Lazaro Nyalandu alivyochemka kwenye BBC HARD TALK

Lazaro Nyalandu alivyochemka kwenye BBC HARD TALK

Tatizo linalowasumbua hawa viongozi ni kushiriki mambo machafu halafu wanajifanya hawahusiki kabisa.
kwa hiyo wanapohojiwa wanajaribu kuficha huku dhamira zao zikiwasuta. Hapo ndipo mkanganyiko unaanzia.

Ni kweli mkuu, kugeuza uongo kuwa ukweli ni kazi ngumu sana.

tatizo unakua unatamka kitu usichokiamini hivyo hata kujiamini kunapotea kabisa.!
 
Nitachangia baada ya kuona hayo mahojiano au ungekuwa umeonesha makosa ingesaidia
 
kwenye bible kuna mistari inasema kuwa "ukaangalie ni wapi ulipoanguka, utubu...". Therefore tanzania ni lazima iangalie ilikosea wapi, tukajirekebishe before it is more than too late.

ufunuo 2:5
 
Unajua viongozi ni waongo, ndio washiriki biashara haramu kwa hyo lazma wakihojiwa hvyo vitu haramu wanagwayagwaya kwasababu wenyewe ni wahalifu.Lawama hizi zitujie watu tunaowachagua maana wanatoka humu humu kwenye jamii yetu wao hawana makosa, makosa tunayo sisi wapiga kura.
Wawo ni sample yetu wa Tz.
 
Hivi kwa nini hawa mawaziri wetu wako so out of depth with issues?

Kajitahidi kujieleza kuhusu pembe za ndovu na mauaji lakini kwa kweli hawa mawaziri wanahitaji wafanyiwe media training namna ya kujibu maswali na kilichoshangaza zaidi ni kuwa huyu NYALANDU ni DIASPORA aliyerudi na kupewa nafasi (inawezekana kuna siri kwa nini wana diaspora wanachukiwa) lakini I wish Mkapa angefungua shule ya kuwasomesha hawa vijana kujiamini na kuweza kumwaga issues bila kutetereka

Sasa hii interview imekuwa ni kama vile TRAIN CRASH.

Sasa tufanyeje? PR imetushinda, English kwetu tatizo, ubishi ndio tunachojua, ufisadi uko kwenye DNA yetu, hatutaki kukosolewa, hatutaki kujikosoa, hatutaki kuingia kwenye duania ya utandawazi, kila kitu chetu substandard, tunawachukia zaidi waliofanikiwa kwenye maisha na biashara, hatupendi kuambiana ukweli, media yetu ni disgrace, wanaisasa wetu (opposition na ruling) nao ni kama vile wendawazimu.

Hivi sisi tumelaaniwa?

hivi kweli huu ni muda wa kufanya PR wakati waua na wafanya biashara haram wanajulikana?

What happened to the rule of Law & Order?

Mkuu kumaliza ubishi huu wa kitoto weka clips tumsikie tuamuewewe pekee haitoshi na hasa ukisema bila ushahidi wa alicho kisema .
 
Mkuu anaetambulika kama mleta mada tata kapotea katika mazingira tata!
 
huyu mleta mada na Nyalandu nani kilaza sasa, wakati mwenzie Nyalandu kahojiwa The hard Talk, Mleta mada anakimbilia JF kureport "Nothing", kama huu siyo ukilaza namba one ni kitu gani?
 
BBC HardTalk inaendeshwa na mtangazaji mkali anayefanya homework
yake vizuri sana - Steven Sucker. Kama wewe unayehojiwa hujafanya
homework ya kutosha unabaki ukibwabwaja tu kwenye maswali magumu
ya Steve Sucker! Nadhani hilo ndilo lililomtokea Lazaro Nyalandu.
 
Nyarandu mnamwonea tu.Labda tu kama mleta mada ndiyo mara yake ya kwanza kuangalia program ya THE HARD TALK by Steven Sucker.That guy is a bad news.He is so good at picking people's brains.Kwa masikio yangu niliwahi kuwasikia akina Tony Blair na Bill Clinton wakipatwa na kigugumizi cha ghafla kufuatia maswali magumu ya Steven Sucker,Siyo mtu yule hafai kabisa.Imagine hao jamaa wawili ni magwiji wa kuviteka vyombo vya habari kwa umahiri wao kuwasilisha madala na kujadili hoja lakini kwa Sucker waliishia kupatwa na kigugumizi.Kikwete hatathubutu kupeleka pua yake kwa Sucker.
 
