Ng'wamapalala umeonesha upungufu mkubwa wa jamii yetu ya kitanzania, binafsi naungana na wewe kusema kwa dhati kuwa dini (tunavyomtumia Mungu) ndilo tatizo letu kubwa, nitaongezea kiasi.
Tukirudi nyuma kwenye historia na kukumbuka zile stage mwanadamu alizopitia hadi kufika sasa, tunaona kuwa tunaishi life style ya watu wa zama za mawe za kati (karne ya 5-15 hivi) na hata hivyo tumefanya mabadiliko kidogo kutoka kwa watu wa kipindi kile.
Tumejifunza kuwa wao walikuwa wanalengo moja kubwa, ambalo ni kuonesha kuwa Mungu yupo, hivyo kila mafanikio waliyokuwa wakiyapata walikuwa wanarudi wakishukuru na kuyahusisha moja kwa moja na uwepo wa Mungu. Walijitahidi kufanya kila kitu (kuutumia ulimwengu na vitu vyake vyote) kuboresha maisha yao na baada ya kufanikiwa wakamshukuru Mungu, tofauti na tunavyoishi kwenye jamii yetu kwanza Mungu baada ya hapo tunafanya kazi kutaka kuboresha maisha yetu, kila tunapokwama tuna kinga, Mungu hajapenda.
Model hii tuliyoibuni tunaiona kwa nchi zote zinazoendelea au kwa kila nchi iliyo masikini, tumejiandaa kushindwa. Ukoloni (wa ndani na kutoka nje) upo kazini, kuna wanaofaidikia sana na jamii yetu kuendelea na mfumo huu.
Tukiangalia nchi zilizoendelea tunaona wametoka kabisa kimtazamo kutoka kwenye mfumo tulionao sisi. Wao wanaamini ulimwengu na kila kitu chake vipo kwa ajili ya kututumikia wanadamu, ni jukumu letu na tupo huru kuvibadilisha ili kuboresha maisha yetu. Tunaposema tupo karne ya 21, ni kwenye makaratasi kwa kiasi kikubwa na kufuata mkumbo, ukweli ni zama za mawe za kati (feki).
Faida moja kubwa ya model hii ya maisha tuliyoibuni ni kuwa kwa kiasi flani tumeendelea kudumisha tamaduni zetu kwa hofu ya Mungu.
Ni tatizo pana na ufumbuzi wake unahitaji uongozi wa kweli, uongozi utakao weka sheria na kuzisimamia kuanzia kwenye familia, inabidi tubadili mfumo wetu, tuanze na elimu na malezi.