LATRA ichunguzwe na mamlaka katika mfumo mzima wa tenda za kufunga Ving'amuzi (VTS), Kuna shida mahali

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
KUNA MENGI YA HOVYO YANAENDELEA KWENYE HII TAASISI, TUNAJIULIZA KAMA MH. WAZIRI MKUU AMEWAWAJIBISHA MENEJA WA TANESCO NA WATU WAKE KWA TATIZO LA KUPATIKANA KWA LUKU. JE HAWA WATU WA TEHAMA WA LATRA WANAAACHWAJE KWA UBABAISHAJI WA KWENYE MFUMO WA ONLINE TICKETING NA KUTUSABABISHIA WENGINE HASARA NA MENGINE YA HUDUMA KUTOPATIKANA AU KWA UBABAISHAJI KWENYE MFUMO HUU?


Ni sisis Wadau wa Usafirishaji wa abiria Arusha kwa niaba ya wadau wengine Tanzania

Nakala ya Malalamiko haya kwa TABOA kwa ufuatiliaji zaidi.
 
"Mkurugenzi mkuu wa LATRA anapaswa kuwa Lockup kueleza inakuwaje Mtoa huduma yuleyule na ving'amuzi ni vilevile, lakini kwenye mabasi ambapo msimamizi ni LATRA gharama anaifanya kuwa ghali mara mbili zaidi ya kwenye Malori bila sababu za msingi kuwekwa wazi ilhali Malori yanakwenda mpaka nje ya nchi ambako gharama za king'amuzi zinaongezeka" .

Ni nani anaechukua hiki kilichozidi ?

Tumepigwa kweupe hapa!
 
"Mkurugenzi mkuu wa LATRA anapaswa kuwa Lockup kueleza inakuwaje Mtoa huduma yuleyule na ving'amuzi ni vilevile, lakini kwenye mabasi ambapo msimamizi ni LATRA gharama anaifanya kuwa ghali mara mbili zaidi ya kwenye Malori bila sababu za msingi kuwekwa wazi ilhali Malori yanakwenda mpaka nje ya nchi ambako gharama za king'amuzi zinaongezeka" .

Ni nani anaechukua hiki kilichozidi ?

Tumepigwa kweupe hapa!
Mama keshasema watu wasisumbuliwe, baaaasi!

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na magumashi katika ununuzi wa hivi vifaa bado kuna rushwa katika ufatiliaji wake. Bus nyingi zina hivi vifaa na bado wanatembea zaidi ya speed 120.
Yaani ni mambo ya hovyo sana chini ya hii Mamlaka. Nadhani wakati wa hii LATRA kuja na maono mapya
 
Hivyo ving’amuzi ndio zile tunaita GPS ya kutrackcmwenendocwa gari hasa speed ili ukizidisha speed ujulikane? Au ni ving’amuzi vyabina gani hivyo na vinazuiaje ajali?
 
Tatizo ni mambo ya Tenda na kulea monopoly. Kama kungekuwa na soko huria ambalo viwango pekee ndio viko regulated, usingesikia hii mambo.

Taboa bado mko karne ya 19. Mkihitaji system mnaitisha tenda. Hii mambo za kizamani sana. Unataka system weka vigezo, ruhusu watu wapige kazi wakikidhi vigezo. Hii ingewasaidia kuongeza ushindani na kupata huduma bora.

Same advice ningeshauri kwa LATRA. Wasipende kulea monopoly. Encourage watu wote wenye uwezo wa kukidhi viwango wafanye kazi. Itaongeza ushindani na wala wao hawatalazimisha watu kushusha bei, soko litawalazimisha kwa sababu ya ushindani..
 
Kwako Afande Hamduni,

Kwanza nikupongeze kwa uteuzi uliofanyiwa na Mama yetu. Hakika inaonesha ana imani kubwa na wewe.

Sisi wadau wa usafirishaji tulilipeleka hili suala kwa mtangulizi wako lakini ni kama aliweka pamba kwenye masikio. Pongezi kidogo kwa Mh. Waziri mkuu aliliingilia lakini ni kama LATRA wamekaidi maagizo yake. Inasemekana huu mfumo uliletwa na Sumatra chini ya Bwana Ngewe kwa ajili ya mapambano dhidi ya ajali. Well and good. Tatizo linakuja katika utekelezaji wake ambao una viashiria vingi vya upigwaji hela na sintofahamu kama ifuatavyo:

1>Hapo awali tulifungiwa hivi vifaa kwa utaratibu wa kukodishwa kwa Elfu 60 kwa mwezi lakini kuna taratibu za kununua kifaa ambazo hazikuwekwa wazi mpaka Mh Majaliwa alipoingilia kati na kulazimisha bei kuangaliwa upya. Lakini tulipowauliza wenzetu wa malori ambao wamefungiwa na kampuni hizohizo za vingamuzi kwa vifaa hivyohivyo wao walikuwa wakilipa kwa Elfu 30 mpaka 40 kwa mwezi. Nini kilisababisha sisi kupigwa hivi, je Sumatra hawakufanya upembuzi kuhusu hizi bei??

