Land Rover Discovery 4 - Mega thread

kuna Toyota hilux 3.0 D4D Legend 45 4 ×4 ya 2016 model hii pick up ni hatari sana sana...kupoteza kumbukumbu ni tatizo la computer box na si engine linatatuliwa kwa kuunganisha waya zako ukiwa chini na kifaa chako basi magari mengi yanapoteza kumbukumbu na si Tatizo la engine hilo...
 
Mkuu @ Isanga family hii Bei ni ya sasa kwa South Africa, jamani hii gari naipenda, namwomba Mungu aniwezeshe kuimiliki, hata iwe private jet na hii gari ntachagua hii gari. nikiwa napita barabarani na boxer nikiona road mpaka nageuza shingo kuisindikiza na macho, kukiwa na foleni nikiiona ntajichomeka kukaa nyuma ya hii gari.
 
bobtony Mungu ni mwema utapata tuu na pia zinapungua bei kila miaka inavyokwenda ila Disco 3 sio ghari ni rand 100,000 mpaka 150,000 kama Tsh 16,000,000 kununua tuu mpaka 20milion ila kodi ipo 24milion kwa boda maana hakuna gharama za bandari na viingereza vingine tena na ya 2005 model mpaka 2007 model ndio zipo bei hizo mbele zaidi zipo bei juu...
 
Usijaribu kununua discovery utaliuguza kila siku. Hayo magari ni spana mkononi, safari moja shamba nyingine garage.

Ni magari mazuri kwa muonekano na nguvu ila hayafai yanaharibika kila siku. Kuhusu mafuta hayanywi yanabugia, ukiongelea discovery unaongelea cc4300 na zaidi, si mchezo. Labda yapo yenye uwezo mdogo fuatilia. Ushauri wangu usichukue discovery.
Tatizo mnakimbilia Yale ya petrol. Tafuteni ya diesel & make sure Ni ya u.k. Mfano tafuta old model td300
 
Discovere 5 a.k.a Discover Sports Nomaa yani hapo nilijitahid kulipiga picha
1470780264428.jpg
 
Kwenye ford ranger napingana na wewe, jaribu kuzunguka huko uone zilivyokufa,nina watu wanne ambao nawafahamu walikuwa nazo, zote zimekufa engine,labda uniambie Amarok yule ndio kaka mkubwa wa p/up.
Ford ranger latest zimeanza 2012 hivi, nyingi bado zimo kwenye warranty, nafikiri unaelewa gari ikiwa kwenye warranty inakuwaje engine ikijifia. Kama unazungumzia za zamani hata toyota zipo kibao zimekufa mitaani na gari usipoitunza kufa ni kawaida si toyota wala nissan.
 
Ford ranger latest zimeanza 2012 hivi, nyingi bado zimo kwenye warranty, nafikiri unaelewa gari ikiwa kwenye warranty inakuwaje engine ikijifia. Kama unazungumzia za zamani hata toyota zipo kibao zimekufa mitaani na gari usipoitunza kufa ni kawaida si toyota wala nissan.
Hizo latest zinaitwa t6,ndio body type yake na engine inayotumia inaitwa duratech au puma engine,ambazo zipo katika landrover 110,sasa tafuta mtu mwenye hiyo 110landrover halafu muulize problem gani kubwa anayoi experience,au nenda sehemu kama arusha kwa wale watu wa safari waulize kwa nn hawaweki hizo landrover 110,kwenye fleet zao.

Engine ya Amarok bado haija diagnose any failure bro,usibishane am into these things physically.
 
Hizo latest zinaitwa t6,ndio body type yake na engine inayotumia inaitwa duratech au puma engine,ambazo zipo katika landrover 110,sasa tafuta mtu mwenye hiyo 110landrover halafu muulize problem gani kubwa anayoi experience,au nenda sehemu kama arusha kwa wale watu wa safari waulize kwa nn hawaweki hizo landrover 110,kwenye fleet zao. Engine ya Amarok bado haija diagnose any failure bro,usibishane am into these things physically.
Siko hapa kubishana. Na mimi maisha yangu yanaendeshwa na hayo madude. I'm out.
 
Kwenye ford ranger napingana na wewe, jaribu kuzunguka huko uone zilivyokufa,nina watu wanne ambao nawafahamu walikuwa nazo, zote zimekufa engine,labda uniambie Amarok yule ndio kaka mkubwa wa p/up.
Mkuu acha kulinganisha amarouk na vitu vya kijinga, ile Volkswagen ya mjerumani, weka mbali na watoto.
 
Cheki Amarok problem South Africa,Latin America na hata German ingiza kwa nchi moja utapata matatizo yake 2012 kuna wateja South Africa walirudisha gari zipatazo 15200 kwa kwa Engine kukosa nguvu na matatizo mengine mengi tuu matatizo ya magari yapo on line cheki utayapata tuu Tanzania Amaroki zipo ngapi mpaka iwe kipimo cha hilo gari au mtu kupata 8000km on clock Tanzania inamchukua muda gani kama sio mwaka...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom