupitia andiko lako nimegundua wewe hauna ukimwi Ila unafanya kazi katika taasisi za Afya na uzi wako ulilenga kutazama kiwango cha elimu kuhusu ukimwi na kupata kukusanya data.

Ufahamu wako na knowledge ni kubwa Sana sio rahisi uwe umeathirika na ukimwi.

Una uwezo mkubwa Sana wakufanya intellectual analytical ambayo lay man au mtu hana maarifa na huu ugonjwa hawezi.

Niseme hongera wewe ni msomi imara.
 
Back
Top Bottom