Land Rover Discovery 4 - Mega thread

The Butcher

JF-Expert Member
May 24, 2015
237
500
Wakuu kuna hawa jamaa wa arusha waitwa capitalzone wanatengeneza landrover 110 mnawaonaje? Na je? Vile vifaa wanavyotumia ni genuine? Mfano engine na vingine kwenye gari..
 

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
1,572
2,000
Wakuu kuna hawa jamaa wa arusha waitwa capitalzone wanatengeneza landrover 110 mnawaonaje? Na je? Vile vifaa wanavyotumia ni genuine? Mfano engine na vingine kwenye gari..
Vifaa ni genuine kutoka Land Rover, wao wanafanya kazi ya kufufua gari kuukuu na kurejesha katika hali nzuri.
 

Nsemwalawi

New Member
Nov 3, 2018
1
20
Wabongo bwana gari kama sio toyota kwao ni shida ,kueni wazi mnaozikosoa zinasubua nini sio mnasema tu nimbovu
 

biharamulojr

Member
May 2, 2017
8
45
Mkuu dengue nunua hiyo gari mimi navutia tela nabeba trekta 165Fm au 135mersey ferguson toka mpumalanga mpaka mbeya na haili mafuta na ina nguvu sana ni disco 3 v 6 ina uzito tani 3 halijawahi kusumbua na mwezi huu linatoka tena na trekta kama kawaida...nipm namba nikutumie picha uitume hapa naona mm hapa inasumbua... d 4 mapumziko yamezidi zaidi hizo gari ukiona dereva kafanikiwa kuipindua matairi manne yote yawe juu unapata zawaidi kwa kupelaka hiyo picha Johannesburg Landrover photoshop wataijua...


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,130
2,000
Jamani mimi naomba mnisaidie. Naona serikali yetu inazima ndoto za wengi kumiliki usafiri. Yaani kodi hazishikiki kabisa. Kitu kingine...gari inavyozidi kuwa mpya ndo inazidi kuwa na ushuru mkubwa wakati nilifikiri kinyume chake kwamba serikali ita kuwa ina encourage watu wanunue magari ya miaka ya karibuni kulinda mazingira. Lakini leo ukisema ulete gari ya 2017 au 2018 au 2019..Kodi yake ni kizungumkuti. Kwa nini?
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,829
2,000
Jamani mimi naomba mnisaidie. Naona serikali yetu inazima ndoto za wengi kumiliki usafiri. Yaani kodi hazishikiki kabisa. Kitu kingine...gari inavyozidi kuwa mpya ndo inazidi kuwa na ushuru mkubwa wakati nilifikiri kinyume chake kwamba serikali ita kuwa ina encourage watu wanunue magari ya miaka ya karibuni kulinda mazingira. Lakini leo ukisema ulete gari ya 2017 au 2018 au 2019..Kodi yake ni kizungumkuti. Kwa nini?
Bado serikalini kuna fikra na mitazamo ya kijamaa: kwamba kumiliki gari ni ufahari. Hivyo, kuwekwa kwa kodi nzito nzito kwa kufikiria kwamba wamiliki magari ni watu matajiri sana.
 

Eminentia

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,648
2,000
Usijaribu kununua discovery utaliuguza kila siku. Hayo magari ni spana mkononi, safari moja shamba nyingine garage.

Ni magari mazuri kwa muonekano na nguvu ila hayafai yanaharibika kila siku. Kuhusu mafuta hayanywi yanabugia, ukiongelea discovery unaongelea cc4300 na zaidi, si mchezo. Labda yapo yenye uwezo mdogo fuatilia. Ushauri wangu usichukue discovery.
Nyie sijui hizi maneno mnatoa wapi..?? Mnakaa vijiweni sana bila shaka !!

Kwann ya cc 2700 si discovery ?
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,829
2,000
Kwa kuwa nimeendesha zote hizo mbili kwa kweli Touarag VW ni nzuri na imeipita mbali kwa usalama wa uendeshaji wa discovery
Don't get me wrong, hata land rover ni gari nzuri na zote nimebahatika kuendesha tena za 2018 ( zimeshatoka huku niliko)

Touareg imetulia sana na features zake ni sawa na discovery ila kuna extra zimo kwenye VW
Kwa mfano ukikata kona na taa zinamulika unakopita bit of a trick yaani taa zinageuka amazing
Pia cruise control inakuja kama standard yaani hulipii kama extra

All in all VW iko juu zaidi na sio rahisi pia
Bending lights....hiyo tech ipo kwenye Volvo kitambo....
 

Comrade 01

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
535
500
Tatizo mafundi wetu nao wanawadanganya sana watu.. ooh hiyo gari mbovu, sijui injini kimeo.. kumbe wao ndio wako nyuma kiteknolojia na wamezoea garage zetu za chini ya mwembe zinazotengeneza 109 za carburetor.
Siku hizi gari full umeme, mafundi jiendelezeni jamani.
By the way, disco 4 ni mwisho wa njia, sema spea zake sio nyingi na mafundi pia wachache, hivyo ikiharibika ujiandae na mpunga wa kutosha kupata spea nyingine..
Daaah hiyo 109 ndio gari yangu ni V8 engine,nimefunga gearbox ya R380 ni moto mwinginee aisee
 
Top Bottom