Laki tano tu unaweza badilisha historia

Laki tano tu unaweza badilisha historia

[emoji102] [emoji102] [emoji102] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Sikuwahi kudhani masanja ni mpuuzi kiasi hiki, kuna wazazi wa watu wanalipwa chini ya hiyo laki tano na wanasomesha watoto na wanategemewa na jamii zao, kupata kwako isiwe dharau kwa wenzako huyo aliyekupa hashindwi kukunyang'anya usidharau wasio nacho bwege wewe
Uwenda haujamuelewa masanja....
 
nashangaa watu wanachangia wanasema ukweli tupu,sijui kuna ukweli gani hapo-life is all about choices and division and specialization of work.usitake kila mtu afanye kama unavyoona wewe hata kwenye kilimo kuna uncertainty nyingi-mfano mabadiliko ya hali ya hewa.
vip ufanikishe na upate fedha za kutosha si lazima utazipeleka bank,kama hamna bank teller wa kukuhudumia?,maisha ni kutegemeana
 
Masanja kaongelea kipato na mahitaji watu wengi wanahitaji maisha mazuri ila kipato chao ni kidogo sana
Kulima ni kuzuri ila 500k haitoshi kulima
Ukiwa na hela yakutosha utashinda
 
watu wote wanapenda kutajirika na kuwa na maisha mazuri lakini siyo kazi rahisi kama anavyofikiria. Je,ukienda kulima kilimo cha matiki maji au maharage alafu mabadiliko ya hali ya hewa yakakuadhiri? Je,bank teller akienda kijijini kulima,huduma za kibenki mtazipatia wapi na nani atawahudumia na kuwatunzia hela zenu?
Je,unadhani kwamba bank teller ndo mwenye kipato kidogo kuliko wote? kwa nini asingewaambia wasaidizi wa ndani wapige kazi kwa miezi kadhaa kisha wakishapata hiyo laki tano warudi kijijini wakalime?
Ukweli ni kwamba wote tunategemeana na itabaki kuwa hivyo.
anawadharau bank tellers na wote wenye kipato cha chini paipo kujua kuwa hata matajiri wakubwa zaid yake pia wanamcheka yeye.

Nakubaliana na wewe kiongozi. What is good for you or has worked for you, may not necessarily be good or work for your colleague. Maisha ndivyo yalivyo. Kila mtu ana namna yake na itaendelea kuwa hivo. Kikubwa tusidharauliane kwa vipato. Maisha ni uamuzi na uchaguzi. Kama umefanikiwa wewe mshukuru Muumba wako kwa kukuchorea mipaka ya upendeleo. Hata huyo Bank teller ana malengo na maono. If he/she can take his children to school and feed his family.kwakwe yanaweza kuwa ndo malengo yake aliyojiwekea. I mean hakuna standard index ya mafanikio. Everyone defines his/her own success.
 
Laki tano ni nyingi. Kwa mtaji wa laki2 tu ukipeleka shamba unafanikiwa kabisa. Tatizo watu wanapenda utozi na usistaduu mjini.
 
View attachment 328257

SHULE BILA ADA:

Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

Je laki 5 yako, unafanyia nini?

#letitshine

aliyempandisha ndo atakae mshusha akili haziko sawa ashukur yy kapewa za kujitambua
 
Nakubaliana na wewe kiongozi. What is good for you or has worked for you, may not necessarily be good or work for your colleague. Maisha ndivyo yalivyo. Kila mtu ana namna yake na itaendelea kuwa hivo. Kikubwa tusidharauliane kwa vipato. Maisha ni uamuzi na uchaguzi. Kama umefanikiwa wewe mshukuru Muumba wako kwa kukuchorea mipaka ya upendeleo. Hata huyo Bank teller ana malengo na maono. If he/she can take his children to school and feed his family.kwakwe yanaweza kuwa ndo malengo yake aliyojiwekea. I mean hakuna standard index ya mafanikio. Everyone defines his/her own success.
What a word! Mkuu umeongea vema Sana,nilijua nakuja kukuta upupu wa Masanja mwenyewe. Kumbe ni mtu mwingine tofauti. Hongera Sana lkn mwajina wako hakufikiria hivyo.
 
ImageUploadedByJamiiForums1457508188.148735.jpg


Ukisoma iyo paragraph ya mwisho inajieleza kabisa kuwa masanja mkandamizaji katolewa ka mfano na mwandishi,,

guys mnasoma post kabla ya kuchangia au mnarukia tuh uzi na kuanza kuchangia?mbona mada inajieleza kabisa wakuu?
 
hawa ndio tulitakiwa tujue source za utajiri wao wasikimbilie kutakasa pesa tu,eti kilimo kilimo !!upuuzi tu mtu unatoa ushauri kimajungumajungu nani ataupokea zaidi ya kukuona kimeo tu,kwanza hapa bongo wengi tu tunasindikiza maisha hata ni hizo bmw x6 zenu,ikipiga enino ya kiuchumi hapa tunaanza kutafutana
 
Kila anayepata basi hugeuka mwalimu wa wasiokuanacho
 
Tatizo watu wengi wanapenda kujisingizia hata kwa sababu za kijinga!. Hata ushauri mnabisha?!
 
Back
Top Bottom