Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

Kama wewe Masanja mungu amekujalia ukalima ukafanikiwa mshukuru mungu sana hiyo bahati kwani kama ni kulima robo tatu ya watanzania ni wakulima lakini mpaka leo hawaja fanikiwa mim ndugu alilima mahindi ekati 200 yalikauka yote mpaka na alikufa kwa presha kwahiyo sio kila alimae anatajirika bahati pia kwani wakulima wote mnaolima huko mbarali wote ni mataji kama wewe ukipata shukuru acha kejeli kwa ambao hawaja fanikiwa
Unapofanikiwa usijiinue ukadhani wenzio hawana bidii, ukute wengine wana hustle kuliko hata wewe,sometimes ts sheer luck
Bt case ya masanja ni sembe
 
Sawa ila topic at hand ni kilimo vs mafanikio ya masanja,awafundishe kwanza wenzie wa orijino komedi
Si uache tu kazi....hivi huwa mnalal a usingizi mtamu kweli maana naona kama mnateseka kweli...
 
Alicho kifanya Masanja ni kutumia chuki iliyopo kwa hawa jamaa kuhalalisha mawazo yake na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa ,
Mimi nauza maji ya kandoro Mkuu
Afadhali yako mkuu ...hata hawa mateller unawazidi mkwanja...
 
Masikini akishapata lazima ... ilie mbwata. Hivi Masanja wakati unazunguka na bidhaa jijini ukiwa mmachinga hayo mashamba yalikuwa yamekwisha huko kwenu Ludewa. Leo hii unabeza kazi za wateja wako waliokuweka mjini kitambo.

Kila kazi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na mzunguko wa life kiujumla, ni mpuuzi pekee awezaye kufikiri wote tunaweza kulima nyanya au auze maji na wote tuwe na maisha mazuri. Hao wanaolipwa laki 5 wote wakitoka ofisini wakauze maji au kulima vitunguu atanunua nani?

Kilimo kingekuwa simple kama unavyobwatuka unadhani nani angekuja mjini kufanya kazi ya laki 5 unayoibeza, mbona Masanja ulikuja ukakomaa hapa hadi ukatoka baada ya kuungua sana na jua. Ulishakuwa hadi HOUSEBOY wewe, leo hii teller wamuona kama hana akili au hana malengo na maisha haya.

Mmekaa tu mnaongelea kilimo kana kwamba ni rahisi saaana. Mngejua watu wanaozewa na mazao mashambani huku kwa kukosa masoko. True vipo vinavyolimwa vinalipa haraka lakini havistawi nchi nzima na kwingineko gharama za kuvilima si ndogo.

Masanja hukutoka kwa sababu una akili kuliko vijana wanaosota,huo ni mzunguko wa maisha tu na bahati iliyochagizwa na kipawa. Ulijituma ndio lakini haimaanishi wasiotoka hawajitumi. Chunga kauli zako bro.
...kula like..umenena vyema!!..na babake au ndungu zake huko ludewa c wakulima mbona hawajatoka had leo hii wapo ludewa wanalima..masanja hii ni dunia bado una safar ndefu usianze mashauz kijana!!
 
Nenda na laki tano yako uone kama hukurud mjini kwa miguu!!! Aache kudanganya watu. Kama ni kilimo cha biashara lazima uwe na mtaji wa kutosha baada ya kupiga hesabu za kuanzia kukodi shamba, kulipa wafanyakazi, pembejeo mpk kuvuna
ana assume mtu hali! all other factors remain constant! uchumi wa waliokosa shule ni sheedah!
 
Wapo wanaopinga ujumbe wake, lakini alichosema haimaanishi kama ni benk teller aache kazi yake akalime, hapa kinachotakiwa ni kwamba kipato kidogo ambacho mtu anapata kutoka kazi yake anayoifanya asikitumie katika anasa, bali awekeze katika mambo yatakayomletea faida hapo baadae, watu wafanye saving ya kile wanachokipata, ukipata mshahara usikimbilie kununua vitu vya anasa kama simu za bei juu na kujiachia kwenye starehe kwa kufuata mikumbo angali kipato hakiruhusu! Tuwekeze katika kile kidogo tunachopata kwa kuwa na uthubutu! Lipo tatizo la wengi kuogopa na kuanza kuwaza ikitokea ukipata hasara utafanyaje, kwa kuwaza hivyo huwezi kufanikiwa...
 