2> Baada ya Mh. Majaliwa kuingilia kati kuhusu bei hizi kuwa kubwa sababu kifaa kilikuwa kinauzwa shilingi Laki 5 wakaamua kutufungia kwa hiyohiyo Laki 5 na mwezi tukalipia elfu 40 ambayo LATRA waliikubali bila kuchunguza. Baada ya kelele nyingi wakapunguza mpaka Elfu 30 ambayo bado ilileta zengwe. Baadaye kuna mfungaji mmoja mpya akaja na bei ya Elfu 20 kwa mwezi na kifaa laki 4 na nusu ndipo hawa wanyonyaji wengine wakashusha kuwa 20 kwa mwezi sababu waliona wameanza kupoteza soko.
Je zile gharama zao za uendeshaji zilipunguaje hadi kufanya waporomoke toka elfu 40 kwa mwezi mpaka elfu 20??.. Kama sivyo ni kweli walikuwa wakipata faida mara 2???. Mbona wenzetu wa Malori waliouziwa hivi vifaa walikuwa wanalipa 15 mpaka 25 kwa mwezi kama wakinunua kifaa na magari yao yanaenda mpaka nje ya nchi amabako inasemekana gharama inakuwa kubwa kwa vingamuzi??. Je kuna Gharama zozote Sumatra walikuwa wanawachaji hawa wafungaji maana tulisikia hata mtandao wa imu huwa wanalipa Sumatra.

3>Sisi kama wasafirishaji tulipokea agizo la waziri mkuu kupitia Taboa kuwa kuna Marekebisho ya bei, lakini marekebisho hayo hayakuletewa mrejesho mpaka leo zaidi ya hizi kampuni kupunguza bei kimagumashimagumashi na bado tunalazimishwa kulipa bila LATRA kuwa na bei Elekezi. Mpaka hivi sasa kuna Kampuni mbili ya Flet na Tela ambao wanatuuzia vifaa hivyo kwa laki 5 wakati wenzao wanauza mpaka kwa laki tatu na nusu. Lakini vifaa hivyohivyo tunavyouziwa sisi kwa laki tano, kuna wenzetu wa Malori wanauziwa mpaka Laki tatu na Nusu na kampuni hizohizo. Je nini kinafanya gharama ziwe juu?.. LATRA wanawachaji hawa jamaa chochote kitu?.Kama lah LATRA hajachunguza hiki kitu?

4> Pia uataratibu mzima wa Warranty ni ubabaishaji, tunaambiwa vifaa vina mifumo ya kuzuia shoti, Lakini kifaa kikiharibika wanasema gari zetu zimeshoti kimekufa tulipie laki 5. Yaani gari yangu Mpya ina miez3 ina shoti kinakufa kifaa chao tu??. Ukimwambia akuonyeshe hiyo shoti au amejuaje ni ubabaishaji, Ukigomea , hawakubadilishii na LATRA wanakusubiri stendi Singida wanazuia gari isifanye kazi mpaka ufungiwe kifaa au unaandikiwa Laki 2 na nusu. Kiufupi huu mradi una nia njema lakini umekaa Kiupigaji waziwazi.

5>Kingine tunaambiwa kuna kampuni ya TELA ambayo tayari ina tenda ya kufunga lakini kuna tetesi kuwa kuna kampuni inaitwa Ict nayo imepewa tenda lakini ina uhusiano wa karibu au ni kama zina undugu wa karibu unaotupa shaka kwani mapaka vifaa vyao ni aina moja, bei zao zinafanana na hata wafanyakazi wao wana aina fulani ya muingiliano.Kwa uwezo wa taasis yako unaweza kupata jibu ya hili jambo.

