LATRA yavunja rekodi ongezeko la nauli, wananchi wataharuki, patashika kwenye madaladala, Viongozi wakaa kimya

MDAU TZ

Member
Jun 9, 2023
8
40
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini(LATRA), imefanya mabadiliko ya nauli kwa mabasi na daradara siku chache zilizopita,huku ikiwa ni miezi kazaa tangu wafanye hivyo,kitendo kinacho onesha ni kuvunja rekodi kwa kubadilisha viwango vya nauli mara mbili ndani ya mwaka mmoja,kitu ambacho pengine hakijawahi kutokea hapo nyuma.

WANANCHI WATAHARUKI kwasababu wamepata na mshangao,taarifa za ongezeko la nauli hazikutolewa kwa uwazi na wala hazikufafanuliwa mbele ya jamii husika,wananchi wanahisi makondakta au wamiliki wamejiamulia na sio tamko la serikali.

imefikia wakati hadi ugomvi unazuka kwenye vyombo vya usafiri na kufikishana hadi kwenye vituo vya polisi,wanaumia kuona hali yao ya maisha inazidi kuwa mbaya kwa kukandamizwa na kuendelea kubebeshwa mizigo mizito.sasa wanafikiria sehemu ambayo walikuwa wakienda kwa 500,sasa ni 600,ukiwa na 1000,huwezi kwenda kazini na kurudi.

Wananchi wanauliza maswali,kwamba LATRA wanapandisha nauli kwa kigezo cha kupanda kwa gharama za uendeshaji pamoja na mafuta,je vipato vya wananchi vimekuwa?,je siku siku mafuta yakishuka na nauli zitashuka?

wafanyabiashara wanaonekana wananguvu sana kuliko wananchi wakawaida,ni kwamba wakisema tunapata hasara,wananchi wanyonge wanapandishiwa gharama za maisha,hana subra wafanyabiashara kama walivyo na uvumilivu wananchi wanyonge.

walipa kodi wanaumia ndani kwa ndani kwakuwa hawawezi kupaza sauti zao zikasikika,lakini ukiwauliza wanasema wamechoka sana na sasa wanasubiri muda tu,wanasubiri kile kipindi cha wabukinafaso,waniger,wamali,au hata wakenya na wanaamini kama mambo yataendelea hivi ipo siku yatatokea yale ya Singapore.

VIONGOZI WAKO KIMYA,licha ya yote hayo lakini hakuna kiongozi anaejitokeza na kuwapa faraja wananchi,sio wa upinzani wala aliopo madarakani,watawa hawajali,watu wanasema hawajali kwasababu hayawahusu,wao hawana bajeti ya 1000, dagaa, robo ya unga,mkaa wa mia tatu, wala hawapandi sogea huko, geukia mbele,shikilia bomba, hawaumii kwasbabu hayawagusi haya yanayowagusa wananchi.

viongozi wanautumia upole na uvumilivu wa wananchi kuendelea kuwaumiza,hawafikirii maisha yao,wala ustawi wa vizazi vyao,bali maslahi binafsi,

Raia wanawakumbusha watawa kama hawawezi kuwasaidia basi wasiendelee kuwaumiza kwasababu wamechoka.
 
Nilichoshangazwa na LATRA, hali ilikuwa imetulia na wametoka kupandisha nauli mwaka jana.. kwanini wakakaa na kuleta sintofahamu ambayo haikuwepo! Gharama gani za uendeshaji zilizoongezeka ambazo mwaka jana hawakuziweka kwenye consideration wakati wanapandisha nauli mara ya kwanza.

Wafanyabiashara wanataka faida kubwa kuelekea wasafiri wa mwisho wa mwaka wakalobby Latra..
 
Leo nilipanda daladala ya Tandika _kariakoo ,kazi yangu ilikuwa moja tu kupandisha sauti kuwaelimisha watu mchawi wenu ni CCM ,nimewaambia ilitakiwa nauli iwe 5000 ili vijana Kwa wazee tutoke barabarani Kwa lazima ili mchawi ajulikane ,nikawaambia nyinyi kila siku Simba na yanga Kwa hiyo nauli hizo zinatakiwa ziongezeke ,akina mama nikawaambia muwaulize maswali hao viongozi wa ccm Kwa nini Hali hii!!! Mwisho nikashuka kwenye gari lakini ujumbe uliwakolea sana
 
20231209_135117.jpg
 
Tatizo huu upandaji wa gharama za bidhaa na huduma mbalimbali, hauendani kabisa na kipato cha wananchi walio wengi. Na hapa ndipo kwenye tatizo kubwa.

Maisha yanazidi kuwa magumu kila uchwao.
Tatizo waandishi watanzania na wenyewe wamekua magoigoi hii nchi maskini ametelekezwa tangu magu amekufa mchwa wako Kila mahali mama hata Hana habari kabisa
 
Back
Top Bottom