Hivi LATRA ipo kwa ajili ya kudhibiti bei kwa ajili ya Mkoa wa Dar es Salaam tu?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Shot.jpg
Kumekuwa na kilio cha kupanda nauli kwa mara mbili kwenye vyombo vya usafiri Nchi nzima,lakini cha ajabu Serikali na LATRA wameshughulikia watu wa Dar pekee.

Sasa naomba kuuliza huko mikoani nauli zimepanda mara tatu lakini serikali haihangaiki wala hakuna wa kuwasemea ila watu wa Dar ndio mnaowasemea.

Hii sio sawa,kama vipi ondoeni maofisa wenu mikoani warudisheni Dar ambako ndiko mnawajali na kuwasikiliza..

Kiukweli nimekwazika Sana yaani sijasikia mkuu wa Mkoa wala nani akiwasemea wananchi wa kikoani.Nauli ya bajaji imetoka 500 hadi 1000 kituo hadi kituo.

Nauli ya boda imetoka 1000 hadi 2,500 kituo kwa kituo.Wakuu wa Mikoa wako kimya,LATRA wako kimya na Polisi nao wako kimya.Hii sio sawa,Tanzania sio Dar au Dodoma - pekee.

=======

Latra CCC yakataa viwango vipya vya nauli​

Summary

  • Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekataa mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.
Dar es Salaam. Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) limekataa mapendekezo ya nauli yaliyotolewa na wadau wa usafiri wa masafa marefu na mafupi.

Uwamuzi huo umefikiwa leo Jumatano Aprili 13, 2022 baada ya Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam kupendekeza kiwango cha nauli kuwa mara mbili ya nauli inayotozwa sasa.

Akiwasilisha viwango hivyo Katibu wa umoja huo, Suleiman Kimwe amesema umependekeza viwango vya nauli kuwa mara mbili ya ilivyo sasa

"Kwa maoni yetu tunaomba ongezeko la nauli ya Sh400 kwa kila njia. Mfano kwa nauli ya Sh500 iwe Sh900 “amesema Kimwe.

Hata hivyo Kaimu Mtendaji wa Latra CCC, Leo Ngowi amesema kuwa safari za mjini ni fupi na abiria wengi wamekuwa wakipanda na kushuka njiani huku mabasi hayo kubeba abiria kupita kiasi.

Katika kuchambua viwango hivyo, Ngowi amesema wamebaini maombi ya nyongeza ni tofauti na bei ya mafuta iliyoongezeka.

"Tunapendekeza wasilisho hili lirudishwe kwa mtoa huduma, lakini kama wanazungumzia hasara pia tunashauri kutumia mfumo wa kuzuia mianya ya upotevu kwa kumtumia tiketi mtandao," amesema Ngowi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kumekuwa na kilio cha kupanda nauli kwa mara mbili kwenye vyombo vya usafiri Nchi nzima,lakini cha ajabu Serikali na LATRA wameshughulikia watu wa Dar pekee..

Sasa naomba kuuliza huko mikoani nauli zimepanda mara tatu lakini serikali haihangaiki wala hakuna wa kuwasemea ila watu wa Dar ndio mnaowasemea..

Hii sio sawa,kama vipi ondoeni maofisa wenu mikoani warudisheni Dar ambako ndiko mnawajali na kuwasikiliza..

Kiukweli nimekwazika Sana yaani sijasikia mkuu wa Mkoa wala nani akiwasemea wananchi wa kikoani.Nauli ya bajaji imetoka 500 hadi 1000 kituo hadi kituo.

Nauli ya boda imetoka 1000 hadi 2,500 kituo kwa kituo.Wakuu wa Mikoa wako kimya,LATRA wako kimya na Polisi nao wako kimya.Hii sio sawa,Tanzania sio Dar au Dodoma- pekee.
Mmmh 1000 paka 2500
 
Naomba kuuliza Kama LATRA Wana ofisi mkoa wa pwani. Nauli zimepanda kwa zaidi ya asilimia 100 njia ya Mbezi Mlandizi.
LATRA tunaomba nauli mlizopendekeza
 
Hii sio sawa,kama vipi ondoeni maofisa wenu mikoani warudisheni Dar ambako ndiko mnawajali na kuwasikiliza..

Kiukweli nimekwazika Sana yaani sijasikia mkuu wa Mkoa wala nani akiwasemea wananchi wa kikoani.Nauli ya bajaji imetoka 500 hadi 1000 kituo hadi kituo.

Nauli ya boda imetoka 1000 hadi 2,500 kituo kwa kituo.Wakuu wa Mikoa wako kimya,LATRA wako kimya na Polisi nao wako kimya.Hii sio sawa,Tanzania sio Dar au Dodoma- pekee.
Hizo Daladala, bajaj na bodaboda nyingi ni za hao vigogo pamoja na traffic police
 
Mitandaoni wananchi wanakolalamika wote wanasema wanaishi dar.

Hata hapa jf tu, watu kibao husema wako dar ilhali si kweli ila tu waliwahi kuishi hapo.

Haya ingia fb 80% ya watu profile zao ni wakazi wa dar.
 
Back
Top Bottom