Wakuu hayo maneno sio ya masanja! Hiyo msg imetumwa sana kwenye Whatsup siku hizi za karibuni!
 
Umeona sasa hapa inadhihirisha kabisa chuki yako kwa hawa jamaa ,wala mimi kuwazidi mkwanja siwezi kwa maji ya kandoro nayouza kwenye vimfuko
Mbali sana mkuu unawazidi sema wao wanakuzidi labda zile gari zao za mkopo.....
 
watu wote wanapenda kutajirika na kuwa na maisha mazuri lakini siyo kazi rahisi kama anavyofikiria. Je,ukienda kulima kilimo cha matiki maji au maharage alafu mabadiliko ya hali ya hewa yakakuadhiri? Je,bank teller akienda kijijini kulima,huduma za kibenki mtazipatia wapi na nani atawahudumia na kuwatunzia hela zenu?
Je,unadhani kwamba bank teller ndo mwenye kipato kidogo kuliko wote? kwa nini asingewaambia wasaidizi wa ndani wapige kazi kwa miezi kadhaa kisha wakishapata hiyo laki tano warudi kijijini wakalime?
Ukweli ni kwamba wote tunategemeana na itabaki kuwa hivyo.
anawadharau bank tellers na wote wenye kipato cha chini paipo kujua kuwa hata matajiri wakubwa zaid yake pia wanamcheka yeye.
Mkuu ma bank teller wengi wao ni wajivuni sana,Hawana adabu Halafu ni wezi. Kwa sababu anafanya kazi bank basi ni balaa. Ukiwa mzowefu bank utayajuwa yote.
 
Kwahiy
mwenzako mkulima mkubwa sana wa mpunga we endelea kusema unga tuu kila anayefanikiwa..
Kwahiyo Masanja ndie wa kwanza hapa Tanzania kulima au?
Je unafahamu Mali anazo miliki?
Je uliwahi kusikia tetesi kuwa ktk Majina 400 ya JK alikuwemo?

Je anamiliki Ekari na trekta ngapi? Je yumo ktk record za wakulima bora Tz?

Mue mnaacha kudanganywadanganywa na nyie kisha kukaririkariri bila kufanya hata ki utafiti kidogo tu
 
Mafanikio ya mwanadamu ni mchakato unaohitaji....KUJITUMA NA NIDHAMU YA HALI YA JUU.....
NIDHAMU NDIO MSINGI WA MAFANIKIO YA KILA KITU NA KUJITUMA.....UNATAKIWA UWE NA NIDHAMU KATIKA KUUTUMIA MUDA WAKO....UNATAKIWA UWE NA NIDHAMU KATIKA KUTUMIA KIPATO CHAKO VYEMA....

VIJANA WENGI WA MIJINI KAMA HAWATABADILIKA NA KUBADILI STYLE YA MIASHA YAO NA JINSI WANAVYOYACHUKULIA MAISHA DAIMA WATABAKI KUWA WATAZAMAJI WA MAFANIKIO YA WATU WENGINE.....

KWA UCHUNGUZI MDOGO NILIOUFANYA NIMEGUNDUA KUWA VIJANA WENGI WA MJINI HAWANA NIDHAMU KABISA KATIKA MFUMO MZIMA WA MAISHA YAO...YAANI WANAISHI KWA SABABU WAPO HAI.....

VIJANA WENGI WENGI BADO WANAISHI MAISHA YA KUFIKIRIKA....WENGI BADO WANADHANI KUWA MAFANIKIO NI KITU KINACHOZUKA TU KAMA BOMU........
WANADHANI KUWA MAFANIKIO YA MTU NI KUDRA TU ZA MWENYEZI MUNGU BILA YA JUHUDI.....HAWAJITUMI WALA KUHESHIMU VIPATO VYAO.......

NI AINA YA MAISHA AMBAYO HAYANA MBELE WALA NYUMA.....
 
Mbali sana mkuu unawazidi sema wao wanakuzidi labda zile gari zao za mkopo.....
Hivi hujajiuliza kwanini Masanja hakutumia mfano wa Walimu ili kufikisha ujumbe wake ??
Ngoja anajiweka tu kwenye spotlight ,siku wakianza kumchimba ndio ataelewa madhara yake
 
Waalimu na polidi wetu nao waache kazi wakalime? Kwa sababu wanalipwa chini ya hiyo laki 5
 
Back
Top Bottom