6> Pia kuna tetesi ya kampuni moja mbayo sisi kama watu wa Mabasi kupitia taboa tuliipendekeza nao wafunge vifaa hapo mwanzoni kuleta usawa sababu latra walikuwa na mfungaji wao mmoja. Hii kampuni imeendelea kufunga vifaa licha ya tetesi kuwa hawajawahi kushinda hiyo tenda na kuna vikampuni vipya kama vinne vimekuja na kupewa tenda lakin hawa hawajawahi kutangazwa kushinda zabuni yeyote licha ya kutoa huduma ya kiwango kilekile kama wengine. Tunajiuliza kwa nini kwenye Tenda hizo mpya hawakupitishwa sababu tayar wanafunga na wana vigezo AU kama hawana sifa za kutoa kwa nini wanaendelea kutuhudumia na kufunga vifaa?.

7> Haya makampuni pia yanakingiwa kifua na Latra kwani kuna mengine yana huduma mbovu, yanatuchelewesha safari, yanatuababishia faini zisizo na msingi sababu ya kutochukua hatua za kurekebisha vitu vyao kwa haraka lakini hatusikii Latra wakiwawajibisha kabisa zaidi ni kutupiga sisi mafaini hata kwa makosa ya vifaa kutofanya kazi au kushoti wakati ni matatizo ya ufundi ya mfungaji.

"Mkurugenzi mkuu wa LATRA anapaswa kuwa Lockup kueleza inakuwaje Mtoa huduma yuleyule na ving'amuzi ni vilevile, lakini kwenye mabasi gharama ilifanywa kuwa ghali mara mbili zaidi ya kwenye Malori bila sababu za msingi kuwekwa wazi ilhali Malori yanakwenda mpaka nje ya nchi ambako gharama za king'amuzi zinaongezeka" : Tumepigwa kweupe hapa!

UCHUNGUZI UANZE MARA MOJA KWENYE HILI KWANI HIVI VIFAA TUMEAMBIWA TUNAFUNGA KUDHIBITI AJALI NA SI KUNUFAISHA WATU KWA KIASI HIKI CHENYE UBABAISHAJI.NA PIA MALALAMISHI MENGINE YA WASAFIRISHAJI HASA KWA MKURUGENZI MKUU WA LATRA MAANA YEYE NDO MSIMAMIZI MKUU MWENYE MAAMUZI YOTE YA MAMBO YA MSINGI.


KUNA MENGI YA HOVYO YANAENDELEA KWENYE HII TAASISI, TUNAJIULIZA KAMA MH. WAZIRI MKUU AMEWAWAJIBISHA MENEJA WA TANESCO NA WATU WAKE KWA TATIZO LA KUPATIKANA KWA LUKU. JE HAWA WATU WA TEHAMA WA LATRA WANAAACHWAJE KWA UBABAISHAJI WA KWENYE MFUMO WA ONLINE TICKETING NA KUTUSABABISHIA WENGINE HASARA NA MENGINE YA HUDUMA KUTOPATIKANA AU KWA UBABAISHAJI KWENYE MFUMO HUU?


Ni sisis Wadau wa Usafirishaji wa abiria Arusha kwa niaba ya wadau wengine Tanzania

Nakala ya Malalamiko haya kwa TABOA kwa ufuatiliaji zaidi.

Hii nchi imechezewa sana. Kama TAKUKURU, kama TRA, nk, LATRA nao dhulumati mwingine wa wazi kwa mwamvuli wa serikali pendwa ya awamu ya tano.
 
Kwanza hii LATRA hivi imetokea wapi...

Maana zamani ilikua una deal na Sumatra na TRA tuu...
 
Ukiona mfanya biashara analalamikia vitu vidogo vidogo, hiyo ni dalili kuwa biashara imeanza kumshinda.
 
tu
Tatizo ni mambo ya Tenda na kulea monopoly. Kama kungekuwa na soko huria ambalo viwango pekee ndio viko regulated, usingesikia hii mambo.

Taboa bado mko karne ya 19. Mkihitaji system mnaitisha tenda. Hii mambo za kizamani sana. Unataka system weka vigezo, ruhusu watu wapige kazi wakikidhi vigezo. Hii ingewasaidia kuongeza ushindani na kupata huduma bora.

Same advice ningeshauri kwa LATRA. Wasipende kulea monopoly. Encourage watu wote wenye uwezo wa kukidhi viwango wafanye kazi. Itaongeza ushindani na wala wao hawatalazimisha watu kushusha bei, soko litawalazimisha kwa sababu ya ushindani..
hata sisi tumeshajiuliza sana kwani hata hao wanaoshinda hizo tenda kuna wengine inasemekana kuwa hata vigezo hawakuwa navyo kabla ya tenda kutangazwa. yaani hata hiyo biashara walikuwa hawafanyi
 
Hizo pesa mnazolipa mlikuwa mwatoa kwa pesa taslimu au mnapewa control number? Hapo panaweza toa hisia halisi.
 
Back
Top Bottom