Kwenye maisha usije kumdharau mtu

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Aug 10, 2021
2,035
2,686
Nakuja ifuatavyoooo...

Nasema tena kwenye haya maisha usije mdharau mtu,nakumbuka kipindi tukiwa wa dogo, msimu wa kufunga shule kwa ajili ya likizo ya December wazazi walikuwa wanatupeleka moshi kwa ajili ya kula Christmas maeneo ya machame, sasa kipindi hicho tukiwa huko machame kijijini watu walitushanga tulivyokuwa tunapendeza, sisi tuliwaona watu waajabu na kuwadharau mbona wachafu tena miguuni hawajavaa hata malapa,wamepauka, nguo chafu tena vimechanika chanika kweli tuliwadharau sana.

Wale tuliowadharau tukiwa wadogo leo hii, wamejenga huko kwao majumba ya ajabu, wanamaisha manzuri sana, sasa hivi wananishanga mimi mbona sijawahi kwenda ulaya,leo hii mimi ndo naonekana mshamba. Daah!

Mwezi wa 8 katika pita pita zangu maeneo ya mabibo mwisho, pembezoni mwa barabara ya treni kuna maeneo ya wazi,ambayo yapo tu yamezungukwa na majani, sasa nilimkuta mzee mmoja analima tena mchana wa jua kali sana, kila mtu alipokuwa anamuona analima walimcheka na kusema pakame hivyo kutaota nini? Wengi walimcheka sana.mini mwenyewe nilimcheka.

Juzi nimepita kwenye maeneo hayo, nimeshangaa kukuta bonge la bustani limekubali sana, mzee kapanda matembele, mboga ya maboga, bamia na mchicha bustani imekubali sana, tena nimewakuta wa mama wanavuna nimeshangaa sana, nikajisemea sitakaa mdharau mtu hata kama yukoje, maana alichokiumba mwenyezi MUNGU hakukosea.

Nawakaribisha kwa maoni na mchango wenu ndugu zangu.

ONE TIME,
ONE FOR THE ROAD.
APPROXIMATELY, ONCE AGAIN
 
Mm mwenyewe nilikuwa nafaulu sana darasani, kila mtu alidhani nitakuja kuwa na mafanikio sana na mm nikawa nawaona ambao hawafanyi vizuri ( wanafeli) watakuja kupataje pesa.
Baada ya miaka 30 sasa, wao wapo mbali sana kimaisha na wanaishi mijini maisha mazuri. Mimi nipo kijijini dhiki haziniishi.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Komaa tu utatoboa
 
Mimi huyu mo deji nilikuwa namuonea shuleni.ilikuwa akija shule na baskeli yake nachukua kibabe naendesha.leo hii similiki ata pagala mwenzangu anamiliki timu kubwa kbs.daahh
😆😆😆😆😆 sio timu tu jamaa billionaire now
 
Back
Top Bottom