Sasa tufanyeje? PR imetushinda, English kwetu tatizo, ubishi ndio tunachojua,

mkuu,chukua tano.pamoja na vitu vingine umeongea jambo la msingi sana.siku zote nilikuwa nadhani watz wote wanaoishi/walioishi ktk mataifa ya wazungu hasa USA na UK wana exposure kubwa na confidence ya kuchambua mambo kupitia lugha ya kizungu.kumbe sikuwa sahihi.ukiachia nyarandu,mfano mwingine ni hapa jf.kuna baadhi ya well known diasporas ambao wanajipambanua kwa uwezo wao kuandika post kwa kingereza ktk forums za saisa,MMU na chitchat.lakini hawana confidence ya kuchangia mada international forum au kenya forum ambako hukutanisha vichwa vya jf members wa nchi jirani kama kenya.nimeshuhudia baadhi yao hata wakiwa mentioned bado hawatii mguu kule. inferiority complex haimtoki mtz hata kama ataishi ulaya miaka mingi.big up to Geza Ulole .
 
Last edited by a moderator:
Wewe bila kujitambua ndiyo umechagiza yale ambayo mleta mada anayalalamikia bila kutueleza kisa chake.
Watanzania tuna matatizo ya kuikimbia njia ya kutafuta ukweli wa maswala magumu na kinzani kwa njia rahisi rahisi ya kumwigiza 'Mungu' kama ndiye saviour instead of stretching our brain to accommodate larger thinking so that, we can never shrink our brain back again to smaller thinking.
Mdiyo yale yale ya kusema tunamwachia Mungu kwa sababu Mungu anajua yote wakati uwezo wa kupambana na mazingira ulishapewa na huyo 'Mungu' wako.
Wewe tayari umeishamuweka Mungu kwenye hoja kama vile Watanzania wametenda dhambi ndiyo maana mambo yao yako nyuma kulinganisha na mataifa mengine.
Kwa hiyo nchi za Magharibi ni maraika ndiyo maana wako mbele kimaendeleo?.
Kwanza kumtaja taja Mungu bure alishasema ni dhambi hasa ikichukuliwa kuwa, solutions za matatizo yanayokukabili ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Na ukitaka kufahamu nini maana ya Bidii na maalifa, basi lazima uende kwenye darasa linalofundisha elimu ambayo mzizi wake ni kukujenga katika fikra na mitazamo ya kupambana na mazingira na kuyashinda kwa kutumia akili yako.
Ni angalizo tu.

Hello Ng'wamapalala, unaongea sawa sawa, kama wewe huishi Tanzania na hujui yanayoendelea Tanzania, but kama unaishi humu nchini unaongea jambo ambalo unalijua lakini unajitoa ufahamu.
Hivi ni kweli hatujui au hatuoni kuwa nchi yetu iko katika hali mbaya na nikitu gani kimetufikisha hapo! uongozi/utawala (governance) tulionao unatufaa? wako kwa manufaa ya taifa na raia zake? Hatukatai kuwa kuna watanzania wavivu ambao hawapendi kujituma kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, na pia pia kuna watanzania waadilifu na wachapa kazi. Na hao wachache wenye moyo bidii yao inamezwa au inadhoofishwa na wale ambao hawataki kukaa katika mstari. Mbona hata ukianza kuangalia kwenye serikali yetu, wale waadilifu na wachapakazi ndio wanaowajibishwa, wale ambao wanapigiwa kelele kwa uzembe na uwezo mdogo ndio wanaokumbatiwa.
Ina maana watanzania wote tumegeuka wanasiasa? Waziri atachachamaa na watu wanaweza kufikiri yuko serious kuondoa uvundo sehemu za kazi, lakini ukija kuangalia watamuondoa yule anayeweka kiwingu na kukwamisha madili yao, viongozi wanakazana kupanga safu kama watakavyo ili ulaji wao usikwame. Elly kusema tuangalie tulipokosea tukajirekebishe yuko sahihi. Utawala tulionao na kama tusipojirekebisha tukaacha ukaendelea huu huu miaka ujue tumeumia. Uongozi ukiwa mzuri tunaweza tukatoka kwenye shida mbalimbali tunazoziona sasa kidogo kidogo tukafunguka.
 
Hivi kwa nini hawa mawaziri wetu wako so out of depth with issues?

Kajitahidi kujieleza kuhusu pembe za ndovu na mauaji lakini kwa kweli hawa mawaziri wanahitaji wafanyiwe media training namna ya kujibu maswali na kilichoshangaza zaidi ni kuwa huyu NYALANDU ni DIASPORA aliyerudi na kupewa nafasi (inawezekana kuna siri kwa nini wana diaspora wanachukiwa) lakini I wish Mkapa angefungua shule ya kuwasomesha hawa vijana kujiamini na kuweza kumwaga issues bila kutetereka

Sasa hii interview imekuwa ni kama vile TRAIN CRASH.

Sasa tufanyeje? PR imetushinda, English kwetu tatizo, ubishi ndio tunachojua, ufisadi uko kwenye DNA yetu, hatutaki kukosolewa, hatutaki kujikosoa, hatutaki kuingia kwenye duania ya utandawazi, kila kitu chetu substandard, tunawachukia zaidi waliofanikiwa kwenye maisha na biashara, hatupendi kuambiana ukweli, media yetu ni disgrace, wanaisasa wetu (opposition na ruling) nao ni kama vile wendawazimu.

Hivi sisi tumelaaniwa?

hivi kweli huu ni muda wa kufanya PR wakati waua na wafanya biashara haram wanajulikana?

What happened to the rule of Law & Order?
Mkuu, ingekuwa vyema kama ungetuwekea alivyochemka Nyalandu, kuliko kulalamika na kueleza fikra zako.
 
Mleta mada ni sabseti ya tatizo walilo nalo Watanzania. I would say mleta mada ni janga kubwa zaidi.

Nimesoma hadi mwisho sijaona popote alipotaja kosa alilolifanya Nyalandu katika mahojiano yake.

Mleta mada ni DIV 5 ya Phillip Mulugo
 
Next time jitahidi kueleza vizuri unachotaka kuzungumzia,kwa mfano ungetueleza nini ilikuwa kiini cha mahojiano hayo kati ya Nyalandu na BBC,ilikuwa lini,wapi aliposhindwa kujieleza au kuficha ukweli wa alichokuwa anaulizwa etc ili tukuelewe,

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi kwa nini hawa mawaziri wetu wako so out of depth with issues?

Kajitahidi kujieleza kuhusu pembe za ndovu na mauaji lakini kwa kweli hawa mawaziri wanahitaji wafanyiwe media training namna ya kujibu maswali na kilichoshangaza zaidi ni kuwa huyu NYALANDU ni DIASPORA aliyerudi na kupewa nafasi (inawezekana kuna siri kwa nini wana diaspora wanachukiwa) lakini I wish Mkapa angefungua shule ya kuwasomesha hawa vijana kujiamini na kuweza kumwaga issues bila kutetereka

Sasa hii interview imekuwa ni kama vile TRAIN CRASH.

Sasa tufanyeje? PR imetushinda, English kwetu tatizo, ubishi ndio tunachojua, ufisadi uko kwenye DNA yetu, hatutaki kukosolewa, hatutaki kujikosoa, hatutaki kuingia kwenye duania ya utandawazi, kila kitu chetu substandard, tunawachukia zaidi waliofanikiwa kwenye maisha na biashara, hatupendi kuambiana ukweli, media yetu ni disgrace, wanaisasa wetu (opposition na ruling) nao ni kama vile wendawazimu.

Hivi sisi tumelaaniwa?

hivi kweli huu ni muda wa kufanya PR wakati waua na wafanya biashara haram wanajulikana?

What happened to the rule of Law & Order?
Tuwekee audio hapa ili tusijetoa maoni onevu au maoni pendelevu.
 
Sina shaka kuwa Bw. Nyalandu atakuwa amechemka, hususan kama tunazungumzia Hard Talk ya BBC. Watu wengi hupata shida kumudu mahojiano hayo. Lakini mleta mada umeshindwa kabisa kuonesha jinsi Nyalandu alivyochemka. Mathala, hujaonesha aliulizwa nini, akajibu nini, na ni kwa namna gani jibu/majibu yake yalikuwa na mapungufu. Kusema tu kachemka bila kukokotoa alivyochemka kunakufanya uonekane ni wewe ni mtu wa majungu tu. Na mtu ambaye unakemea tatizo ambalo na wewe unalo la udhaifu katika kujenga hoja.
 
mkuu,chukua tano.pamoja na vitu vingine umeongea jambo la msingi sana.siku zote nilikuwa nadhani watz wote wanaoishi/walioishi ktk mataifa ya wazungu hasa USA na UK wana exposure kubwa na confidence ya kuchambua mambo kupitia lugha ya kizungu.kumbe sikuwa sahihi.ukiachia nyarandu,mfano mwingine ni hapa jf.kuna baadhi ya well known diasporas ambao wanajipambanua kwa uwezo wao kuandika post kwa kingereza ktk forums za saisa,MMU na chitchat.lakini hawana confidence ya kuchangia mada international forum au kenya forum ambako hukutanisha vichwa vya jf members wa nchi jirani kama kenya.nimeshuhudia baadhi yao hata wakiwa mentioned bado hawatii mguu kule. inferiority complex haimtoki mtz hata kama ataishi ulaya miaka mingi.big up to Geza Ulole .
Aasante mzee ila mambo ya serikali ya Kikwete yanatia kichefuchefu si kwamba hamna watu wenye exposure bali kuna ile tabia ya kupeana madaraka kiundugu au kiurafiki au kimaslahi fulani! Hebu niambie yule mama aliyepewa uwaziri wa fedha sidhani kama hata ana diploma sasa hebu niambie mkutano wa Davos mwaka kesho akiwekwa kwenye panel ya think-tank ataongea nini kama si cinema nyingine ya Mugulo.
 
Back
Top Bottom